Mila na desturi ziwakomboe wanawake kuondokana na madhira magumu wanayoyapitia

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Katika jamii nyingi vikwazo vingi kwa wasichana na wanawake vinaanzia kwenye mila na tamaduni zisizo na manufaa kwa jamii isipokuwa ukandamizaji tu kwa hasa kwa hii jinsia ya kike ambapo ukienda baadhi ya jamii fulani ni kwamba ili mwanamke aojione anapendwa ni lazima japo apigwe na mume wake bila ya kosa lolote.

Sasa ukiangalia kwa umakini utaona ya kwamba hizi mila na desturi zinahamasisha vitendo vya unyanyasaji na ukatili chungu mzima jambo lisilo jema kwa wanawake wote. Na mengine ambayo mila na desturi zetu inatakiwa kuyatupilia mbali ni kama yafwatayo

1.kushinikizwa kufunga Ndoa za utotoni
2.Kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
3.Ukeketaji kwa wanawake
4.Ukosefu wa haki zake yeye kama mwanamke
5.wasichana Kukosa elimu
6.ujando na unyago

Hivyo hatua zichukuliwe Elimu zitolewe kwa jamii Kwa kuwa hayo ndo Mambo yanayomkandamiza Mwanamke katika jamii zetu
Asante.
 
Kwa umoja tunaweza kusaidia hili hasa kwa kutumia njia rafiki kuwafikishia ujumbe wananchi. Hili litafanikiwa kwa kuifikia moja kwa moja jamii inayokumbwa na madhira husika..njia za kufanya hivi ziko nyingi lakini ninalo wazo ambalo kwa kushirikiana na wadau wa haki za bindamu tunaweza kulifanikisha.
 
Ahaa sawa kiongozi kwa hakika nakuunga mkono katika hili na endapo tutafanya hivyo tutaweza kudhibiti hali zote zenye ukatili katika jamii yetu ambapo itasaidia kuwakomboa wake kwa waume wanaopitia vipindi hivi vigumu. Pia niseme Asante sana kwa mchango wako bila shaka tupo pamoja.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hapa kama kuna mtu kutoka WILDAF/WLAC/TAWLA and the like tunaweza kujadili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom