Mila na Desturi na Dhulma za familia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mila na Desturi na Dhulma za familia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tumsifu Samwel, Mar 26, 2009.

 1. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwenu Ndugu wanajamii,

  Kabla ya yote naomba kuelezea historia yangu kwa kifupi.

  Mimi ni kijana wa umri wa miaka 24, ni muenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro natokea kijiji cha Machame Nkuu. Kwenye familia yetu tupo watoto watatu mimi nikiwa ni mtoto wapili, mnamo mwaka 1988 Baba yetu mzazi alifariki.


  Kabla Baba hajafariki maisha yake yote alikuwa anaishi Moshi mjini hakuwa na utaratibu wakutembelea kijijini kwake. Hivyo pale kijijini alikuwepo kaka yake pamoja na mzazi wake yaani babu yetu.Baada ya miaka kadhaa ya Baba kutokufika kijijini kwake kaka yake alipata matatizo yalio mpelekea kufungwa hivyo Babu akawa hana mtu wa kumtunza,kwa kuwa babu alikuwa hana nguvu Ya kufanya kazi ya kumpatia chakula.Ili mlazimu babu kuuza mashamba yake kidogo kidogo ili apate pesa ya kula.

  Baada ya miaka mingi kupita Baba mkubwa alipata msamaha wa rais na alipo rudi kijijini alimkuta Baba yake (Babu) ameuza sehemu kubwa ya mashamba baada ya muda babu alifariki. Kutokana na mila za kichagga watoto wakiume ndio wanao risishwa ardhi baba mkubwa alijigawia sehemu kubwa ya mashamba na kubakisha sehemu ndogo ya kijishamba ambapo ndipo kwenye nyumba ndogo ambayo alikuwa anaishi babu.

  Kwa mila za kichagga mtoto wa mwisho ndiye ana rithishwa sehemu hiyo kwa kuwa baba alikuwa mtoto wa mwisho hivyo baba mkubwa alimpatia baba sehemu hiyo na kumuambia wewe nimekupa sehemu hii ndogo kwani wewe ulizamia huko mjini na kumuacha baba(babu) anauza mashamba huku…

  Naomba nije kwenye dhumuni lenyewe la waraka huu,

  Baada ya Baba kufariki ilitulazimu kurudi kijijini kwetu Machame Nkuu na tukaanza maisha mapya ya pale kijijini kwetu.Mama akawa ana jishughulisha na maswala ya kilimo pamoja na kufanya vibarua vya kulima kwenye mapori ya watu.alifanikiwa kutusomesha elimu ya msingi
  kutokana na shughuli hizo. Wakati tukiendelea kuishi pale kijijini baba mkubwa alikuwa anamyayasa sana mama kwa kuingia shambani kwetu kuchukua mazao ya kahawa na mengineyo ingali mama yeye ndiye mwenye shamba na ndiye anayelitunza na kulima mazao yote.

  Nakumbuka mwaka 1990 nikiwa na umri 6 mama alikata mti shambani kwetu kwa jili ya kujengea banda la kuku baba mkubwa alipita pale na kukuta huo mti umekatwa alikasirika sana na kumwambia mama nani kampa ruhusa ya kukata mti huo baba mkubwa alichukua panga na kutaka kumkata nalo mama alikimbia na kurudi kwa wazazi wake,Baada ya muda kiliitishwa kikao cha familia na mama kurudi tena kwenye mji wake.
  Baada ya sisi kukua tuligundua kumbe mama alikuwa anayanyaswa na baba mkubwa ili akimbie pale nyumbani amuachie lile shamba ili aweza kulichukua yeye baba mkubwa hivyo dhamira yake ilishindikana kutokana na msimamo wa mama.

  Mwaka 2004 alitokea kijana mmoja ambae wanadai ni mtoto wa baba amabeye alizaa na mwanamke mwingine hivyo baba mkubwa alivyo mwona kijana huyo alifurahi sana na kusema bora umekuja kabla sijafa ili niweze kukupa shamba lako.

  Baba mkubwa alimchukua na kumpeleka kwenye shamba letu na kumwambia sehemu hii ndio yako hivyo utajenga hapa. Pasipo kumshirikisha mama, mama alikasirika sana na kumwambia huwezi ukamrisisha mtu nisie mjua shamba langu,Mama akaitisha kikao cha wana familia na kuniita na mimi.

  Tulifanya kikao na kumuhoji yule kijana kwamba yeye amekuja hapa kijijini kwa nia ya kutaka shamba au ni kwa nia ya kuja kusalimia alijibu nimekuja kusalimia.Basi nika gundua ni njama tu ya baba mkubwa kutaka kuchukua sehemu hiyo kwa mkumtumia kijana huyo ili kijana huyu atakapo rithishwa sehemu hiyo baba mkubwa aje kuinunua koka kwa huyo kijana,tangu hapo wakawa ni watu ambao wananichukia sana hadi ilifikia wakati kawapigia watoto wake simu na kuwaeleza kuwa nimemtukana sana kwenye kikao kitu ambacho sio kweli.hali ambayo ilinijengea chuki na watoto wake.


  Sasa hivi majuzi wameleta tena jambo lingine wanataka kupitisha barabara ya kwenda kwenye shamba lao ambalo lipo nyuma ya shamba letu ingali wao walikuwa na sehemu ya kupitia kwenda shambani kwao ila wamejenga hapo na kuzungushia ukuta sasa wanataka kupitisha barabara kwenye shamba letu na mimi nimemwambia mama nikitu ambacho hakiwezekania kuwapa barabara kwenye shamba letu ingali shamba letu ni kasehemu kadogo tu je sisi tutajenga wapi endapo wao watapitisha barabara hapo?

  Basi kutokana na kauli yangu hiyo jana tarehe 23/3/09 mke wa baba mkubwa amemfuata mama nyumbani na kumtukana sana na kumuambia kuwa lazima wapitishe barabara hapo na kumwambia mama asipo angalia atamfungia nje yaani atafunga nyumba yetu mama akose sehemu ya kuishi.

  Leo tahere 24/3/09 mtoto mwingine wa baba mkubwa amemfuata mama na kumtishia na kumwambia asipotoa hiyo barabara ata mpasua au kwa maana nyingine ata mdhuru mama,kitu ambacho kimempa mama wasi wasi sana hadi ana niambia ana taka kuhama mji. Ndugu zangu naomba msaada wenu wa ushauri maana naona wataniulia mzazi wangu huyu kwa presha.

  Huku na mzee wa ukoo akamfuata mama na kumwambia kuwa ametumwa na mtoto wa baba mkubwa ambae ndiye amepewa hilo shamba ambalo lipo nyuma ya kiwanja chetu anataka barabara hapo na endapo mama atakataa basi huyo mzee ataitisha kikao cha ukoo kilazimishe mama kutoa sehemu hiyo ya barabara.Je ndugu zanguni hii ni haki kweli kwa kitendo hicho hawa ndugu zangu wanafanya ?

  Kwa upande wangu naona ni unyanyasaji kabisa,watapitisha vipi barabara kwenye sehemu yetu ingali wao walikuwa na sehemu yao ya kupitia ila wamejenga kama sio unyanyasaji ni nini? Ndugu nina mpango wa kumshitaki mke wa baba mkubwa kwa kumtukana mama na kumtishia maisha yake .
  Na pia nina wasi wasi na hawa watu jinsi ninavyo wajua wanaweza kumfanyia mama kitu kibaya hivyo nina wasi wasi sana na jambo hili, ndio maana nataka kuripoti swala hili polisi. Je ndugu zangu nitakuwa nimefanya kosa kwa jambo hili ambalo nakusudia kufanya maana nimechoka na manyanyaso ambayo ana yapata mama.

  Na jua hapa kuna watu wa aina mbali mbali waki wemo wana sheria naombeni muongozo wenu ndugu zanguni nifanye je?,pia kwa wale ndugu zangu hapa wachaga naomba mniambie hizi ndio mila za
  kichaga zinavyo kwenda au ni unyanyasaji?
  Nategemea mtanipa ushauri mzuri ambao utanisaidi maana hili jambo linanisumbua sana mpaka nashindwa kufanya vizuri kwenye masomo yangu.

  Nategemea kusikia mengi mazuri kutoka kwenu.
   
  Last edited by a moderator: Mar 26, 2009
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  sasa sii kama hapatoshi sii mhamie sehem zingine za jamhuri? Morogoro, Tanga kuna mapori tu!!

  Kwa nini mnataka kubanana hapo?
   
 3. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #3
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0


  Awali ya yote naomba Uchange kichwa cha posting yako, KISA HIKI KINAWEZA KUTOKEA KWENYE KABILA LOLOTE hakina uhusiano na kabila fulani.
  Kosa lilianza kwenu kutotembelea kijijini kwenu, baba/babu yenu anakosa mtu wa kumtunza mpaka anauza mashamba? angeuza yote kwa kukosa msaada kwenu ungekuwa unatoa stori gani hapa?
  MIMI nadhani hii ni matokea ya manunguniko aliyoondoka nayo babu wa watu.

  CHA MSINGI NENDENI KANISANI/MSIKITINI/KWENYE MAWE kulingana na imani yenu tubuni kwa mola fanya sala ya mapatano, kaeni kwa amani Mwenyezi MUNGU ATAKUWA UPANDE WENU.
  AMEN
   
 4. u

  urassa Member

  #4
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwashe, hayo mambo yapo sehemu nyingi, ila chukuwa taadhari kwa kuyafikisha kwenye vyombo husika.Lakini tumesikia malalamiko ya upande mmoja hatujui wa pili, waweza kukuta baba mkubwa yupo sahihi pengine anahitaji jasho lake la ziada alilotumia kumtunza babu yenu wakati nyie mnaishi town
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono Kanda2 ..nilipoona kichwa cha habari nilidharau hata kusoma maudhui maana nilijua ni yale yale ya ukabila.
  Mtoa mada ushauri wa bure ni kuwa siku nyingine ukitaka usaidiwe tena kwa haraka usiweke vichwa vya habari vyenye kugawa watu... nenda moja kwa moja kwenye kiini.Ukweli ni kuwa una hoja nzito au una ishu inayohitaji msaada ila umekosea kuiweka.Unapaswa kuzingatia yafuatayo katika kutafuta haki yako:
  1. Ni bahati mbaya sana sasa nyie mnalipa kwa makosa aliyoyafanya baba yenu - kutelekeza shamba lake kijijini na kuzamia mjini.Kama unavyojua- asiyekuwepo mara nyingi husahaulika na lake linakuwa halipo.Hata kisheria ukitelekeza ardhi kwa kipindi fulani unapoteza haki kwenye ardhi hiyo.( kwa wale wenye ardhi zilizokaa bure - mnaohodhi mnatakiwa kuweka ushihadi kuwa mpo au mtarudi)
  2.Hilo la kunyanyaswa na huyo baba yenu mkubwa pengine ( sina uhakika) alipokuwa kifungoni,nduguye ambaye ni babako naye hakuijali familia aliyoiacha nyuma, au wala hakujali kwenda kumtembelea gerezani.Na kwa binadamu wengi, muosha huoshwa! Anawafanyizia hayo yote kama kisasi.
  3. Bila kuingia kwa undani sana,naungana na Mzalendohalisi kuwa maisha yapo popote na si lazima mkae hapo Machame Nkuu... kwanza wewe sasa ni kijana wa umri wa kutosha..toka katafute maisha pengine utafanikiwa na hata utawasaidia ndugu na mamako.
   
 6. R

  REOLASTON Member

  #6
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo aliyepewa hicho kiwanja nyuma ya nyumba yenu hana sehemu nyingine ya kupitisha barabara? kama hana mwambieni mpime hiyo sehemu anayotaka kupitisha halafu ariplace upande mwingine. yaani mbadilishane. Na wewe nakushauri uende kijijini ukaonane na wazee msuluishe hayo mambo kabla hujaenda Police
   
 7. M

  Makfuhi Senior Member

  #7
  Mar 26, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inaelekea hivi vitu ulivyoandika umesimuliwa kwa sababu havilingani na umri wako. Uliza vizuri
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Jambo hili litakusumbua kama na wewe unadhani ni lazima kuishi moshi, ila kama mmoja hapo juu alivyokushauri kuwa po pote panaweza kufaa basi angalia wazo hilo.
  Mimi na wadogo zangu tulifanyiwa hivyo( sisi kaka yake baba kiukoo amejenga ktk shamba la bibi, babu alitusaliti mchana kweupe) lakini tuliamua kukaa kimya na tukanunua shamba lingine kubwa zaidi ili kuepusha shari.Sijui ni Mungu au nini,sasa hivi tuko huru na tuna mashamba mazuri yasiyo ya urithi. Mimi na wadogo zangu tuliangalia nini cha msingi kwa wakati ule; tukachagua shule kwanza na mengine baadaye. La pili je hakuna njia mbadala ya kupata shamba lingine,tukaona ipo.

  Mdogo wangu,usiangalie hicho kipande kidogo cha ardhi,wape njia,achana na ugomvi wa kiukoo/familia,ugomvi huo hautakaa uishe( wachaga na ardhi),mshauri mama awe mpole,kwa maelezo yako mko peke yenu. Ukimaliza masomo tafuta ardhi kwingine kwa kadri ya uwezo wako.
   
 9. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #9
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa kuna mapori mengi sana,kama ulivyo sema ila ndugu yangu kwa nini niache haki yangu wachukue watu? je nitakapo kuwa na watoto wangu wakaniambia kuwa wanataka kwenda kuona sehemu niliyo tokea nita wapeleka wapi?

  je ndugu yangu we unaona ni bora ni waachie ?
  je mzazi wangu ni mpeleke wapi? ingali me bado na soma na sina kipato cha kuniwezesha kununua kiwanja na kujenga kwa sasa?
   
 10. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #10
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Shukran ndugu yangu, kuhusu kichwa cha posting yangu naona ni sahihi kabisa maana sisi wachaga tumekuwa ni watu wa dhuluma sana hasa kuhusu maswala ya ardhi kiasi kwamba watu wanafukia atua ya kutoana roho.

  Na shukuru kwa ushauri wako.
   
 11. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #11
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hivi ni Duluma au Dhuruma?

  Teheee hivi wakati ule ulimuuliza mzee akupeleke? au umejifunza jambo. piagania haki yako, suala la barabara ni la maongezi.

  VIPI USHAURI WA KANISANI HAUJAKUINGIA????
   
 12. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #12
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ekambee Urassa, umenifurahisha sana ndugu yangu ,kweli jasho lake alikwisha kulichukua toka mwanzo kabisa na hatuja lala mika kwa hilo maana yeye alichukua hekari 3 wakati sisi tuna nusu heka tu na wanataka hicho hicho kidogo wakimege tena wakati alikwisha jimegea sehemu yake kubwa na hakuna aliye lalamika kwa hilo.

  ndio mmesikia malalamiko ya upande mmoja tu na kama mimi ningeweka malalamiko yangu yote hapa ungestajabu mwenyewe,pia mtoto wake yupo humu Jf, anaweza kuwakilisha malalamiko yao hapa kama anayo, sidhani hata kama anayo.
   
 13. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #13
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni Dhuluma na sio Duluma.

  Ushauri wakanisani umeniingia sana akilini,mwaka 2004 tulifanya hivyo na kumuita mchungaji wausharika kwenye kikao cha wana ukoo wajili ya kutatua tatizo ili na sasa limejirudia tena ndio maana nimeona nibora nika chukua hatua za kisheria japokuwa ndio nita zidisha huasama zaidi.
   
 14. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #14
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ahsante kwa kunikosoa hapo nimekubaliana nayie wote mlio ni kosoa kwa kichwa cha posting yangu.

  1.Baba yetu hakutelekeza shamba kama umenielewa vizuri, ni kwamba wakati huo yupo mjini bado alikuwa hajapewa ardhi yake,baada ya babu kufariki dunia ndio walijigawia sehemu na ndio baba mkubwa akajimegea sehemu kubwa ya shamba hilo kwa sababu yeye ndiye alirudi na kumtuza tena babu na hakuna aliye lalamika kwa hilo, na baada ya kugawiana mashamba baba alijenga pale,baada ya mwaka ndipo alifariki na sisi kurudi pale Machame, hivyo hakutelekeza shamba lake but alimtelekeza baba yake wakati ule.

  2.Tunapo sema alimnyanaysa mama ni kwamba alimuingilia kwenye mahamudhi yake,na kutaka kuendesha mji wetu kama yeye ndio mwenye hadi alifikia wakati anamfukuza mama kwenye mji wetu je hayo sio manyanyaso? sisi hatukutaka huduma yake yoyote bali tulitaka amuashe mama afanye anavyo taka juu ya mali za mume wake.

  3.Maisha ni popote na mimi sina mpago wakuishi pale ila ni lazima ni jenge pale nyumba yangu ya kufikia wakati nikienda kutembelea huko,siwezi acha mali yetu,mama yangu kwa sasa anaishi pale je tumuamishe kwa sababu ya hawa ndugu zangu wenye tamaa ya ardhi?
   
 15. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #15
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyu aliyepewa hicho kiwanja anayo sehemu nyingine ya kupitisha barabara,na hapo anapotaka barabara ipite ndio sehemu mimi nategemea wakati wa usoni ni jenge hapo nyumba yangu,hata wakisema tupime alafu wa-replace sehemu nyingine itakuwa vigumu kwa kuwa watakuwa wamearibu kiwanja changu hivyo itakuwa shida mimi kupata sehemu nzuri ya kuweka nyumba yangu.

  Ndio kusudio langu kwenda kijijini, kuhusu kusuluisha tumeshafanya hivyo sana kama umenielewa vizuri kwenye maelezo yangu ya mwanzo.


  Ushauri wako umenikuna sana ndugu yangu ubarikiwe sana.
   
 16. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #16
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kweli baadhi nime simuliwa kama ya babu alitelekezwa na n'k, kuhusu haya mengine nimeshuudia mwenyewe kabisa,ebu angalia tukio la mwaka 1990 nikiwa na miaka 6 nilishudia mama anakimbiwa na pangu huku amembeba mdogo wangu wa umri wa miaka 2 mgongoni.

  hayo nilio simuliwa nimbele ya wana ukoo hayo mambo yali semwa.
   
 17. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mangi pigania haki yako Meeku!! hadi kieleweke!

  Fungua kesi Ardhi Moshi kuna mabaraza ya ardhi kama unaona Ukoo unakuonea.. it will take time ila haki itapatikana!
   
 18. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #18
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ubarikiwe sana ndugu,ushauri wako nimeupokea japo kwa shingo upande,ila kuhusu kwa upande wenu ni heri yenu mlifanikiwa kusoma n'k mimi ndio nimejisimamisha kama mimi maana baba alituasha kwenye hali mbaya sana kama nilivyo andika mwanzo kuwa ilimlazimu mama kufanya vibarua ili tuweze kusoma angalau elimu ya msingi.

  nimekuelewa vizuri sana ndugu yangu asante sana.
   
 19. Mchola

  Mchola Member

  #19
  Mar 26, 2009
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu,
  Nunua amani kwa gharama yoyote na sio kihamba kwa gharama kubwa. Mwambie mama akubali baranara ipite pale kwenye shamba lenu hata kama bado ni dogo. usipofanya hivyo vita itaendelea na hapatatosha!!
  Mimi pia nimeipitia hiyo hali. Baba alipofariki mama mdogo na wanae waliturusha shamba la ekari 10. Tulisamehe na tukajitahidi kusoma na sasa tuna mashamba mara kumi ya hilo. watoto wa huyo mama ni wavuta bangi na wachovu wakubwa!!! Achana na kihamba hicho wachukue kama watatjirika!!
   
 20. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #20
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ha!ha!ha! kupigania haki yangu ni lazima ndugu yangu kwani ni kilala hakuna atakaye pigania haki yangu pasipo mimi mwenyewe.swaka la kesi kwa mahakama zetu hapa Bongo, utafuatilia mpaka unaingia shimon,
  ila nipo mbioni kaka!
   
Loading...