Mil. 90 Zinahitajika kuokoa Uhai wa Dr. Ulimboka

Jopo la Madaktari wanaomtibu Dr. Ulimboka katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili wamesema zinahitajika shilingi Milioni Tisini (Tsh.90,000,000) kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Dr. Ulimboka. Madaktari wanasema Dr. Ulimboka ana matatizo ya Ini na kuwa Matatizo hayo ya Ini hayawezi kutibika katika hospitali yetu ya Muhimbili. Jopo la Madaktari limesema mpaka sasa zimepatikana Tsh. milioni 40 zilizochangwa na Madaktari. Dr. Ulimboka anahitaji kusafirishwa kwenda nchini India ambako anaweza kupatiwa matibabu stahiki.

Nilikuwa napendekeza Chama Cha Madaktari (MAT) au kikundi kingine kuratibu zoezi la kukusanya michango kutoka kwa wananchi wenye nia njema na wanaomtakia kupona Dr. Ulimboka.

Pamoja na mdai Mengine Madaktari wanasema kuwa “Sisi madaktari kwa umoja wetu, tumechoka kushuhudia Watanzania wakipoteza maisha kwa magonjwa tunayoweza kuyatibu, kufanya kazi katika mazingira magumu huku kukiwa hakuna mipango ya kuboresha mazingira ya kazi, kukosekana kwa dawa na vifaa tiba.”

Ulaji huo
 
Mil 90 kuokoa mtu mmoja???

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
Yeah hata hiyo ni kidogo sana fikiria safari yenyewe kwanza pia INI ni very complex Organ upasuaji wake ni mgumu sana na unahitaji vifaa maalumu na skill maalum pia!!
 
Tutachanga, lakini sasa kwa nini serikali isimplipie kama raia wa Tanzania (siyo kama Dr Ulimboka) wakati wao wamekuwa kila siku wanakimbilia huko India?

Yaani serikali hii hii iliyomtenda haya bado igeuke imtibu tena? wao wanaomba kila siku afe ili mchezo ukamilike!
 
Kiongozi, soma hapo chini, kuna uzi umewekwa sasa hivi una number za kuchangia.
MAELEKEZO RASMI YA KAMATI KUHUSU UCHANGIAJI WA FEDHA ZA MATIBABU YA DR.STEVEN ULIMBOKA.

Baada ya majadiliano kati ya familia ya Steven Ulimboka,kamati ya jumuiya ya madaktari na MAT.Zifuatazo ni namba za mawakala zitakazotumika kuchangia.
MPESA 31915
TIGOPESA 05416
.
CHITAGE.
nimejaribu kuchangia kwa kutmia hii ya mpesa inasema umekosea namba ya simu. kuna kitu nakosea au haijakuwa activated?
 
nimejaribu kuchangia kwa kutmia hii ya mpesa inasema umekosea namba ya simu. kuna kitu nakosea au haijakuwa activated?

mkuu hii ni namba ya wakala hivyo unachofanya ni kutoa pesa ukiombwa namba ya wakala ndiyo una weka..
 
Kuna nyuzi nyingine wameandika million sitini na nane (68,000,000) hapa tisini (90,000,000). Bongo Bingo.

wewe gamba,
hujalazimishwa kutoa na kwa maoni yangu wewe kama ccm mliohusika na unyama aliofanyiwa ulimboka naomba mkae pembeni, muendelee kutafuta mwingine wa kuua maana huyu imegonga..
 
Nawaomba wahusika waeleze vizuri jinsi ya kuchangia - naona kama kuna contradictions kidogo. Tatizo kubwa tunalokuwa nao tulio wengi ni kukosa kuamini. Tunao uwezo mzuri wa kuchangia kitu muhimu kama hiki lakini lazima tuelimishwe vizuri. Ninachokimaanisha ni kwamba litolewe tamko na mtu maalum anayehusika na kutupa uhakika wa wapi tutume pesa. Tujulishwe na maendeleo kuepusha watu wenye nia njema kujiaminisha kwamba 'labda wameishachangia wa kutosha na pesa imetimia'. Tutaikomboa nchi yetu kwa namna hii hii - mshikamano wa kweli.
 
Ngoja niwahi zangu MPESA nitume hyo hela tumwokoe ndugu yetu Dr Uli na Mungu atamsaidia
 
WanaJF hasa madakitari mlio hapa ukumbini,
Ninapenda kuwafahamisha kuwa mimi ninaurafiki na uhusiano wa kikazi na madakitari wa hospitali maarufu Marekani na ningependa kuwauliza kama wanaweza kusaidia katika matibabu ya Dr. Ulimboka marekani badala ya kupelekwa India. Kitu ambacho sielewi na ningependa kujua ni hayo maandalizi ya kwenda India yamefikia wapi na vile vile kama kuna mtu yeyote mwenye namba ya simu ya dakitari yo yote kati ya wanaomtibu Dr. Ulimboka pale Muhimbili. Hata simu ya MOI itasaidia. Nina uhakika nikiwaonyesha hii picha ya doctor na kuwapa sababu iliyopelekea haya kutokea watakuwa tayari kusaidia. I am confident that USA hospital will do better than Apollo, but of course, which route to follow will depend on how urgently the treatment is required.

Jopo la Madaktari wanaomtibu Dr. Ulimboka katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili wamesema zinahitajika shilingi Milioni Tisini (Tsh.90,000,000) kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Dr. Ulimboka. Madaktari wanasema Dr. Ulimboka ana matatizo ya Ini na kuwa Matatizo hayo ya Ini hayawezi kutibika katika hospitali yetu ya Muhimbili. Jopo la Madaktari limesema mpaka sasa zimepatikana Tsh. milioni 40 zilizochangwa na Madaktari. Dr. Ulimboka anahitaji kusafirishwa kwenda nchini India ambako anaweza kupatiwa matibabu stahiki.

Nilikuwa napendekeza Chama Cha Madaktari (MAT) au kikundi kingine kuratibu zoezi la kukusanya michango kutoka kwa wananchi wenye nia njema na wanaomtakia kupona Dr. Ulimboka.

Pamoja na mdai Mengine Madaktari wanasema kuwa “Sisi madaktari kwa umoja wetu, tumechoka kushuhudia Watanzania wakipoteza maisha kwa magonjwa tunayoweza kuyatibu, kufanya kazi katika mazingira magumu huku kukiwa hakuna mipango ya kuboresha mazingira ya kazi, kukosekana kwa dawa na vifaa tiba.”
 
MAELEKEZO RASMI YA KAMATI KUHUSU UCHANGIAJI WA FEDHA ZA MATIBABU YA DR.STEVEN ULIMBOKA.

Baada ya majadiliano kati ya familia ya Steven Ulimboka,kamati ya jumuiya ya madaktari na MAT.Zifuatazo ni namba za mawakala zitakazotumika kuchangia.
MPESA 31915
TIGOPESA 05416.
CHITAGE.
Mshafanya ni dili la kupata pesa,eti milioni 90,kwa maana iyo yy ni muhimu sana kuliko awo raia wanaopoteza uhai kila aiku kwa ajili ya yy kuongoza migomo,pumbavu mkubwa,na akipona arudie tena,hili suala mm siafiki ata kodogo watanzania tuache unafiki.
 
Hivi watanzania wameifanya India kuwa ni tenderer wa kuwatibu! Hakuna matibabu sehemu nyingine duniani isipokuwa India tu? Je, ni wakazi wa dunia nzima wanatibiwa India au ni watanzania tu?

Bwana tunaenda india kwa sababu gharama ni ndogo na matibabu ni ya uhakika
 
Mshafanya ni dili la kupata pesa,eti milioni 90,kwa maana iyo yy ni muhimu sana kuliko awo raia wanaopoteza uhai kila aiku kwa ajili ya yy kuongoza migomo,pumbavu mkubwa,na akipona arudie tena,hili suala mm siafiki ata kodogo watanzania tuache unafiki.

unawaongelea watanzania gani?
Mbona huku vijijini wamekuwa wakifa kama mchwa kila siku bila huduma?

Serikali ya chama cha majambazi inawachangisha wanavijiji pesa kila mara kila mwaka ili wapelekewe huduma za afya lakini hakuna kitu ,maeneo mengi hata Dispensary hakuna,na pale palipo na jengo linaloitwa hospitali hakuna hata Panadol sasa hospitali ni jego au huduma.

Watu wangu wamewekwa kwenye mapango wala hapana asemae rudisha wewe ni mmoja wao.,
 
JAMANI KWA WALE AMBAO WANAONA TAARIFA HAIJAKAA VIZURI MAELEZO THABITI HAYA HAPA CHINI
TUJITOLEE KUMCHANGIA MATANZANIA MWENZETU COMRADE WETU KAMANDA WETU

Haya ni maelezo ya Dkt. Hobokela Stephen, kaka yake Dkt. Ulimboka Stephen.

Dear all,

Thank you very much for your candid support in this.

I would like to bring to your attention that we had a meeting this afternoon between myself and a team of specialist to discuss modalities of collecting contributions.

In order to efficiently coordinate contributions it was agreed to use m-pesa agent number 31915 belonging to Christine Hobokela and and tigo pesa agent number 05416 belonging to Hedaya Stephen Mwaitenda.

For those who want to send foreign currency (USD) please send to Dr. Hobokela Stephen, Stanbic Bank Tanzania Limited Account number: 024003849360, SWIFT CODE: SBICTZTX

The reason I'm sending this is because I have been asked several times to clarify on this and after consuling with MAT president, he advised me to provide this clarification.

Below are some steps on how to send money to m-pesa and tigo pesa:

M-pesa

1. piga *150# OK
2.Chagua 2, toa pesa.
3.Ingiza namba ya wakala ambayo ni 31915
3.Weka kiasi cha pesa unachotaka kuchangia eg 50000
4.Weka nambari ya siri - namba yako ya siri
5. Bonyeza 1 kuthibitisha muamala

Utapata ujumbe kuwa mefanikiwa kutoa pesa kwa Christin Hobokela

Tigo pesa

1. piga *150*01# OK
2.Chagua 3, kutoa pesa.
3.Ingiza namba ya wakala ambayo ni 05416
3.Weka kiasi cha pesa unachotaka kuchangia eg 50000
4.Weka nambari ya siri - namba yako ya siri
5. Bonyeza 1 kuthibitisha muamala

Utapata ujumbe kuwa umefanikiwa kutoa pesa kwa Hedaya Mwaitenda
----------------
Once again we thank you very much for your support.

Hobokela Stephen

Source: Call for donation/Njia za kuchangia ili kulipia gharama za matibabu ya Dkt. Ulimboka Stephen - wavuti
 
Weka namba ya simu, namba ya wakala haitoshi.
MAELEKEZO RASMI YA KAMATI KUHUSU UCHANGIAJI WA FEDHA ZA MATIBABU YA DR.STEVEN ULIMBOKA.

Baada ya majadiliano kati ya familia ya Steven Ulimboka,kamati ya jumuiya ya madaktari na MAT.Zifuatazo ni namba za mawakala zitakazotumika kuchangia.
MPESA 31915
TIGOPESA 05416.
CHITAGE.
 
FREEWorld: what has Chadema has to do with this? r u suggesting that Chadema was behind this tragedy? Or u r trying to shift our focus and start a 'blame game'? Pliz, stop playing politics and be sensible.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu nawaomba wanaoratibu zoezi la kukusanya michango wafanye matangazo ya kutosha,na ikibidi watumie radio na TV na kubandika matangazo hasa mikoani,maana watumiaji wa JF sio wengi ki vile,lakini unyama aliofanyiwa Dr Ulimboka umewagusa raia wengi,hata hapa Dar kuna watu hawajawahi kugusa computer lakini wanaweza kuchangia japo elfu mbili ahadi tano,sasa kama number za kuchangia ziko tu kwenye JF tunaweza kukosa fedha zingine za watu wenye mapenzi mema.kumbukeni jambo hili limewagusa watu wa kada mbali mbali.

Naomba pia tushirikishwe siku ya kumsafirisha ikibidi watu tujipange barabarani kumuaga,na ikibidi tkuwe na maombi maalumu kwa dini zote,naomba jambo hili liwe la wananchi madaktari wetu mtakuwa viongozi na waratibu wa zoezi zima,hivyo kwa mawazo yangu naomba wananchi tushirikishwe kwa hatua zote,kwa mawazo yangu napendekeza maandamano ya kumsindikiza dr akatibiwe,watu wako tayari,najua watajitokeza kumsindikiza jemedari wetu.wala hatuhitaji kibali cha polisi,na wala msikubali fedha kutoka serikalini,wala msikubali kusindikizwa na watu wa wizarani.
Mungu umtangulie Dr Ulimboka na wanaoratibu zoezi la kuchangisha fedha.
 
Back
Top Bottom