Mil 10 nilizodhulumiwa PPF sikuzaliwa nazo, nilizaliwa nikali Uchi kutoka tumboni mwa mama yangu

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,534
Baada ya kudhulumiwa jasho langu na PPF pesa zangu nilizozipata Kwa dhiki mno, pesa ambazo Serikali haikuchangia hata cent, hatimaye Nimeamua kupata faraja kutoka ktk neno la Mungu.

Na mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu tupu... Ayubu 14:1.

Mil 10 zangu, sikuzaliwa nazo, nilizaliwa nikali uchi na pia nitaondoka duniani nikali uchi.
Walionidhulumu pesa zangu laana i juu yao na kamwe hawataweza kujenga kiwanda hata kimoja Kwa ufanisi na kikadumu, kila kiwanda kitakachojengwa Kwa kutumia pesa ya dhuluma ya jasho la wanyonge lazima kitakufa.

Dhuluma ni laana, nao walionidhulumu pia wataondoka Duniani wakali uchi, hayo mabilioni yetu waliyotudhulumu hawataondoka nayo.
Mungu ni mwema na jina lake lihimidiwe.
 
Watajengea viwanda vya kufanyia tafiti za maganda ya korosho!
Hizo tafiti zitasimamiwa na mtu mmoja tu mwenye Ph.D ya hayo mavitu!
 
Baada ya kudhulumiwa jasho langu na PPF pesa zangu nilizozipata Kwa dhiki mno, pesa ambazo Serikali haikuchangia hata cent, hatimaye Nimeamua kupata faraja kutoka ktk neno la Mungu.
Na mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu tupu... Ayubu 14:1.
Mil 10 zangu, sikuzaliwa nazo, nilizaliwa nikali uchi na pia nitaondoka duniani nikali uchi.
Walionidhulumu pesa zangu laana i juu yao na kamwe hawataweza kujenga kiwanda hata kimoja Kwa ufanisi na kikadumu, kila kiwanda kitakachojengwa Kwa kutumia pesa ya dhuluma ya jasho la wanyonge lazima kitakufa.
Dhuluma ni laana, nao walionidhulumu pia wataondoka Duniani wakali uchi, hayo mabilioni yetu waliyotudhulumu hawataondoka nayo.
Mungu ni mwema na jina lake lihimidiwe.
Mkuu,,mbona mali walizotudhulumu wazungu zilizidi kuwapaisha?...
We samehe tu...Mola hupenda waja wanaosamehe
 
Kila ulicho sema kitakurudia wewe. ..maana neno linasema mtu anayelaani mabaya hayatamtoka. ..mkumbuke yule mama mjane na yule kadhi. .alikwenda kumdai na hakuchoka wala hakulani. ..mpaka akapewa haki yake! Tubu kwa MAULANA MOLA wetu atakusamehe na uanze tena....nakutakia heri ndugu yangu. ..
 
Back
Top Bottom