Mikutano yote ya hadhara imepigwa marufuku Tanzania, hata diwani haruhusiwi kuongea na wananchi wake

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
13450036_950586908373282_8061591640874954582_n.jpg


Diwani wa kata ya Nyamisangura wilaya ya Tarime amezuiliwa kufanya mkutano wake kwa kuwa mikutano yote ya hadhara imepigwa marufuku Tanzania
 
Utii wa sheria bila shuruti utaleta maendeleo....!
 
tehe tehe tehe wapige marufuku na ya mwenyekiti wa mtaa maana sheria ndogo za mtaa ninaoishi ni balaa, yaani Mwenyekiti wa mtaa akiitisha mkutano wa hadhara mwananchi ambaye hatahudhuria analipa faini ya Tshs.5,000/= halafu mbaya zaidi mikutano hiyo inakuwa siku za Jumapili kuanzia saa kumi jioni muda ambao na mie ndio nataka nikasafishe jina baa.
 
Basi tu-centralize maagizo na mipango ya maendeleo yote ya kila kijiji na kata ifanywe na serikali kuu
 
Kwenye gazeti la Jamboleo la leo tarehe 16 June 2016, limemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba akisema kwamba mikutano iliyopigwa marufuku ni ile ya kitaifa lakini kwa ngazi ya jimbo inaruhusiwa. Sasa hao Polisi waliozuia mkutano wa Diwani wanatokea nchi gani?
 
HII IMEKAA POA, nime print hii, ikifika jumamosi ya mwisho wa mwezi mwenyekiti wa kijiji akituita kwaajili ya usafi. Nampa hii, Najua mtasema kuwa usafi hauusiki kwenye hii, LAKINI pia usafi si mnakutana hadharani pamoja? basi huu nao ni mkuataniko wa hadhara nao pia ni batili. Jumamosi ya mwisho wa mwezi nitakaa kwangu nitafanya usafi wa viatu vyangu basi.
 
Hii si kurudi miaka 50 nyuma, hapa ni sawa tupo kwenye ardhi isiyo na utaifa, hatujui hata misingi yetu tupo zaidi ya wanyama wa porini.
 
Ni kutojiamini ndo kunawafanya kutenda ovyo! Hivi kama kuna jambo la muhimu kuongea liongelewe wapi? Au tuviziane kwenye misiba ndo tuongee mambo ya maendeleo! Naiona Tanzania yangu mfukoni mwa wasiotaka uhuru halisi.
 
Back
Top Bottom