Mikutano ya kisiasa iruhusiwe ukimya uliopo ni mbaya sana

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,759
Labda ni mawazo yangu kulingana na mambo ya hapa na pale yanayotokea kwenye nchi yetu.

Wakati sijaanza kukusimulia ndoto yangu. Nikuchekeshe kidogo, utajisikiaje kama utapewa adhabu ya kuto kuongea Kwa angalau siku 7?

Ni bora unyimwe chakula au unyimwe zawadi yoyote. Bila shaka kuongea ndio maisha yenyewe.

Watu huoana kwa mazungumzo lakini pia hutengana Kwa mazungumzo. Njia mojawapo ya kujua familia Yako ikoje ni kusikiliza mazungumzo yao.

Hapo utayajua yale wanayopenda na wasiyoyataka na wakizungumza usione kama wanapiga kelele maana hata Msitu unaotisha hutawaliwa na kelele za ndege na viumbe vya aina mbalimbali, hivyo bila kelele za viumbe na mimea Dunia haiwezi kunoga.

Mama nchi yetu IPO kimya sana Watu bado wanaogopa kuongea!

Mikutano ya siasa ilichangamsha sana nchi yetu wakati wa jk! Hata vyombo vya habari vilinoga sana!

Watu walikuwa wanawahi nyumbani kusikiliza taarifa ya habari Kwa kuwa ilikuwa na mvuto wa aina yake.

Huku utamsikia Lissu, kule utamsikia heche, mara kinana ukibadili chanel nyingine unakutana na peter msigwa baadae majibu ya serikali kukosoana na kuambiana ukweli huleta maendeleo chanya hata wizi wa Mali za imma ulipungua sana!

Sasa hii silence uliyoiacha iendelee ni mbaya sana! Kwa sasa unapongezwa Kila siku na watu wale wale waliopo kwenye systeam ,lakini hamjawapa nafasi ndege wapige kelele Ili tuisikie milio yao mmewazuia kwamba wanaleta fujo.

Wakati wa kampeni utastahimili kelele zao? 2025 sio mbali 'watu wanapofanya mikutano wanatuonesha ni wapi Panavuja! Ukiwauzuia hawatasema ila mioyoni wameyajaza! 2025 utayastahimili?

Sawa kazi iendelee lakini bila wakosoaji? Ok nikusimulie ndoto yangu !! Nimeota mbolea haipelekwi vijijini inaishia wilayani wale waliojiandikisha wanatumiwa msg wazifuate je wataweza? Asante mama!!
 
Back
Top Bottom