Mikutano ya JK, Wananchi wanafuata mkutano au kuangalia wasanii?

Dullo

JF-Expert Member
Oct 24, 2009
251
64
Hivi ni kweli watu wote wanaokwenda katika mikutano ya JK wanakwenda kwa ajili ya kumsikiliza mgombea wao au wanakwenda kuwaona wasanii wanaoambatana na mgombea huyo, Jamani mnaokuwa maeneo hayo hebu tusaidieni!!
 
Subiri jibu 31 Octoba.
 
Kinachowavuta kwenye mikutano ya JK ni burudani tu kwani JK hana jipya la kuwaelezea watanzania
 
and the funny thing JK anahutubia for only less than 10 minutes siku hizi. Hana kitu cha kuwaambia wananchi.
 
Subiri jibu 31 Octoba.

Jibu hili hapa.

1. Wengi ni watoto waliotoroka majumbani mwao kumwona raisi, ama wamelazimishwa ili kujaza mkutano kama tulivyosikia kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi

2. Kuna ambao wanapewa posho kwa ajili ya kwenda kwenye hiyo mikutano (posho haizidi 5,000/=)

3. Kama tunavyojua watz wengi maisha ya umaskini wa kutisha so wanakuwa wanaona kama starehe kuparamia hayo malori yanayotolewa ili kuwahamasisha kwenda kwenye hiyo mikutano.

4. Halafu kundi kubwa zaidi ni linalofuata wasanii.. Na ndio maana CCM kwa kujijua wazi wamechokwa wakaona watumie wasanii ili wavutie watu..
 
Back
Top Bottom