Mikutano mikubwa ya kisiasa inaendelea kwenye daladala, mabasi, masokoni, vituo vya bodaboda

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
sijui kama mtukufu anajua kwamba ile mikutano ya kisiasa sasa inaendelea katika maeneo yasiyo rasmi.

Ni mikutano mikubwa na wahudhuriaji wanapokezana kuhutubia huku wakishutumu vikali hali ya kiuchumi.

Wanaopanda madaladala wanajua hili,kuna mapambano makubwa ya kisiasa yanaendelea ndani ya vyombo hivyo vya usafiri ambapo abiria huhubiriana mambo mbali mbali kuhusu nchi yao,haswa masuala ya kiuchumi,na wengi huongea kwa hisia kali.

hali hii inaendelea katika mabasi,vituo vya daladala,sokoni na sijui kama kuna wa kuizuia.wote.wanajadili hali ngumu ya kiuchumi na hali mbaya kisiasa.

Hakika wananchi wana bunge lao na mikutano yao inaendelea,japo serikali inajifariji kwamba imeipiga marufuku
 
Yes, ila kwa wapinzani. Ila hii ya kwenye mabasi haizuiliki, kwa sababu mwitishaji hajulikani na wahudhuriaji hawajulikani, ni juu kwa juu.
na wanausalama wanakuwemo wamejikalia kimya
 
Wakuu hata wanausalama nao huwa wanachangia

Hakuna tena oooh sisi sijui ni nani, wengine wanajitambua sana
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom