MIKUMI: Mkulima aliyechomwa mkuki na Wafugaji apata nafuu baada ya matibabu

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,761
OFISI YA MBUNGE Jimbo La Mikumi inalaani sana kitendo cha kinyama kilichofanywa na Ndugu zetu wa jamii ya wafugaji kwa kujichukulia sheria mkononi na kumjeruhi vibaya Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi ambapo leo tarehe 25 desemba majira ya Mchana amechomwa mkuki mdomoni na kutokezea nyuma ya shingo yake, ambapo alipelekwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadae amekimbizwa hospitali ya mkoa MOROGORO ili kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na kwa matibabu zaidi.
AUGUSTINO MTITU alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani yake kufukuza Ng'ombe wasiharibu mazao shambani kwake,

Kipande cha mti kinachoonekana hapo mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali, Inasemekana MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa.

WITO KWA SERIKALI.
Ofisi Ya Mbunge Mikumi inatoa wito kwa Serikali kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.

Imetolewa na:-
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Mikumi.

kilosa-1.jpg

kilosa-2.jpg

kilosa-3.jpg


========

UPDATES

img_20161226_203021-png.450664


Maendeleo Ya Ndugu AUGUSTINO MTITU aliyejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki jana tarehe 25/12/2016 Kijiji cha Dodoma Isanga Kata Ya Masanze Jimbo La Mikumi na jamii ya wafugaji, hivi sasa anaendelea vizuri na matibabu baada ya kutolewa mkuki mdomoni salama salimini kwenye HOSPITALI YA MKOA MOROGORO na amelazwa wodi namba moja hospitalini hapo.

Ofisi Ya Mbunge Jimbo La Mikumi inatoa shukrani zake za dhati kwa Madaktari na wauguzi waliofanikisha zoezi hilo, Lakini pia Ofisi Ya Mbunge Mikumi itakuwa ikiwapa maendeleo ya Bwana AUGUSTINO MTITU mpaka hapo hali yake itakapokua imetengemaa.

Lakini la muhimu zaidi Mh. Mbunge amefanya mawasiliano na ngazi mbalimbali zinazohusika akiwemo Waziri wa Mambo Ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba juu ya kile kilichotokea na waziri amesikitika sana na ameahidi kulifuatilia suala hili kwa kina na kulitolea maamuzi magumu.

Imetolewa na :- Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Jimbo La Mikumi

 
Pole sana Majeruhi!
Halafu mbona kama hii trend inazidi kushika kasi?haiwezi pita siku bila kusikia au kuona habari yenye tukio la purukushani kati ya wakulima na wafugaji?
Na ukafuatilia cases nyingi 4 kati kumi,unakuta ni mikoa ya pwani na morogoro?
Kwanini iwe mikoa hii zaidi?
Serikali ifanye kazi yake kuhakikisha watuhumiwa wanafikishwa kwenye sheria ili haki itendeke!
Na nampa hongera huyu mkulima,huyo mkuki,ingekuwa ni wengine wangeshakufa!Huu ujasiri aliyonao wapaswa kupongezwa!
Pole pia Prof J,na hongera kwa kutetea masilahi ya mpiga kura wako!
 
Pole sana Majeruhi!
Halafu mbona kama hii trend inazidi kushika kasi?haiwezi pita siku bila kusikia au kuona habari yenye tukio la purukushani kati ya wakulima na wafugaji?
Na ukafuatilia cases nyingi 4 kati kumi,unakuta ni mikoa ya pwani na morogoro?
Kwanini iwe mikoa hii zaidi?
Serikali ifanye kazi yake kuhakikisha watuhumiwa wanafikishwa kwenye sheria ili haki itendeke!
Na nampa hongera huyu mkulima,huyo mkuki,ingekuwa ni wengine wangeshakufa!Huu ujasiri aliyonao wapaswa kupongezwa!
Pole pia Prof J,na hongera kwa kutetea masilahi ya mpiga kura wako!
... Umeuliza why mikoa ya Morogoro na Pwani, jibu ni kwamba mikoa hii kwa uzoefu wangu hawana uthubutu wa kukabiliana na wafugaji, na pia wako divided - viongozi wa kijiji na vitongoji wabashirikiana na wafugaji kuwahujumu wananchi wao. Wafugaji kwa hakika maeneo haya huwa wanatamba wapendavyo...
 
Hawa wafugaji hawajali mazao ya wakulima as long as mifugo yao ishibe.Mara nyingi utakuta wanaachia vitoto vidogo visivyo na akili vinavyoingiza mifugo shambani.Ukitaka kukamata mifugo ufidie ndio hayo matokeo
 
Pole sana aiseee na hapo Morogoro hospital kama ngoma ni nzito hiyo plse kimbiza haraka sana Muhimbili Hospital ili kuminimize complication.

Hatari sana ugomvi kati ya haya makundi mwili Mfugaji vs Mkulima.

Kuna haja ya kuwa na utatuzi wa kudumu ktk matumizi ya ardhi otherwise matukio kama hayo ktk picha itafika mahali yatakuwa common tu.
 
Wamasai hawana tofauti kama ilivyo polisiccm dhidi ya wapinzani wa cicim
Kweli unaichukia CCM na serikali yake mpaka kuifananisha na tukio.

Hapana Siasa isikuharibu kiasi hicho Serikali iko makini na majukumu yake kwa wanainchi hata kama ni ngumu kumeza ndiyo hivyo hakuna namna ndo msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano,kila MTU afanye kazi kwa nguvu zote vya bure muda wake umekwisha.

Kama Mungu alivyosema Mwanaume kwa jasho lako utakula ndiyo sasa na Rais hatanii ktk hili.
 
Jamani hawa Wamaasai Tuwafanye nini? mbona ni makatili sana. Nafikiri Serikali itachukua Adhabu kali kwa jamii hii ya kimasai (Wafugaji)
Pole sana Ndg yetu, Mtanzania mwenzangu.
Dawa ni kuua mifugo yao kwa njia zozote maana wao wamekuwa wakihama toka mikoani kwao kuja mikoa mingine kuwasumbua wenyeji.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom