Mikumi: Hakuna taabu, ngono chini ya uvungu wa magari

Giro

JF-Expert Member
Feb 9, 2009
359
22
BEDA MSIMBE,
Daily News; Sunday,March 01, 2009 @19:00

Moja ya miji ya zamani kabisa katika barabara ya kwenda Zambia, Tanzania, ni Mikumi. Mji huu ambao upo mwendo wa saa takribani nne na nusu kutoka Dar es Salaam, ni mji ambao umebanwa kila mahali. Pamoja na uzuri wake ni mji unaoweza kuwa yatima baadaye.

BEDA MSIMBE anaandika alichokiona na mahojiano na watu.
MAJIRA ya kuanzia saa moja jioni mji wa Mikumi hubadilika sana. Kutoka mji uliokuwa kimya wakati ukiingiza gari lako majira ya saa sita mchana, mji huu unalipuka kwa wingi wa watu majira hayo ya jioni.
Watumiaji wakubwa wa njia hiyo ndio wanaofanya kuwapo na haja ya kuwa na mama lishe kwa muda mwingi na baa chache kuendelea kuhudumia wateja. Ni mji mdogo kimazingira, lakini ni mkubwa mno kwa pilikapilika zake ambazo nyingi zinaashiria maisha ya hatari.

“Hapa Mikumi kuna matatizo mengi yanayochangia mji kuwa nyuma kimaendeleo, uchafu kama uchafu unafukuza wateja wanaohitaji kupumzika maeneo haya,” anasema mkazi wa Mikumi aliyejitambulisha kwa jina moja Daudi. Hata hivyo, anasema licha ya uchafu huo wa mikojo, uchafu mwingine unaodaiwa na wakazi wenzake wa mji huo ni kwa eneo hilo kutumika kwa ngono hasa nyakati za usiku.

“Mikumi sasa imegeuka kuwa eneo la kufanyika uchafu wa kila aina …tukiacha huu wa mikojo na takataka nyingine, sasa umezuka uchafu mwingine wa vitendo vya ngono ambazo hufanywa na madereva wa malori makubwa tena chini ya uvungu wa magari yao,” anasema Daudi.

Mmoja wa walinzi wa Saccos moja ya Mikumi, Yuda Lushinge, anasema pamoja na kufanyika kwa ngono hizo chini ya uvungu wa magari hayo pia nyakati nyingine zinafanyika kando kando ya barabara kuu bila ya aibu wala woga. Ni lakshari na suna kwa maneno yao, wanajivinjari nyakati za usiku katika barabara za Mikumi.

Wakati fulani unajiuliza swali ni ukahaba au umalaya au umasikini? Binti mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kwamba ni umasikini hakuna cha kufanya, na mji ni mdogo. Ukiangalia kwa makini kweli mji ni mdogo kwa kuwa umebanwa kila mahali na mambo yanayohusu hifadhi na pia mashamba makubwa ya watu.
Upande mmoja kuna milima ya Udzungwa ambayo ni hifadhi, kuna hifadhi ya Mikumi na pia kuna mashamba makubwa ya miwa na sukari. Mashamba ambayo yamepakana na mji. Kibiashara, unaweza kufikiria kabisa kwamba ni mji ingawa mdogo basi uwe na maendeleo ya kutosha kutokana na kuwa jirani au kupakana kabisa na hifadhi ya Mikumi ambayo ni sehemu ya hifadhi ya Selou.

Ikiwa ni mbuga yenye kilomita za mraba 1,165 na wanyama wa aina mbalimbali ni dhahiri kuwa mji wa Mikumi ungelisheheni hoteli na loji ambazo zinaweza kusaidia wanaokuja kutalii majira ya Juni hadi Oktoba ambapo barabara zinaweza kupitika na watalii kuweza kuona wanyama.

Shughuli mbalimbali zinaweza kufanyika ambazo zinaambatana na biashara ya utalii lakini vijana wengi hapa pamoja na mji wao kuwa mgumu, mabinti jioni wanazagaa na kutumia urithi wa asili yao kuweza kuishi.

Huwezi kusema huu ni ukahaba au umalaya na huwezi kusema huu ni umasikini lakini unaweza kusema kwamba mji huu unahitaji kwelikweli 'michoro' thabiti ya kuwanasua vijana hasa wa kike kutegemea miili yao kufanya maisha yawezekane. Kama miradi inaweza kuibuliwa kwa kuambatana na mazingira ya mji wenyewe hii kasi ya mabinti wengi kujimwaga mtaani jioni inaweza kupungua na jioni ikawa ya kawaida.

Mwenyeji wangu ambaye alisema wasichana wengi wamekuwa wakiongezeka nyakati za jioni kutoka katika maeneo mbalimbali ya mji na viunga vyake huwa na kazi moja muhimu, kukutana na madereva wa magari makubwa ambayo kwa sasa yamekuwa mengi nyakati za jioni katika mji wa Mikumi.

Wapo pia wanaoambatana na madereva hao wa malori ambayo hutumia eneo hilo kama sehemu ya kupumzika.Huwezi kujua mara moja kwamba kuna ngono hatari eneo hili mpaka pale unapotembezwa na mwenyeji wako nyakati za majira ya saa tano usiku na ukakuta watu wameegesha miili yao chini ya malori wakiwa wameegemea magari yao.

Wasichana wengine ambao walikuwapo katika baa moja tuliyopumzika na kupata supu nyakati za jioni, walisema kuwa wanaofanya biashara hiyo wanaifanya kwa uamuzi kwani mji huo una nafasi nyingi za kufanya vitu mbalimbali, hasa mama lishe kutokana na ongezeko la magari na watu nyakati za usiku.

Takwimu za hivi karibuni kutoka Hospitali ya Mtakatifu Kizito ya Mikumi zinaonyesha kuwa kati ya watu 1,533 waliopimwa, watu 314 wamebainika kuwa na VVU kati ya hao, wanawake ni 180. Hizi ni takwimu za karibuni sana.
 
Inasikitisha sana. kabla sijachangia zaidi labda niulize hali ikoje kwa vijana wa kiume wa mji huo?. je kuna wizi wakupindukia?, au wamekimbilia mijini kutafuta riziki?. Kama wapo hopo wanajishughurisha na shughuli gani?. Nauliza hivi kwasababu imekuwa ni kawaida kuona fulsa zipo lakini mabinti huona miili yao ni fulsa mbadala. Ni vema kutafakari kama ni tatizo la jamii nzima au jamii ya kike tu.
 
yes pale ni hatari sana. wiki mbili zilizopita, tulipita pale mida ya saa tano usiku palikuwa pamechangamka kama mchana mpaka tukaogopa hata kusimama/kupumzika. watu walikuwa wengi sana wake kwa waume, tena vingi ni visichana vidogo umri wa shule za msingi. na malori yalikuwa mengi mno barabarani yakiwa yamepaki.
MUNGU atuokoe na hii biashara ya UZINZI. kutokana na hali ngumu ya maisha watu wanaona kuwa uzinzi ndiyo njia pekee rahisi ya kujipatia kipato. na hapa si mikumi tu. hapa dar je? balaa tupu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom