Miktano ya CHADEMA kusini watu wachache kuliko kawaida | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miktano ya CHADEMA kusini watu wachache kuliko kawaida

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BigMan, Jun 8, 2012.

 1. B

  BigMan JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  NIMEFUATILIA BAADHI YA PICHA NIKABAINI KWAMBA SIYO KWELI MIKUTANO YA CDM KANDA YA KUSINI INAJAZA KAMA INAVYODAIWA NA CHAMA HICHO, SITAKI KUSEMA CHADEMA KASKAZINI OK LAKINI BADO SAFARIO NI NDEFU KATIKA KUJIHAKIKISHI INATWAA NCHI UCHAGUZI UJAO. ANGALIA HII PICHA


  Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika Akihutubia na akisikiliza maswali na kutoa somo la kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi, elimu ya katiba mpya na M4C, kwa wanakijiji katika maeneo ya wilaya tofauti za Newala na Nanyumbu
  [​IMG]
  Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika Akimsikilzia Katibu wa Tawi wa CUF, Bi. Zaituni baada ya kutoa somo la kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi, elimu ya katiba mpya na M4C, kwa wanakijiji katika maeneo ya wilaya tofauti za Newala na Nanyumbu.
  Picha na Habari na Kurugenzi Ya Habari-CHADEMA
  MICHUZI: Operesheni Okoa Kusini
   
 2. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  MKUCHIKA, GHASIA, CHIKAWE NA MEMBE WAENDA KUUZIMA, CCM KUJIPIMA NGUVU JANGWANI KESHO
  VUGUVUGU la Mabadiliko (M4C) linaloendeshwa na Chadema katika mikoa ya Lindi na Mtwara, limewatisha mawaziri wanne wanaotoka katika mikoa hiyo, ambao wamelazimika kurejea majimboni mwao kusafisha hali ya hewa.

  Mawaziri waliorejea majimboni kufanya kilichoelezwa ni shughuli za kiserikali ni pamoja Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

  Kwa wiki takribani ya pili sasa, Chadema kimekuwa kikiendesha operesheni hiyo ya vuguvugu la mabadiliko katika mikoa hiyo ya kusini mwa nchi.

  Jana, taarifa zilizopatikana mkoani Lindi zilisema Ghasia alifanya mkutano katika jimbo lake la Mtwara Vijijini akiwa katika harakati za kufuta nyayo za Chadema.
  Oparesheni hiyo ya Chadema jana na leo ilitarajiwa kuingia jimbo la Mtama ambalo linaongozwa na Membe.

  Vuguvugu hilo linaongozwa na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, ambao ni Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambao wanatarajia kuhutubia mikutano yao katika kata aliyozaliwa Membe.

  Mkuchika alithibitisha jana kuwa yuko jimboni kwake Newala, na alipoulizwa kama lengo lake ni kufuta nyayo za Chadema, aling'aka, "Kwani kila siku nikija nyumbani kwangu huwa mnaniuliza, mimi nimekuja nyumbani kwangu bwana. Niacheni nipumzike nyumbani kwangu."

  Membe alipotafutwa kuzungumzia taarifa hiyo simu yake haikuwa hewani, lakini Msemaji wa wizara hiyo, Assah Mwambene alipoulizwa alipo bosi wake alithibitisha kwamba yuko jimboni kwake.

  Jana, vuguvugu hilo lilikuwa katika Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, lakini lilikumbana na upepo mzito wa kisiasa baada ya bendera mpya za CCM kuonekana kupamba kona mbalimbali za jimbo hilo.
  Waziri Ghasia na Chikawe pia hawakupatikana kupitia kwa simu zao kuzungumzia taarifa hizo.

  Msigwa ashambulia mawaziri
  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliwashambulia mawaziri hao wanaotoka majimbo ya mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, akihoji ni kwanini wanaikumbatia CCM.
  Msigwa alisema CCM imeshindwa kuwasaidia kuleta maendeleo katika mikoa hiyo ya kusini mwa Tanzania, ndiyo sababu, watu wanaishi katika hali ya umasikini wa kutisha.

  "Mimi ninawashangaa wabunge wa majimbo ya Lindi na Mtwara wakiwamo mawaziri Hawa Ghasia, Mkuchika na Bernard Membe ni kwa nini wanakiunga mkono CCM wakati majimbo yao yamekithiri kwa umaskini," alisema Msigwa na kuongeza;

  "Nashangaa Membe, Hawa Ghasia na Mkuchika sijui kiburi wanakipata wapi. Ndiyo sababu wamehama majimbo yao na kuishi Dar es Slaam, haiwezekani leo mikoa wanayotoka, wilaya na hata majimbo yakawa na sura kama ilivyo sasa. Nitakwenda kuwabana bungeni,'' alisema Msigwa.

  Msigwa alitamba kuwa yeye na wabunge wote wa Chadema wanaishi kwenye majimbo yao, ndiyo sababu wamekuwa wakifanikiwa katika mikakati yao ya kutetea na kuwaletea maendeleo wananchi wao.

  Sugu alia umaskini
  Katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) alisema ukarimu wa wakazi wa Lindi na Mtwara kwa CCM ndio uliosababisha mikoa hiyo kuwa katika lindi la umaskini.
  Mbilinyi alisema wabunge kupitia chama hicho hawana uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na mfumo wa chama hicho kukumbatia matajiri na kuachana na maskini.

  Alisema ndani ya CCM, watu wa kipato cha chini hawawezi kupata ubunge, akitoa mfano kwamba fomu ya ubunge ya CCM inachukuliwa kwa Sh100, 000 ilihali ya Chadema ni Sh50,000.

  "Nawasihi vijana wenzagu kuungana na kuwa na ujasiri wa kuamua katika masuala ya kimaendeleo. Mimi nilikuwa mitaani na muziki wangu, lakini nikatokea Chadema na kunipa nafasi ya kugombea ubunge ,lakini ningekwenda CCM wasingenipa nafasi ya kugombea kwa sababu ya umaskini wangu," alisema Mbilinyi na kuongeza:

  "Hivyo, basi wazee na vijana nawasii kuachana na CCM kwa sababu chama hicho kimekosa mwelekeo tangu alipofariki Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, CCM iliyobaki ni ya wanjanja sio wewe ulioko kijijini."

  CCM kujipima nguvu Jangwani
  Wakati Chadema ikizidi kuwasha moto wa vuguvugu la mabadiliko, Chama tawala CCM kesho kitafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, kutoa msimamo wake kuhusu mambo muhimu yanayogusa taifa.

  Mkutano huo unafanyika ikiwa zimepita takribani wiki mbili tangu Chadema wafanye mkutano mkubwa katika viwanja hivyo uliohudhuriwa na mamia ya watu, na kuzindua kampeni yake ya M4C', yenye lengo la kushika dola mwaka 2015.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana katika mtandao wa chama hicho tawala jana, iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa mkoa huo, Juma Simba ilieleza kwamba mkutano huo utaanza saa 8 mchana.

  Simba alisema katika taarifa hiyo kwamba, chama hicho kitatumia mkutano huo kuwaeleza Watanzania msimamo wake kuhusu hatma ya maisha yao.

  "Utaeleza hatma ya maisha ya Watanzania katika suala la ajira, miundombinu ya barabara, reli, bandari na anga, bei za bidhaa mbalimbali, umeme na rasilimali za taifa," alisema Simba.

  Alifafanua kwamba jambo jingine litakaloelezwa katika mkutano huo, ni msimamo wa chama hicho kuhusu mchakato wa Katiba Mpya pamoja na vurugu za Zanzibar.

  Katika mkutano huo watakuwapo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali na kutoa ufafanuzi juu ya masuala hayo, yaliyoainishwa kama msimamo wa chama hicho.  Mwananchi
   
 3. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akihutubia wakazi wa Lindi.

  [​IMG]

  [​IMG]
  Mwenyekit wa CHADEMA Freeman Mbowe akifungua moja ya matawi ya CHADEMA Mkoani Lindi.

  [​IMG]
  Kina mama Wa Lindi wakiwa na Furaha kwa kupata mkombozi walisikika wakisema Peeeeplesssss Powerrrr.

  [​IMG]
  Foleni kubwa ya kuchangamkia kadi za Uanachama za CHADEMA.​
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Usijaribu kupika habari. Baada na kabla ya mkutano wa hadhara viongozi wote wa CDM hugawanyika katika meza mbaimbali kuongea na wananchi na kupata wanachama wapya.
   
 5. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  [​IMG]
   
 6. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  mbona mnahangaika saaana?
   
 7. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  So what? Chadema haina tamaduni ya kununulia watu ubwabwa na kuwapakia kwenye mafuso
   
 9. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,026
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  peoples poweeeeerrrr ni kama jua bana..lazima liwake tu..
   
 10. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenye macho haambiwi tazama,binafis nilishuhudia mkutano wa Lindi,wenyewe wanasema haijawahi kutokea chama cha upinzani kukusanya watu wengi vile!
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ukisikia kuweweseka ndiyo huku!! Na bado watani zetu, nyinyi badala ya kuhangaika na kiutimiza ahadi zenu, nimefarijika kwamba sasa mnacheza tune za dance la M4C!!
   
 12. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,230
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Mkuu kiganyi kwa Picha hapo juu umemaliza ubishi wote maana mtoa mada ameshidwa kuweka ushahidi wa mkutano wenye watu kiduchu. Naona watu wanakula CHATA za Lema, kama ulaya vile kabla na baada ya mechi watu wanavyopigiwa ma siginecha. CDM uko juu. Nyota yenu unang'ara kwa sasa.
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,942
  Trophy Points: 280
  Propaganda dhaifu. Jipange na uje tena, hoja dhaifu kama hizi utanyimwa posho yako bure.
   
 14. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ezekia Wenje

  right now niko jimbo la mtama kwa mh membe,niko kwenye kijiji cha nyangamala hakuna maji,dispensary,wala barara alafu ndo makao makuu ya tarafa and mh membe hajawahi onekana hapa toka achaguliwa huku anajiita jogooo,nimedhamiria kuvua gamba kata nzima leo.
   
 15. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hivi huyu michuzi si yule aliyekwenda Brazil pamoja na baba Rizone? Kwa nini magamba mnahangaika namna hii? Kwa msitu jifunzeni. Mnapoona miti imeanza kupukutisha majani mjue kiangazi kinakuja! Na kwenu si kiangazi tu, ni jangwa!
   
 16. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  May God be with you dear!
   
 17. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 18. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  [​IMG]
   
 19. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Njia ya Mwongo(CCm) ni fupi sana!
   
 20. B

  BigMan JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  fungua link baaada ya mada hapo chini uone mkutano wa mnyika ulivyokuwa na watu kiduchu kinachotumuka hapo ni kutumika kwa picha za maeneo machache ya mjini yenye watu wengi kwa waandishi wenu wa habari mnaowanunua kwani nani hajuhi hilo ?
   
Loading...