Raphael phockus
JF-Expert Member
- Nov 4, 2018
- 778
- 4,518
Habari ya muda huu wanajanvi.
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu, ungana nami katika habari hii inayo husu uwezo wa ndege vita aina ya MiG 25 ya muungano wa Usoviet miaka ya 1970's
Mikoyan-Gurevich, MiG 25 ni ndege ya mwisho iliyoundwa na MIKHAIL GUREVICH kabla ya kusitaafu shuguri za uundaji wa ndege.
MiG 25 ni ndege iliyo undwa na muunganiko wa vyuma viwili ,ndege hiyo ilikuwa na uwezo wa kukwepa makombora huku ikiwa na sifa ya kukimbia mara tatu(×3)
zaidi ya mwendokasi wa sauti.
Ndege hii ilizalishwa kati ya miaka ya 1964 na 1984 .Terehe 6 mwezi march 1964 kwa mara ya kwanza ilianza kufanyiwa mazoezi.
Ilipofika mwaka 1970 ilianza rasimi kutumika kama ndege ya mashambulizi ya kivita.
Mwezi Novemba 1971 Israeli ilikumbana na moja ya ndege hizo ikirusha makombora kutoka
umbali wa futi 30,000 angani. Ilikuwa ndege yenye kasi kubwa na tayari ilikuwa imeondoka eneo
hatari kabla ya makombora ya Israeli kupaa.
Jeshi la Marekani lilibaini kuwa ndege hiyo ilikuwa ni ile iliyoonekana kupitia picha za satelaiti zake za kijasusi. Ghafla waliamini kuwepo ndege ambayo ina uwezo kushinda ndege yoyote
katika jeshi la Marekani.
Hitimisho.
Uzalishaji na muendelezo wa MiG 25 ulikamilika mwaka 1984 baada ya muungano wa Usoviet kutimiza idadi ya ndege vita 1184.