Mikopo

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
6,824
14,175
naombeni more info,nataka kujenga nyumba,ni benki gani na kwa utaratibu upi inatoa mikopo,kwa kutumia hati ya kiwanja au nyumba,nifahamisheni wakuu
 
Nenda kajaribu Twiga Bancorp kama una sifa, hasa dhamana ya mkopo kama ipo.
 
Nenda kajaribu Twiga Bancorp kama una sifa, hasa dhamana ya mkopo kama ipo.

sina hakika asilimia mia ila Azania wanatoa mkopo kwa ajili ya nyumba ila mkopaji lazima awe amekamilisha kwa asilimia fulani na atatakiwa kuwasilisha salary slip zake kama ni mfanyakazi na kama ni mfanyabiashara atawasilisha bank statement yake
 
Hapa kwetu bado utaratibu wa kupokea hati za nyumba au kiwanja haiwezekani. Nimeenda benki zote tajwa nikiwa na hati nikashindwa. Tena nikiwa nataka milion tano wakati kiwanja changu kikiwa na thamani ya milion kumi. Nikajaribu kuwaomba wanunue mkopa nilionao kwa kuwa mimi ni mwajiriwa na nimekopa lakini ikashindikana. Benki zetu hazitusaidii kabisa
 
Have you tried CBA and Akiba Commercial Bank?
 
Kote huko nieenda mpaka Stabic wanao tangaza kwa sana. Mabadiliko yanahitajika ktk sector ya bank.
 
Kuna wakati huwa najiuliza hao wanaokopa wana sifa gani za ziada?. Mimi nimekuwa na akaunti Barcklays kwa taribani miaka 3 na nimekuwa nikitumia hiyo tu, lakini ninapouliza suala la mkopo huwa naelezwa kwamba bado utaratibu haujaruhusu. Kwa kweli inakatisha tamaa sana kwa benki zetu.
 
pole mkuuu nchi yetu hii hamna mazingira mazuri ya kutoa mikopo na ukibahatisha unaumia sana ila ndo hivyo hatuna ujanja maana hata serikali haina mpango wa kuongea na mabenki ili kuweka mazingira vizuri. umaskini hautaisha sana sana kupata madeal ya ofisini mambo yaende kama uko kwenye nafasi ya kuruhusu kupata deals nzuri kama commission ambazo hazitakuletea matatizo baadae
 
bank tz hazipo kumsaidia mtanzania mikopo wanapewa wahindi na waarabu tuu bila hata hati maana wengi wao wanaishi nyumba za nhc.wanadai watz hatulipi mikopo.sioni hata faida ya kutumia bank kwani unapotaka hata vijisenti vyako usumbufu mtupu mara system down mara manager hayupo mara foleni kubwa etc
 
Back
Top Bottom