Mikopo ya watumishi CRDB

Watumishi wote wa Serikali na Umma au wao wenyewe CRDB kujikopesha?
fafanua
 
Walisimamisha utoaji wa mikopo, vipi!! Wameanza upya kutoa mikopo kwa watumishi!!?
Juzi nilienda Crdb Singida kuulizia. Nikajibiwa kuwa, wao bado hawajaanza kutoa mikopo ila baadhi ya matawi mikopo imeanza upya.

Nilipoomba wanitajie hayo matawi, jamaa akanijibu kuwa hata yeye amesikia kuwa baadhi ya matawi wameanza ila hajui ni matawi yepi!!
 
Bado Hawajaanza Hofu Yao Ni Watumishi Hewa
Pia Form Za Mkopo Utatakiwa Kuambatanisha Barua Ya Mwajiri Wao Akiihakikishia Crdb Kuwa Muombaji Siyo Mtumishi Hewa.

Mambo Bado Magumu Sana Ndg
 
  • Thanks
Reactions: ffq
watakua hawajaanza kutoaa....mambo ni magum kupita maelezo wao wenyewe wamekula hasara...walikopesha watu kibao kumbe ni watumishi hewa....hatar
 
Watoe mikopo pesa wazitoe wapi? Ndio wanapita mitaani na gari la matangazo wakihimiza watu wakafungue account kwa elfu kumikumi.

Tayari benki za kigeni wameshaanza kuwachangamkia wateja wao, ukienda stanbic nbc standered chartered ukasema unamkopo crdb wanaununua fasta, juzi nilienda crdb kuomba statement nikaambulia matusi.
 
Kennedy, crdb hawatoi hata kwa watumishi wa secta binafsi wakati watumishi hewa wako serikalini, haya tuliyasema wakati wa JK wakasema ooh kimei yuko vizuri sana haya yakowapi sasa? Bora huyu mzee astaafu asijetimuliwa na Beno Ndullu.
 
Mkuu Eddy Nchi Hii Imeoza Hata Haya Majipu Utamkamua Mgonjwa Wapi ? Yaani Mwili Wote Majibu Mwisho Mgonjwa Atakakufa.

Kama Unakumbuka Uzinduzi Wa Call Centre Za Police Alisema Kimei Kuwa Naogopa Kukutana Na Rais Atanitumbua Jamani. Huyu Dr Kimei Anajua Kuwa Mirija Imekatwa Hakuna Tena Ujanja Ujanja Kamwe
 
Tulisema hii bank imekuwa kubwa sana kimei haiwezi tena atafutwe mtu mwenye weledi wa juu zaidi watu wakawa wabishi.

Inabidi Danida walete mtu wao asaidie kuinusuru kufilisika kabisa.
 
Back
Top Bottom