Kessy Wa Kilimanjaro
JF-Expert Member
- Jan 23, 2016
- 327
- 208
Tuiangalie elimu kama bidhaa na huduma zingine kwenye soko la biashara. Bidhaa yeyote ile kukiwa na demand ikipanda basi na bei itapanda. Lakini bei inashuka kukiwa na mashindano. Sasa kukiwa na watu walio na hela nyingi za kutumia na kununua hiyo bidhaa basi watoa bidhaa wanapandisha bei wakijua watu wataweza kulipa.
Elimu ya juu ya University ndivyo hivyo hivyo. Kuna demand ya elimu ya juu sasahivi kwahiyo bei inapanda.
Kinachozidi kuipandisha bei ni mikopo kutoka kwa serikali kwenda kwa wanafunzi. Haijalishi hao wanafunzi wanasoma nini lakini as long as kuna hela ambayo hao wanafunzi wakiidai kutoka kwa serikali wataipata basi watoa huduma au wauza elimu ambao ni university wataongeza bei kwasababu bidhaa yao iko in demand.
Serikali haielewi matatizo inayoyasababisha kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi. Cha kwanza ni kwamba inaongeza bei ya elimu kukua kwasababu inaongeza demand.
Cha pili ni kwamba kila mtu atataka mkopo akati wengine hawana akili za kwenda elimu ya juu na wanaenda kusomea mambo ambayo hayahitaji university.
Hao wataishia kumaliza kusoma na kukosa kazi na kukosa uwezo wa kulipa mikopo.
Mikopo ingekuwa inatolewa na benki binafsi, benki zenyewe zingekuwa zinafanya jitihada kubwa zaidi ya kuchagua nani mwenye akili anayeweza kutumia mkopo huo kusoma kwa bidii na anafaa kupata mkopo. Hii ni kwasababu ingekua ni hela ya hizo benki ambazo zingepotea kama wangechagua kuwapa wanafunzi wajinga mikopo. Kwahiyo wangekua makini kuto toa mikopo ovyo ovyo na hii hatua ingepunguza idadi ya demand ambayo ingepunguza bei ya elimu ya juu.