Mikopo ya Kilimo na mifugo kwa mkulima mmoja mmoja

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wakuu habarini

Nimenunua eneo kwa ajili ya ufugaji wa nguruwe , kuku na mbuzi. Tayari nimeshajenga banda la nguruwe kwa kutumia matofali ya kuchoma yaliyojengwa na cement na kuezeka kwa mabati yaliyotumika. Nimeshanunua nguruwe 10 wenye umri wa miezi 4. Hili limekamilika kwa 100%.

Kwa issue ya ufugaji wa kuku, nimeshanunua wavu (BRC) tu. Bado mabati used na mambo mengine , kuku bado sijawanunua.

Nimekwama mtaji /hela ya kusonga mbele ili kukamilisha yote hayo.

Ni wapi naweza kupata mkopo wa kama 1.5 mil?

Asanteni
 
Hao nguruwe 10 umenunua Tsh ngapi? Maana naona kabisa hapa ilikuwepo hiyo 1.5M unayotaka ukope kama ungeamua kuanza na nguruwe wachache. Hata watano!
 
Harafu ukipigwa za uso unarudi kuongea peke yako barabarani.

Project za ufugaji usizichukulie poa hivyo, kuku unaweza kununua 100 mara wakataga mara wakafa wote

Anza na mradi huo huo wa mbuzi katoliki kwanza kisha kidogo kidogo unakuja faida ndiyo unaendeleza kujenga miundombinu. Mambo ya kukopa kwa hapo tu inaonesha miundombinu humudu sana imeashiria tu kwenye mabati used. Ungekuwa unatengeneza mabanda ya kisasa kama cages hapo ungekuwa unauhakika wa kukopa.

Ushauri endelea kupata uzoefu na hao madude kisha save money jenga mabanda, usikimbilie mafanikio kwa haraka hivyo ndani ya mwaka mmoja, unavyoendelea utajifunza mengi hata changamoto za masoko pia
 
..nashauri uendeleze mradi wa nguruwe, halafu faida utakayopata ndio ikusaidie kuanzisha mradi wa kuku, etc etc.

..kwasababu ndio kwanza umeanza ufugaji / ujasiriamali siyo vizuri ukawa na pressure za kulipa deni kipindi hiki cha mwanzo wa safari yako ya ujasiriamali.

..all the best.
 
Back
Top Bottom