Mikopo ya haraka inapatikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikopo ya haraka inapatikana

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by sanya juu, Feb 7, 2009.

 1. s

  sanya juu Member

  #1
  Feb 7, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  MIKOPO HARAKA INATOLEWA KWA WALE WOTE WENYE KUHITAJI HELA ZA HARAKA KWA AJILI YA BIASHARA ZAO NA MAHITAJI MENGINE.
  HAKUNA URASIMU. MASHARTI YA KUPATA MKOPO NI KUWEKA DHAMANA YA GARI.
  MAWASILIANO,NITUMIE MESEJI NO YANGU NI 0782440468
  AU EMAIL. somigroup@yahoo.com
   
 2. s

  sanya juu Member

  #2
  Feb 9, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wale wote wanaohitaji mikopo ya hela tuwasiliane.
  Kuna kampuni inatoa mikopo ya hela ya haraka.
  Masharti ya kupata mkopo unatakiwa kuweka dhamana gari lako.
  Mawasiliano zaidi ntafute kwa 0713902202
   
 3. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  Mimi nahitaji mkopo wa kununua gari, sasa dhamana ya gari nitaitoa wapi wakati ndio kwanza nahitaji kupata fedha ili ninunue hiyo gari? Sidhani kuwa watu wengi wenye kuhitaji mikopo kama tayari wanamiliki magari. Labda kwa faida ya jamii kwa ujumla ungeweka Vipeperushi (bronchure) zao hapa ili watu waweze kupitia na kufahamu zaidi kabla ya kukupigia simu. Isije kuwa dili!
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Feb 9, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mkuu weka mambo yote hadharani kampuni yako inaitwaje iko wapi tovuti yake kama ipo pamoja na mambo mengine kwa mawasiliano zaidi kuna member mmoja zamani aliweka tangazo kama hilo badala yake watu walichukuliwa magari yao kule katika chatroom mpaka huku yupo
   
 5. T

  Tango Member

  #5
  Feb 9, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Tunataka kujua pia na interest na mambo ya namna hiyo. Isije ikawa kama kampuni moja iliyokwisha kujadiliwa kuwa inawaumiza walimu kwa mikopo ya haraka haraka
   
 6. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuna vijana wanajaribu biashara ya kukopesha kwa kuwazurumu wenzao. Naita kuzurumu kwa sababu masheriti yake ni yakihuni na hayapo katika taratibu za mikopo ulimwenguni. Utakuta mtu anakwambia riba ni '' kila shilingi 1000 unarudisha shilingi 200 kwa siku sasa we piga hesabu mfano umekopa laki moja. Maana yake kama ni mkopo wa mwezi mmoja utatakiwa kurudisha 100,000/1000 *200*30 = 600,000. Huu ni wizi mkubwa kwa maskini watanzania wenzetu. mtu anakopa 100,000 analipa 600,000. Huyu mheshimiwa aweke terms zote hadharani asije waumiza ndugu zetu huko
   
 7. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Msituletee utapeli hapa. Ni kwa vipi mikopo ikatolewa kwa movable assets kama magari? hili linahitaji kupata undani zaidi kabla ya kulivaa kichwa kichwa.
   
 8. GP

  GP JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  huu kweli ni WIZI MTUUPU!, yani ukope laki moja ulipe laki sita jamani?, duh!. hii inakua kufa kufaana.
  lakini vp kuna kampuni moja nadhani inaitwa DECI hii iko mabibo na maeneo kadhaa wana ofisi zao, wao wanaita kupanda na kuvuna, kwa mfano ukiweka laki moja baada ya miezi 3 inazaa laki 2.5, wanakata 15% na kutoa mbegu(100000) unapata 127500, hii iko vipi haiwezi kuja kuleta magumashi hapo baadae kama GTV kwa kisingizio cha kufilisika?
   
 9. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mkuu

  Hata mim nahitaji mkopo ili niweze kununua Gari. Sasa unaniambia niweke dhamana Gari NTALITOA wapi?. Tisaidie watanzania wenzako na sisi tuwe na Magari na si kutuambia tuweke dhamana Gari wakt gari sina. Nisaidie ili niweze kununua hilo gari. Interest ni % ngapi. Weka mambo hadharani acha bla bla hapa
   
 10. Piemu Esquire

  Piemu Esquire Member

  #10
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kama dhamana ni gari,umri wa garije manake mie nina gari aina ya fomoko la mwaka 1935 nilipewa urithi na babu yangu,Lina hati zote za kulimiliki na bima hadi 2010 .Swali je litakubalika kama dhamana?
  Isitoshe kiasi chenyewe cha mkopo na thamani ya gari vinaendana?Kwani RAV 4 yangu mpya ya mwaka 2008 ina thamani ya Tshs,78Mil.Wasije wakasema kiwango cha mkopo kisizidi SH.10Mil.kwa dhamana ya RAV 4 yangu.
  Huu waweza kuwa ni utapeli wa kiaaina kwa sababu kijiwe hicho hakina kibali cha BOT kufanya biashara ya fedha.Wadau muwe waangalifu hata kama magari hamna lakini ndugu zenu wanayo WATAHADHARISHENI NA MATAPELI HAWA.
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280


  Wewe sanya juu weka mambo hadharani hapa ili adau watoe maoni kuhusu hiyo kampuni. We need copmany profile hapa na reference ya wateja reputable ambao wamefaidika nao. Kumbuka ile thread ya DECI ambayo inatoa mikopo watu waliweza kuichangia vilivyo kwa sababu tulipata reference humu ndani ya forum japo wengine akiwemo Mzee Mwanakijiji alitutahadharisha na aina ile ya biashara. Tumechoka na matapeli hapa. Je gari yangu sema nikichukua mkopo wa miezi mitatu nikaiacha pale itakuwa inafanya kazi gani?? Usikute wenye kuacha soloons zitakuwa taxi bubu za usiku???/!!! Kuwa macho!!!!
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Na sisi tulio mikoani tufanyeje? Kwa nini usiweke anwani kamili kama vile Jina la Kampuni, Anwani ya Posta na barua pepe, mahali ilipo-Jengo/Mtaa ili kuondoa gharama za kukupigia simu?
   
 13. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Sanya juu nyumbulisha vigezo na masharti...
  Tusker Bariiiidi!!!
   
 14. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF mnataka mikopo mkakope katika Benki zinazotambulika au mjiunge na SACCOS msijihusishe na vikampuni vya mitaani msije mkaingizwa mjini.
   
 15. s

  sanya juu Member

  #15
  Feb 10, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mawasiliano ya simu ni rahisi sana hata kwa meseji inatosha kukuelewesha na maswali yako kujibiwa hata kukuelekeza ukitaka kuja ofisini.
  riba asilimia 30 ya mkopo.
  mkopo utakaopata unakuwa nusu ya dhamani ya gari yako
  Mfano gari yako ina dhamani ya milioni 50 unakopeshwa milioni 25.
  muda wa mkopo mwezi 1.
  Baada ya mwezi 1 unarudisha milioni 32500000.
  mikataba yote inasimamiwa na wanasheria.hakuna udanganyifu.
  garama za kulipia valuation ya gari yako kujua dhamani yake unalipia wewe mwombaji mkopo.
  aliyekuwa serious awasiliane na mimi namba 0713902202 nitamuelekeza atakuja ofisini na jina la ofisi atalijua .
   
 16. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Sanya Juu

  AchaUfisaji kwa Watanzania wenzako, RIBA 30%???????????...UUUUUUUUUUUUUUUUFFFFFFFFS. Halafu eti muda wakulipa mkopo ni Mwezi mmoja(1) UMELOGWA sio?
   
 17. s

  shorty Member

  #17
  Feb 10, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani naomba tuwe makini...duuh hii ni soo Tzs 7.5million per month kwa 25million???in a year INTEREST alone kwa "mkopo" wa 25million ni 90million...that is 360% interest per year guys..are you serious abt this mkuu?add the principal of 25million that is 115million..man afadhali uende BANK kwenye 22% interest PER YEAR..
  life is abt information...
   
 18. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Riba 30%??? halafu kwa mwezi mmoja????!!!!!

  Sanya wewe, wizi huu ni zaidi ya ufisadi. Biashara gani hiyo mtu atafanya kwa mwezi mmoja aweze kurejesha 30%???

  Yaani ukopeshe 25,000,000. Baada ya Mwezi urejeshewe 25,000,000/= na zawadi ya 7,500,000/=. Kama inawezekana kuchuma 7,500,000 kwa mwezi mbona wote wangeshakuwa matajiri? Kwa mTz wa kawaida anayelipwa 800,000/= kwa mwezi hiyo ni pesa nyingi sana! Kwa nini ni Ahangaike na ajira??

  Kwa maneno mengine wanakuibia 25,000,000/= (nusu ya thamani ya gari lako, na wao wataliuza kwa gharama halisi ya millioni 50. Hii itawafanya wapate jumla ya 75,000,000 faida tupu!) huku ukiwa umejisainisha mkataba wa kuibiwa. Ukifanikiwa kurejesha watakuwa wamekuibia 7,500,000/= wa sign yako mwenyewe.

  Jamani waTanzania fungukeni macho na wezi/mafisadi hawa. Tena wanakukamatisha kisheria, wakuibia gari lako la millioni hamsini kwa sababu wanajua kabisa kwamba si rahisi wewe kupata faida ya zaidi 7.5 m kwa mwezi itakayokufanya urejeshe huo mkopo.
   
 19. S

  Simoni Member

  #19
  Feb 10, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wewe Sanya juu!!Tukupe magari yetu halafu ukayauze kama vyuma chakavu. Hebu acha hizo eboo
   
 20. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  We kijana wa Arusha unakijua unacho kisema hapa? Hivi niambie utafanya biashara gani wewe in one month upate more than 30% ya capital uliyoinject kwenye business? Wewe unacho sema ni kwamba;

  Jan 1: Unanipa Tshs 1,000/=

  Feb 1: Nakurudishia Tshs 1,000 + 30%*1,000=1,300!

  Ukiacha hiyo hesabu hapo juu, natakiwa kugharimia initial costs like lawyer's fees, evaluation fees, stamp duty (1% ya contract value). So ukiziunganisha hizi costs, then ukacalculate THE EFFECTIVE INTEREST RATE itakuwa ni higher than 50%.

  Pia hapo sija take into account the taxation effect!

  So ilikuweza kuzilipa hizo gharama in one month, natakiwa kupata faida ya more than Tshs 1,000 kwa mwezi......this is super normal profit, ambayo sijui ni biashara gani inawezekana kama si UFISADI!

  Bwana Sanya, hivi hiyo biashara ya hela mna kibali chochote kutoka BOT au mamlaka yoyote? wanajua kuwa mnawacharge watu 30% interest kama riba? na je, mmesajiliwa na BOT and BRELA?

  No to any of these questions, means nyie ni wezi na matapeli!
   
Loading...