Mikopo ya elimu ya juu mpaka leo waombaji wako njia panda

Arabi Nanjewa

JF-Expert Member
Sep 22, 2017
325
410
Ndugu zangu wanabodi, kumekuwa na kizungumkuti kikubwa sana katika suala hili la mikopo ya elimu ya juu. Na hii ni kutokana na ukweli kwamba waombaji wa mkopo mwaka wa masomo 2017/2018 hawajui la kuganya.. Aidha mwanzoni kabisa tuliona mvutano mkubwa kati ya HESLB na wadau mbalimbali wa elimu ya juu kama vile mtandao wa kutetea wanafunzi tanzania ambapo kulikuwa na vuta nikuvute kuhusu vigezo vya mwaka huu vya waombaji (tulishuhudia EATV kipindi cha hot mix siku moja ambapo mkurugenzi wa bodi alikuwa anatolea ufafanuzi jambo hili... Ila cha kushangaza zaidi siku kadhaa zilizopita kulienea taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusisha waombaji takribani elfu kumi na sita hatarini (kama sikosei) ila mpaka leo hayajatolewa majina ya waliokosea ili waweze kurekebisha..bikumbukwe waombaji wengi ni watoto wa wakulima ambao kama si mkopo ni vigumu kuendelea na elimu ya juu... Ningeomba HESLB walione hili..
 
mkiandamana safari hii na nyie tunawapima mikojo kuangalia kama nlipas kidato cha sita
kudaaadeki.
 
  • Thanks
Reactions: m2u
Majina yatatolewa tuu hata mwaka jana walitoa so kuwen na subira tuu mambo yataenda sawa ila tusisahau kuomba mungu kuweka wepesi wake
 
  • Thanks
Reactions: m2u
Hakuna namba ambayo itaachwa kusomwa,mapigo ya JPM yanapiga yeyote bila yakujali huyu ninani.
 
Nilivoambiwa na official wa heslb ni kwamba majina yatatoka two hadi three weeks kabla hatujafungua vyuo
 
Back
Top Bottom