Mikopo ya elimu itolewe kwa wanafunzi wanaosomea fani za vitendo tu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,903
Kwa utafiti wangu wengi wasio na ajira ni wale waliosomea digrii za bla bla zisizo za vitendo mfano za sheria, Bussiness Administration, Uchummi, Uhasibu, Uandishi wa Habari nk.

Serikali itoe mikopo kwa wanaosomea fani kama Engineering, Kilimo na Ufugaji, za Ujenzi na Uvuvi, Udaktari, Ufamasia nk.

Hizo digrii za blabla serikali imapoteza tu pesa zake kukopesha watu ambao ni vigumu kuajirika au kujiajiri hivyo mikopo kushindikana kulipika.
 
tatizo huyo mtu wenu kiswahili fasaha hajui kingreza ndo balaa kabisa...hivyo haeleweki!.
 
Vocational training kuna siku tutakuja kuiamkia "shikamoo"

Narudia tena Chuo kimoja cha Ufundi Stadi (VETA) kilichokamilika ni bora kuliko shule 100 za sekondari

Najua hamjanielewa

Au nasema uongo ndugu zangu??
Upo sawa mkuu
 
Wote tukisomea hizo fani za vitendo kwa kufuata mkopo hizo shughuli zingine ambazo zinahitaji usomee fani isiyo ya vitendo zitafanywa na nani?. Kama ni hivo hata kwenye ulipaji wa kodi wafanye exception kwa waliokuwa hawana kazi waondolewe kodi kwenye manunuzi watakayofanya
 
Kwa utafiti wangu wengi wasio na ajira ni wale waliosomea digrii za bla bla zisizo za vitendo mfano za sheria, Bussiness Administration, Uchummi, Uhasibu, Uandishi wa Habari nk.

Serikali itoe mikopo kwa wanaosomea fani kama Engineering, Kilimo na Ufugaji, za Ujenzi na Uvuvi, Udaktari, Ufamasia nk.

Hizo digrii za blabla serikali imapoteza tu pesa zake kukopesha watu ambao ni vigumu kuajirika au kujiajiri hivyo mikopo kushindikana kulipika.
Kiongozi wa North Korea aliwahi kuulizwa, mnawezaje kujitegemea na mnavikwazo kila kona. Moja ya jibu lake alisema elimu yao wameiplana kuwa humanity science ni asilimia 30 tu. Asilimia 70 ya wanagunzi chuoni walikuwa wanachukua Natural science. Upo sahihi. Sayansi hata nje ya nchi unaajirika kirahisi. Hata ukienda nchi wanaongea lugha ambayo huijui utaajirika.
 
Back
Top Bottom