Salaam kwenu wadau wa maendeleo humu JF;
Katika harakati nyingi za kujikwamua na maisha binadam anatumia kila fursa illiyopo mbele yake ili afanikiwe na kujikwamua katika shida zinazomkabiri;
EPUKA KUKOPA PASIPO NA FAIDA;
Katika vitu vinavyo ua watu siku hizi mikopo ni moja wapo,Ndugu zangu kabla hamujaamua kukopa pesa nyingi SACCOS,VIKOBA na BANK ebu jaribuni kutafta njia nyingine ya kufanikisha jambo lenu, Mikopo mingine hailipiki, Kukopa ni sawa na kutoboa mifuko yako mwenyewe pasipo kujitambua, Punde ukishakopa pesa zako zote zitaishia kwenye marejesho yaliyojaa riba, ambapo hautakaa kwa amani kwa stress ya deni kwa kuhofia dhamana kuuzwa na kuadhiliwa vibaya. Sifa kuu za mikopo ni kuanzia sirini ila huishia kudhalilishwa hadharani, mikopo ni sawa na mimba itungwapo sirini ila inapokuwa kila mtu hujuwa kwamba yule alifanya mapenzi tena bila kinga ndio maana ANA MIMBA.
Punde ukisha kopa basi wewe ndiwe utafanyika mtaji utakaekuwa unachakarika na kuhangaika huku na kule kuwataftia wenyewe ambao wao wanahesabu siku tu ushindwe wapulize.Tena hakuna kitu kizuri kwa bank kama mteja anaposhindwa kulipa yaani wanafurahi kwelikweli maana hela yao hurudi kwa haraka na penalty kibaooo.
MIKOPO MINGI INA LAANA ZA KISHIRIKINA;
Epukeni kukopa hovyo kwa watu na vijitaasisi uswahilini kwa dhamana kubwa, ikubukwe shida humfanya mtu awe hajitambui, mtu anakukopesha elfu 50000/= unaweka dhamana FRIJI LA NDANI, tena bila mke/mme kujua, mtu anakopa laki 5 anaweka dhamana gari, watu wengi hawajui kama kuna uchawi katika haya, ndugu zangu punde unaposaini makubaliano ya mikopo basi utaipata na mazingaombwe yake wallah mkopo ule utakusumbua mpaka utakushinda, inaweza ikatokea ukapata kabisa ile pesa ila hautarejesha kwa kujifariji utapata nyingine punde kumbe ndio kiini macho cha kufirisiwa dhamana yako.
MKOPO HUZAA MKOPO
Punde unapoingia kwenye jinamizi hili zito la mikopo, kaa ukijuwa Shetani anagonga mlango kukufirisi, Hakuna wakati mgumu kama ukiwa na rundo la madeni, kila siku wewe utakuwa mtu wa kukopa tu.Hela utakayopata utaishia kulipa riba tu, kumbuka mikopo huwa ina penart ambazo wengi wao hushindwa…EPUKENI MIKOPO ISIYO YA LAZIMA NI SHETANI
SHUHUDA ZA MIKOPO ZILIVYOFIRISI WATU.
1. Kuna jamaa mmoja ninamfahamu, alikopa pesa mil 30 katika Bank moja, akanunua FUSO la kubeba mizigo kwenda Zambia, kwakuwa aliona watu FUSO inawalipa naye akakopa akijuwa, likipeleka mzigo na kurudi dar anakunja mil 2 CASH, alifanikiwa kuagiza gari ile na alipoipata bandarini kuitia mkononi ikamlamba kama mil 4 kwa marekebisho madogo madogo, ILE FUSO ilienda Zambia trip moja tu HAIJAWAHI rudi hadi leo, Na bora isingerudi kwa kuibiwa bali ilikula mkenge wa maana kule iringa wakatoa injini tu, na shehena ya mzigo ikapotelea kitonga. Bank wakafirisi shamba zuri lililokuwa kimara.
2. Kuna Bosi wangu mmoja mhindi hapo kariakoo kakonda kaisha kisa alichukua mkopo katika Bank moja ambapo mpaka sasa anarejesha riba tu, katangaza kuuza YARD yake na haiuziki, na hata akiuza bado haitafaa kumaliza deni lililojaa penalty.
3. DILI ZA KUTAJIRIKA HARAKA ZINAVOWAUA VIJANA-Kuna watu wanapata kazi tu na kukimbilia mikopo ya magari halafu hela ya parking tu shida, hela ya mafuta tu ni shida, na magari hayawaiingizii faida zaidi ya hasara huku mikopo ikiendelea kuwatafna.
Wanaofanikiwa kwa mikopo inakadiriwa kuwa ni asilimia 20% tu. Wengi huteketea na kushindwa, Ikumbukwe kwamba wengi wanaofanikiwa kupitia mikopo huwa wanahisa katika Mabank hivyo kuna unafuu wa urejeshaji kuriko wewe mgeni.