MIKOPO tele iliyochukuliwa na serikali kwa miaka michache iliyopita, sasa inaweka Kenya katika hatari kubwa ya kuzama kiuchumi kupitwa na Tanzania

Kingmaja

Member
Sep 15, 2018
68
109
Na Majaliwa Abdulkadli Amran

MIKOPO tele iliyochukuliwa na serikali kwa miaka michache iliyopita, sasa inaweka Kenya katika hatari kubwa ya kuzama kiuchumi kupitwa na Tanzania.

Wakati huu wa janga la corona, Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayoathirika sana kiuchumi.

Kwa msingi huu, wataalamu wanasema ingehitajika taifa litenge fedha ambazo zingesaidia kufufua uchumi wakati janga la corona litakapoondoka. Badala yake, imebainika fedha nyingi zimetengewa ulipaji madeni kwenye bajeti ya mwaka huu wa kifedha.

Wataalamu hao sasa wanapendekeza serikali iangalie upya makadirio ya bajeti hiyo ya Sh3.15 trilioni ya mwaka wa kifedha wa 2020/2021.

Afisi ya Bajeti katika Bunge (PBO) pamoja na Mbunge wa Gatundu Kusini, Bw Moses Kuria, walitambua kwamba katika bajeti hiyo ambayo ndiyo kubwa zaidi kuwahi kuwepo nchini, fedha zilizotengewa masuala ya corona ni Sh2.6 bilioni pekee.

Hizi si fedha ambazo zitatumiwa kuinua uchumi na kulinda wananchi kiriziki, bali zimenuiwa kutumiwa kupima wananchi kwa wingi ili kubainisha walioambukizwa virusi vya corona.

“Kwa kuzingatia janga linalotukumba, mkakati mwafaka ambao umeshuhudiwa kimataifa, ungekuwa ni kutenga fedha za kufufua uchumi. Hili lisiwe tu kwa minajili ya kusaidia kiafya na kimapato katika kipindi hiki cha sasa, bali kwa ufadhili wa awamu nyinginezo za kuboresha uchumi baada ya janga la corona. Bajeti ya 2020/2021 imefeli katika hili,” afisi hiyo ikaonya, kupitia kwa arafa iliyowasilishwa bungeni.

Madeni
Madeni ya Kenya kwa jumla yalipita Sh6 trilioni kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2019, kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Kenya (CBK).

Baadhi ya mikopo ilichukuliwa kutoka China na serikali ya Rais Uhuru Kenyatta, ikisemekana itatumiwa kustawisha miundomsingi.

Hata hivyo, wachanganuzi wa kiuchumi na baadhi ya wanasiasa hukashifu serikali kwa kutumia vibaya fedha hizo kwani mwananchi wa kawaida hajanufaika.

Inahofiwa China inaweza kutwaa mali muhimu za taifa ikiwa Kenya itashindwa kulipa madeni hayo kwa muda unaofaa, kama vile Bandari ya Mombasa, ingawa serikali hukana kulikuwa na makubaliano ya aina hii.

Mataifa ya Afrika yamekuwa yanajikakamua kuomba nchi za nje ziwaruhusu kutolipa madeni hadi janga la corona litakapoondoka, lakini suala hili halijafaulu kufikia sasa.

“Endapo China itakubali kupunguza mzigo wa madeni, itasaidia kuondoa dhana kwamba walituwekea mtego,” mtaalamu wa masuala ya kifedha kimataifa, Bw Leonard Wanyama, akasema.

Kwa sasa, serikali inahitaji kukopa Sh1.3 trilioni nyingine kujaza pengo katika makadirio ya bajeti. Hii itaongeza madeni hadi takriban Sh7.2 trilioni.

“Hili haliwezi kugharamiwa. Omba omba hawana aibu. Inafaa tuambie wale tuliokopa kutoka kwao kwamba hatuna uwezo wa kugharimia madeni yetu hadi mwaka wa 2023. Hivyo, tutapata Sh1 trilioni ya ziada kila mwaka kwa miaka mitatu,” akasema Mbunge Kuria, ambaye pia ni mtaalamu wa kifedha.

Hayo yanatokea wakati ambapo karibu shughuli zote muhimu za kiuchumi zimekwama, na zile chache zinazoendelea zikiwa zinajikokota.

Bw Kuria, kwenye taarifa yake, alisema Kenya ilikuwa tayari inatatizika sana kifedha kabla ya janga la corona na hali itakuwa mbaya zaidi kama maafisa serikalini hawatatumia busara kuhusu bajeti ya taifa na matumizi.
 
watu wakilala wakiamka habari ni kuhusu tanzania kuipita kenya kiuchumi.
Imagine, hadi nashindwa kuna nini? na hili jambo walianza kulisema tangu 2017 hadi wa leo ..uchumi ya kenya bado inazidi kupanda, gap bado linazidi kuongezeka.
 
Kwan hiyo habari si imeandika na mkenya mwenzenu
Hebu niambie umejuaje kuwa Majaliwa Abdulkadli Amran ni mkenya? Kwa sababu mimi simfahamu
Alafu pili aliyeleta hiyo taarifa hapa jukwaani ni mtanzania
 
We've been hearing this song for over 15 years now yet the gap increases.
Kwa hii wimbo ya kuipita Kenya wajitayarishe kufunza vitukuu wao, vile mababu zao waliwafunza. Kwa sahi GDP ya eac (nchi zote za eac) kiujumla ni $220 billion. Kwa hiyo $220 billion, Kenya iko na karibu 50%, ikiwa na $109 billion GDP (Hiyo ingine igawanywe kati ya nchi zilizobaki), kwa hivyo wajitayarishe koo.

Kufikia mwaka 2029 Kenya itakuwa na uchumi kubwa kushinda nchi zote za eac zikiunganishwa.
 
Hebu niambie umejuaje kuwa Majaliwa Abdulkadli Amran ni mkenya? Kwa sababu mimi simfahamu
Alafu pili aliyeleta hiyo taarifa hapa jukwaani ni mtanzania
Hamna mtanzania anaweza kuandika kiswahili kibovu hivyo, hata mtoto wa darasa la 3 anamshinda uandishi na lugha
 
Kwa hii wimbo ya kuipita Kenya wajitayarishe kufunza vitukuu wao, vile mababu zao waliwafunza. Kwa sahi GDP ya eac (nchi zote za eac) kiujumla ni $220 billion. Kwa hiyo $220 billion, Kenya iko na karibu 50%, ikiwa na $109 billion GDP (Hiyo ingine igawanywe kati ya nchi zilizobaki), kwa hivyo wajitayarishe koo.

Kufikia mwaka 2029 Kenya itakuwa na uchumi kubwa kushinda nchi zote za eac zikiunganishwa.
Tanzania tumekua vinara toka 1960s mpaka 1980s na 1990s & 2000s so tunao uzoefu wa kutosha kabisa kwenye hiyo nafasi na in fact sisi ndio powerhouse kwenye hii region
 
Deni lingine kubwa kuliko lolote ni la kugharamia uchaguzi wao wa 2022, yaani hapo lazima wafike trillion 15, sababu kuanzia saivi mpaka 2022 hapa katikati watakopa zaidi kugharamia budgets zao kwa zaidi ya 70%

Hahahaha mpaka raha, nataka nione Kenya inapigwa mnada na majembe auction mark
 
Hamna mtanzania anaweza kuandika kiswahili kibovu hivyo, hata mtoto wa darasa la 3 anamshinda uandishi na lugha
hio ndio sababu...kuna watanzania hawawezi kuandika kabisa afadhali huyo wakiswahili kibovu
 
Tanzania tumekua vinara toka 1960s mpaka 1980s na 1990s & 2000s so tunao uzoefu wa kutosha kabisa kwenye hiyo nafasi na in fact sisi ndio powerhouse kwenye hii region
we jamaa yafaa uamshwe...nadhani uko ndotoni
 
hio ndio sababu...kuna watanzania hawawezi kuandika kabisa afadhali huyo wakiswahili kibovu
Ninyi ndio mnaongoza ukanda huu kwa kutokujua kuandika na kusoma
2507261_cross-country-literacy-rates.png
 
Gap fake,cause it doesn't relate with Kenyan majority way of life, economic holded by Mr freedom and his team .

Wash your ✋, Corona bado ipo
 
Deni lingine kubwa kuliko lolote ni la kugharamia uchaguzi wao wa 2022, yaani hapo lazima wafike trillion 15, sababu kuanzia saivi mpaka 2022 hapa katikati watakopa zaidi kugharamia budgets zao kwa zaidi ya 70%

Hahahaha mpaka raha, nataka nione Kenya inapigwa mnada na majembe auction mark
😃😃😃
 
Back
Top Bottom