Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
- Thread starter
- #21
Unasema kweli, huwa sipendi mijadala ya kulaumu mtu ama Chama na kusahau wajibu wa waliowaweka hao madarakani.Inamaana sisi ni wajinga kiasi gani?
Mpaka Leo tunatembelea mambo ya Nyerere hata kama yana kasoro?
Tukae kumlaumu MTU aliyekufa zaidi ya miaka 20 iliyopita wakati sisi uwezo Wa kurekebisha tunao
Kitu ni simple tu kubadili au kurekebisha katiba baaaaasi
Tusisahau kuwa, haki na wajibu ni vitu viwili vinavyoshirikiana katika masuala ya demokrasia na haki za hinadamu.
Ukiwa mzuri kudai haki zako, jitahidi pia uwe mzuri kufahamu wajibu wako katika kuzidai hizo haki hasa mipaka ya haki zako.
Kama Katiba ndilo suala muhimu, mbona wapiga kura huwa hawachagui wanaopiga kampeni za Katiba Mpya. Je, ni kosa sisi kudai kuwa, wanaodai Katiba Mpya ndio hawawaelewi wananchi wanachotaka?