Mikopo tarajiwa ya China kwa Tanzania inayofikia Trilioni 46 kwa ajili ya Bagamoyo Port na SGR, hatarini kushikilia vitega uchumi vya Tanzania

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
IMG_0277.JPG

Gazeti la The Guardian, lina taarifa inayoeleza kuwa, Mkopo wa China kwa Tanzania, ambao mpaka sasa ni Tsh. Trilioni 5.3 (U$ 2.347 Billion), unaweza kuongezeka maradufu hadi zaidi ya Trilioni 23 (U$ 10 Billion) endapo fedha zilizoombwa kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya SGR (U$ 7.6 Billion), pamoja na Mradi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Mchuchuma-Liganga (U$ 3 Billion) utaidhinishwa.

Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa akipinga kuchukua mkopo mkubwa mwingine wa Trilioni 23 (U$ 10) kwa ajili ya Mradi wa Bandari ya Bagamoyo kwani mikopo hiyo inaweza kuisababishia Tanzania kuingia deni kubwa na China linalofikia Trilioni 46 (U$ 20.6 Billion).

China bado inagumia kimoyomoyo na kuugulia maumivu ya kuumizwa kwa ego yao kwa namna Rais Dk. John Pombe Magufuli alivyofanikiwa kuruka kiunzi chao cha kumzungusha mkopo wa kujenga Reli ya SGR, kwa kuupata Uturuki. Uamuzi wa Magufuli ku-opt Waturuki ulikuwa ni wa kijasiri sana kutokana na kwamba Uturuki haijihusishi sana na Afrika kwenye miundombinu ya kisasa barani Afrika kama zilivyo China, Japan na Ulaya Magharibi.

Aidha, Tanzania ilichelewesha Mradi wa Uwekezaji wa Bandari ya Bagamoyo na kuzua hofu kwa Wachina juu ya uwezekano wa Mradi huo kusitishwa.

Hivyo, kwa namna yoyote Wachina watakuwa na hasira na Tanzania japokuwa hawawezi kuionyesha wazi wazi kutojana na kuona kuwa Tanzania ina Rais asiye na mzaha kabisa kwenye masuala ya kulinda maslahi na rasilimali za Taifa lake, huku muda wote akipigania a win-win situation.

Kenya inayodaiwa na China U$ 9.8 Billion kwa sasa inahenyeshwa sana na China, hali ambayo imepunguza hali ya utulivu wa kiuchumi nchini humo. China imesita kufadhiri SGR kipande cha Kisumu - Malaba kwa kigezo cha kuwa uneconomical.

Kenya ina uchumi mkubwa zaidi kuliko Tanzania na ukiacha Mradi wa Mafuta ya Lokichar (Turkana - Lamu Pipeline) na SGR (Mombasa - Kisumu - Malaba), haina Miradi mikubwa mingi inayoipa headache kama ilivyo kwa Tanzania ambako kuna Miradi mikubwa mingi ikiwemo:
  • Stiegler's Gorge (Rufiji HEP): gharama U$ 3.6 Billion;
  • SGR (Dar - Dodoma - Mwanza & Kigali): gharama U$ 7 Billion;
  • Bomba la Mafuta ya Uganda (Hoima - Tanga Pipeline): gharama U$ 3.5 Billion;
  • Kiwanda cha Kuchakata Gesi (LNG), Lindi: gharama U$ 30 Billion.

Endapo Mkopo huo wa U$ 7.6 Billion utaidhinishwa na China, utaifanya Tanzania ambayo kiuchumi ni ya 10 barani Afrika, ikiwa na GDP (PPP) ya U$175 Billion, kuwa ya pili nyuma tu ya Angola (yenye deni la U$ 42.8 billion) kwa Nchi zenye madeni makubwa kutoka kwa China barani Afrika. Hata hivyo, Angola ina utajiri mkubwa wa mafuta wa kuiwezesha kulipa deni hilo, tofauti na Tanzania ambayo haina chanzo kikuu cha mapato mpaka sasa.

Lisemwalo lipo, kama halipo basi laja. Baada ya kuzagaa kwa taarifa kuwa, China imetaifisha vitega uchumi kadhaa katika Nchi za Djibouti, Zambia na Kenya kwa kushindwa kulipa madeni.p, kumesababisha hofu kubwa kwa Waafrika dhidi ya China; Nchi iliyoonekana kuwa kimbilio na mkombozi wa Afrika katika miaka ya 2000s lakini leo hii inaanza kuonekana Nchi isiyo na huruma kwa Waafrika.
Licha ya hatua kadhaa kuchukuliwa na Serikali ya China ya ku-address hofu hii ya Waafrika dhidi yao, bado zimeshindwa kuondoa wasiwasi huu kwa wananchi wengi hadi kuwa mojawapo ya ajenda zinazoibuka mara kwa mara katika Sera za uwekezaji na za maendeleo ya kiuchumi.

Ni wazi pia, fursa ya haraka haraka iliyoletwa na Rwanda, ilikuwa ni kubwa sana kiuchumi. Of course, kulegalega kwa kipande cha SGR kutoka Kisumu - Malaba (Kenya) kulionekana machoni mwa Wanyarwanda kuwa, Wakenya hawakuwa serious na Mradi wa SGR kutoka Mombasa - Nairobi - Kisumu - Kampala - Kigali.

Of course, ni wazi Rais Dk. John Magufuli kupitia maelewano na Paul Kagame, ilisaidia sana Rwanda kuigeukia SGR ya Tanzania, ambayo ilkuwa imeshaanza kujengwa katika kipande cha Dar - Morogoro. Sasa, unafanyaje kuifikisha haraka SGR kutoka Dar hadi pale Rusumo, Ngara? Ukichelewa, Rwanda wanaweza kubadilisha tena gia angani na kurudi kwa Wakenya.
Rwanda kwa sasa inapitishia asilimia 40% ya mizigo yake Bandari ya Dar, hivyo SGR ikikamilika, mizigo itaongezeka maradufu siyo ya Rwanda pekee bali ya Mashariki ya DRC, Burundi na Kusini mwa Uganda.

Kwa kuwa, wakati Serikali inatangaza kuanza ujenzi wa SGR na wa Stiegler's (Rufiji) Gorge, kulikuwepo matumaini makubwa kuwa, mapato yatakayokuwa yakipatikana kupitia Bomba la Mafuta ya Uganda (Hoima-Tanga Pipeline), ambayo ni Dola 12 kwa pipa (mapipa 200,000 kwa siku), sawa na Tsh. 5,500,000,000 kwa siku.
Hivyo kwa mwaka, Serikali ingekuwa inapata kodi ya Tsh. 2,000,000,000,000 (Trilioni 2). Fedha hizi zingerahisisha sana ulipaji wa madeni yoyote tuliyoingia na tunayoingia kujenga miundombinu muhimu hapa nchini.
Hata hivyo, kwa kuwa ujenzi umepelekwa tena mbele hadi mwakani 2019, inaweza ikaichukua Tanzania hadi mwaka 2021 kuanza kufaidika na mafuta ya Uganda.

Vilevile, Mradi mwingine mkubwa na super wa kuchakata gesi (LNG), mkoani Lindi, ulionekana kuwa mkombozi mkubwa sana kwa mapato serikalini, huku ukikadiriwa kuwa na uwezo wa kuiingizia Tanzania Tsh. 5,000,000,000,000 (Trilioni 5) kwa mwaka.

Baada ya Makubaliano na Kampuni za Gesi kukwama, Serikali yajipanga upya: Kiwanda cha LNG kuiletea Tanzania Tsh. 5,000,000,000,000 kwa mwaka. - JamiiForums

Ushauri:
Ni vyema Serikali iangalie upya makubaliano ya kukopeshwa fedha za ujenzi wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ili kuangalia namna ya kuusogeza mbele ujenzi wake ama kusogeza mbele Mpangala wa kulipa mkopo huo.

Serikali iahirishe kwa muda kuchukua mkopo kwa ajili ya ujenzi wa SGR, kipande cha kuanzia Dodoma - Tabara - Mwanza & Kigali ili kusubiri majaliwa ya mapato ya Bomba la Mafuta, mwaka 2021. Hii ni kwa sababu inawezekana ujenzi huo ukachukua muda mrefu zaidi ya mwaka 2021 unaotajwa. Ikumbukwe, awali uzalishaji ulipangwa kuanza mwaka 2019 lakini ikashindikana.

Serikali ihusishe Bunge, juu ya mkwamo wa LNG kwani ndiyo njia pekee ya uhakika kwa sasa ya kuongeza mapato maradufu serikalini. Na kwa kuwa ujenzi unachukua muda mrefu wa hadi miaka mitano, hivyo ni ngumu kuwa na uhakika na bill ya deni la China litajavyokuwa kufikia miaka ya 2023, kipindi ambacho tunaweza kuwa katika mazingira mazuri ya kuweka kuchakata gesi.

IMG_0276.JPG
 
Sisi ni wajinga wacheni wabebe kila kitu.

Watu mna katiba inayolinda watawala badala ya kulinda maliasili za nchi na mmeridhika sasa mnatarajia nini?

Katiba inaruhusu serikali kukopa inavyotaka,kuingia mikataba bila kulishirikisha Bunge,n.k. alafu mnalilia nini?!

Katiba na sheria zetu zimeacha mwanya wa kisheria miswaada inayohusu maliasili za Taifa kupelekwa na kujadiliwa Bungeni kwa hati ya dharura alafu mnatarajia nini?

Kinga ya Raisi haina mashariti yoyote hata kama atatumia madaraka vibaya kwa kuingia mikataba mibovu inayotafuna nchi eti hapaswi kushitakiwi!

Katiba hiyo hiyo imelifanya Bunge kukosa meno hivyo hata watawala wakiingia mikataba mibovu Bunge halina cha kuwafanya kwani taratibu za Bunge kuisimamia serikali ni kama za kiini macho tu.

Ni katiba hii inafanya vyama vya upinzani visiwe na sauti Bungeni kuweza kuihoji serikali kwani katiba hii inaruhusu Spika,Naibu Spika na wenyeviti wa Bunge watokane na chama cha siasa na kibaya zaidi Katiba na hata sheria zetu pamoja na kanuni za Bunge hazilazimisha uwepo wa Spika au Naibu Spika kutoka upinzani.

Watu wanapodai katiba mpya sio wajinga, bali wanajua umuhimu wake na tujue bila katiba mpya yenye kuweka mifumo ya kisheria inayolinda maliasilI zetu na si watawala,siku zote tutaendelea kuwa ombaomba na tutawaliwa tu na watu weupe kwa mashariti ya ushoga na mashariti mengineyo watakayopenda kutuwekea.
 
Sisi ni wajinga wacheni wabebe kila kitu.

Watu mna katiba inayolinda watawala badala ya maliasili za nchi na mmeridhika sasa mnatarajia nini?

Katiba inaruhusu serikali kukopa inavyotaka,kuingia mikataba bila kulishirikisha Bunge,n.k.

Katiba hiyo hiyo imelifanya Bunge kuwa kibogoyo hivyo hata watawala wakiingia mikataba mibovu Bunge halina cha kuwafanya.

Ni katiba hii inafanya vyama vya upinzani visiwe na sauti Bungeni kuweza kuihoji serikali kwani katiba hii inaruhusu Spika,Naibu Spika na wenyeviti wa Bunge watokane na chama cha siasa na kibaya zaidi Katiba na hata sheria zetu pamoja na kanuni za Bunge hazilazimisha uwepo wa Spika au Naibu Spika kutoka upinzani.
A cha uzwazwa ndugu yangu. Hiyo Katiba unayoongelea haina tu gear na Wabunge waliozaliwa mbinguni bali wametoka kwa Watanzania. So, kama Wabunge wengi waliozaliwa na Watanzania wataona ni sawa, hao wachache waliotaka kuibadilisha ni akina nani hao hadi tufuate misimamo yao na si ya wengi? Ndiyo demokrasia mnayotaka kutufundisha kwamba tuwe tunasikiliza maoni ya wengi na kufuata ya wachache?

Kama Wabunge ndiyo wanajiamulia na hawafuati maslahi ya Watanzania wengi, mbona wamekuwa wakirudishwa bungeni kila Uchaguzi unapofanyika na siyo Wapinzani?

Hivi, mbona hao hao Wabunge wa CCM wakiwa CCM huwa wanakuwa wabaya lakini wakienda Upinzani wanakuwa watakatifu?
 
Sisi ni wajinga wacheni wabebe kila kitu.

Watu mna katiba inayolinda watawala badala ya kulinda maliasili za nchi na mmeridhika sasa mnatarajia nini?

Katiba inaruhusu serikali kukopa inavyotaka,kuingia mikataba bila kulishirikisha Bunge,n.k.

Katiba na sheria zetu zimeacha mwanya wa kisheria miswaada inayohusu maliasili za Taifa kupelekwa na kujadiliwa Bungeni kwa hati ya dharura alafu mnatarajia nini?

Kinga ya Raisi haina mashariti yoyote hata kama atatumia madaraka vibaya kwa kuingia mikataba mibovu inayotafuna nchi eti hapaswi kushitakiwi.

Katiba hiyo hiyo imelifanya Bunge kuwa kibogoyo hivyo hata watawala wakiingia mikataba mibovu Bunge halina cha kuwafanya kwani taratibu za Bunge kuisimamia serikali ni kama za kiini macho tu.

Ni katiba hii inafanya vyama vya upinzani visiwe na sauti Bungeni kuweza kuihoji serikali kwani katiba hii inaruhusu Spika,Naibu Spika na wenyeviti wa Bunge watokane na chama cha siasa na kibaya zaidi Katiba na hata sheria zetu pamoja na kanuni za Bunge hazilazimisha uwepo wa Spika au Naibu Spika kutoka upinzani.
"Watu mna katiba inayolinda watawala badala ya kulinda maliasili za nchi na mmeridhika "

NIMELIELEWA SANA HILO NENO
 
Watanzania ni watu wa kuangalia na kusubiri matokeo, sisi huwa hatuhangaiki kujaribu kubadilisha mambo..labda tusubiri hivi vitega uchumi vikiisha tutaamka.
 
Bwana mikopo,kuliko kuongeza GDP.Ajae atapata tabu sana atafanya Kazi ya kulipa mikopo awamu zake zote
 
Mleta uzi acha upotoshaji kuhusu bomba la mafuta. Hilo bomba sio letu bali ni Uganda iweje utaje gharama za huo mradi kwamba ni wetu? Mradi w stiegler gorge bado ni siasa za kick na wala hakuna hela japo mkulu huuongopea umma kwamba pesa zipo. Hiyo reli ya SGR hata kipande cha Dar-Moro ni kuzungumkuti kukamilika kwake kwani hela zinasumbua. Hapo siongolei kabisa kipande cha Moro- makutopora. Huo mradi wa bagamoyoo wala sio magu kasitisha bali hao wachina walikuwa na makubaliano na JK na hawamsomi huyo Magu. Mradi wa LNG hautakaa utekelezwe kipindi chote cha magu, kwani hana uwezo wa kushawishi kupata ufadhili wa mradi wowote unaozidi $10b. Kwa mwenendo huu wa Magu kama atapata mkopo basi hauwezi kuzidi $3b. Huo ndio ukweli na hii ndio dunia inayohitaji diplomasia na yeye hana.
 
Chanzo ya katiba mbovu wa kulaumiwa ni Nyerere ndo alieleta shida hii,alitukuza utawala badala ya uchumi. Katiba chakavu ya MWALIMU si katiba ya kizazi cha sasa
Inamaana sisi ni wajinga kiasi gani?
Mpaka Leo tunatembelea mambo ya Nyerere hata kama yana kasoro?

Tukae kumlaumu MTU aliyekufa zaidi ya miaka 20 iliyopita wakati sisi uwezo Wa kurekebisha tunao

Kitu ni simple tu kubadili au kurekebisha katiba baaaaasi
 
Inamaana sisi ni wajinga kiasi gani?
Mpaka Leo tunatembelea mambo ya Nyerere hata kama yana kasoro?

Kitu ni simple tu kubadili au kurekebisha katiba baaaaasi
Tuombe wazungu watusaidie labda,katiba inalinda watawala, sio kulinda raslimali zetu.Hakuna mwananchi aliyewahi kaa na Nyerere kushirikishwa kwenye uundaji wake.Nchi yatakiwa iongozwe na watu sio MTU.Hii ya kuongozwa na MTU tutasubiri sana kila ajae anakuja na yake
 
Chanzo ya katiba mbovu wa kulaumiwa ni Nyerere ndo alieleta shida hii,alitukuza utawala badala ya uchumi. Katiba chakavu ya MWALIMU si katiba ya kizazi cha sasa
Huyo Nyerere ndiye aliyesumbuka kuleta uhuru lakini ndiye aliyeliunganisha Taifa kwa kiwango kikubwa. Amani ya Tanzania inatokana na vita ya Nyerere kwa ukabila. Isingekuwa Nation-building effort za Nyerere, Tanzania isingekuwa na tofauti na majirani zake ambao hupigana mara kwa mara kutokana na Viongozi wao wa awali kukazania uchumi kwa gharama ya amani, umoja na mshikamano.

Mwenge wa Uhuru unaweza kuwa unadharauliwa kwa sasa lakini believe me, ni moja ya alama muhimu kwa Tanzania kwa namna ulivyoiunganisha Nchi hii hasa miaka ya nyuma.
 
Mgambilwa ni Mntu said:
Hivi, mbona hao hao Wabunge wa CCM wakiwa CCM huwa wanakuwa wabaya lakini wakienda Upinzani wanakuwa watakatifu?

..ni kwasababu wabunge wa CCM huwa hawapingi wala kuhoji pendekezo lolote la serekali hata kama wanajua halina faida au lina madhara kwa taifa.

..wabunge wa upinzani peke yao ndiyo hutekeleza wajibu wao wa kuisimamia serekali.
 
A cha uzwazwa ndugu yangu. Hiyo Katiba unayoongelea haina tu gear na Wabunge waliozaliwa mbinguni bali wametoka kwa Watanzania. So, kama Wabunge wengi waliozaliwa na Watanzania wataona ni sawa, hao wachache waliotaka kuibadilisha ni akina nani hao hadi tufuate misimamo yao na si ya wengi? Ndiyo demokrasia mnayotaka kutufundisha kwamba tuwe tunasikiliza maoni ya wengi na kufuata ya wachache?

Kama Wabunge ndiyo wanajiamulia na hawafuati maslahi ya Watanzania wengi, mbona wamekuwa wakirudishwa bungeni kila Uchaguzi unapofanyika na siyo Wapinzani?

Hivi, mbona hao hao Wabunge wa CCM wakiwa CCM huwa wanakuwa wabaya lakini wakienda Upinzani wanakuwa watakatifu?

Wingi wa wabunge wa ccm hausababishwi na kura za wananchi bali amri ya rais kwakuwa ni amiri jeshi mkuu. Yeye ndio huamrisha tume ya uchaguzi kumtangaza mgombea wa ccm hata kama wananchi hawajaridhia, na wananchi wakionyesha kutokukubaliana na hilo huamuru vyombo vya dola kuumiza wananchi. Hivyo wingi wa wabunge wa ccm ni katiba mbovu inayompa madaraka rais ya maamuzi dhidi ya mamlaka zote za nchi.
 
Dhana ya kununua nguo za mtoto kabla hajazaliwa mimi huwa naipinga.

Ona sasa tunaambiwa faida tutakayo ipata baada ya kufanya hiki na kile.
Yaani tunazipigia na mahesabu kabisa hiyo pipe ya mafuta na Gas ya Lindi kwamba tukimaliza hela zinaingia kiulainiii
 
Sisi ni wajinga wacheni wabebe kila kitu.

Watu mna katiba inayolinda watawala badala ya kulinda maliasili za nchi na mmeridhika sasa mnatarajia nini?

Katiba inaruhusu serikali kukopa inavyotaka,kuingia mikataba bila kulishirikisha Bunge,n.k. alafu mnalilia nini?!

Katiba na sheria zetu zimeacha mwanya wa kisheria miswaada inayohusu maliasili za Taifa kupelekwa na kujadiliwa Bungeni kwa hati ya dharura alafu mnatarajia nini?

Kinga ya Raisi haina mashariti yoyote hata kama atatumia madaraka vibaya kwa kuingia mikataba mibovu inayotafuna nchi eti hapaswi kushitakiwi.

Katiba hiyo hiyo imelifanya Bunge kuwa kibogoyo hivyo hata watawala wakiingia mikataba mibovu Bunge halina cha kuwafanya kwani taratibu za Bunge kuisimamia serikali ni kama za kiini macho tu.

Ni katiba hii inafanya vyama vya upinzani visiwe na sauti Bungeni kuweza kuihoji serikali kwani katiba hii inaruhusu Spika,Naibu Spika na wenyeviti wa Bunge watokane na chama cha siasa na kibaya zaidi Katiba na hata sheria zetu pamoja na kanuni za Bunge hazilazimisha uwepo wa Spika au Naibu Spika kutoka upinzani.

Watu wanapodai katiba mpya sio wajinga na bila katiba mpya yenye kuweka mifumo ya kisheria inayolinda maliasilI zetu na si watawala,siku zote tutaendelea kuwa ombaomba na tutawaliw tu na watu weupe kwa mashariti ya ushoga na mashariti mengineyo.
Kwanini habari hii imeletwa na Mamluki Mgambilwa ni Mmuntu ?
 
Back
Top Bottom