Mikopo nafuu kutoka Bank of Africa (BOA)

Je waijua *BANK OF AFRICA (BOA)*
Hii ni Benki inayotoa mikopo rahisi ya hadi asilimia kumi nukta saba tu kwa mwaka.
Mfano ukikopa milioni 1.
Riba ya mwaka mzima itakuwa 107000.
Yaani kwa mwaka mmoja utarejesha riba na mkopo jumla milioni moja laki moja na elfu saba *(1107000)*
Makato kwa kila mwezi mmoja kwa kipindi cha miezi 12 yatakuwa ni 92,250.
Kwa miaka miwili makato yatakuwa
58,583.
N.k
Hii ni tofauti na Benki nyingine zinazotoa asilimia 18 au 17
Mfano kwa milioni moja katika Benki inayotoa riba ya 17 utakatwa 97,000 kwa mwezi.

WANAPATIKANA WAPI HAWA JAMAA?
Makao Makuu ni pale POSTA opposite na MAHAKAMA YA RUFAA
 
Naona wakopaji wamepungua sana kwenye benki zote, juzi kati nmb wamekuja ofisini kubembeleza watu wakope na rejesho miaka 7 au miezi 84 na wananunua madeni ya mikopo mingine. Tutakomaje
Watu wameanza kuelewa mikopo na adha zake. Hawadanganyiki kirahisi rahisi.
 
Mnaongelea mambo ya riba je vigezo vya kupata mkopo ni vipi? Kuna muda mtu unapata hitaji la kifedha na unakuwa tayari kuchukua mkopo wa riba yoyote lakini masharti yanakuwa magumu. Benki zote zinataka mshahara upite kwao na uwe umedumu kwa zaidi ya miezi sita na kuwe na mkataba baina ya benki na mwajiri wako sasa waajiri wa sasa hivi wengi wagumu kwenye hilo.
Benki gani haina masharti magumu na hao BOA vigezo vyao ni vipi?

Opera Min Joseverest etc
 
Wewe ndio umeleta hizi taarifa halafu umeisifia Bank kabisa inakuaje uulize wanapopatikana?
 
Mnaongelea mambo ya riba je vigezo vya kupata mkopo ni vipi? Kuna muda mtu unapata hitaji la kifedha na unakuwa tayari kuchukua mkopo wa riba yoyote lakini masharti yanakuwa magumu. Benki zote zinataka mshahara upite kwao na uwe umedumu kwa zaidi ya miezi sita na kuwe na mkataba baina ya benki na mwajiri wako sasa waajiri wa sasa hivi wengi wagumu kwenye hilo.
Benki gani haina masharti magumu na hao BOA vigezo vyao ni vipi?

Opera Min Joseverest etc
Kwani mikopo ni kwa wafanyakazi Tu? Kuna mikopo ya kibiashara pia
 
Back
Top Bottom