Papaa007
JF-Expert Member
- Sep 4, 2016
- 1,101
- 1,721
Hukujarb kuuza illegal issues ufidie deni
2018 nilikuwa na ndoto kubwa, niliona matumaini na mafanikio ya kiuchumi. Nilikopa nikawekeza, 2019 mambo yalibadirika biashara zikagoma kwa uzembe na nyingine ilikuwa lazima zife hasa za kilimo mvua ilisomba mazao. Madeni yakaingia yakakuwa , nikakwama siwezi yalipa yote, wadai hawaelewi ukiwaambia ukweli wanaona unawadharau, ukiomba muda zaidi hawaelewi wanataka niwape tumaini kuwa nitawalipa haraka naogopa kudanganya, nakaa kimya nikiendelea kuomba Mungu afungue milango nilipe madeni ya watu. Nashukuru Mungu familia inanilisha . Ni mtumishi mshahara mdogo nalipa madeni wote hata sadaka sibakiwi nayo. Nashukuru kazini ni karibu sihitaji nauli. Madeni mabaya wapendwa, ukiweza usikope kabisa , nimeharibu undugu, urafiki ,familia, naishi kwa Neema ya Mungu na kuomba nisipate stress. Mbinu zote za kibinadamu nimetumia ili nilipe madeni nimeshindwa, sasa hivi natumaini Mungu tu. Wapendwa msikope madeni in utumwa in kifungo kibaya.