Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu

mjasiria

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
4,156
1,849
Habari zenu wakuu,
Siku ya Ijumaa ya tarehe 2/9/2011 TCU kwa kushirikiana na HESLB walitoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwango cha mikopo ambacho watapatiwa. Ambacho sikuweza kukielewa ni jinsi mgawanyo wa mikopo ulivyofanyika kwa sababu kwanza badala ya kuonesha kwa asilimia wao waliweka kiwango cha fedha ambacho mwanafunzi husika atapatiwa. Sasa swali langu ni kuwa je hizi fedha zilizoandikwa ni kiasi ambacho mwanafunzi atapatiwa kwa muda wote wa kipindi cha masomo atakapokuwa chuoni?? au ni kwa mwaka wa kwanza peke yake??

Kwa mfano nina mdogo wangu ambaye amechaguliwa katika kozi ambayo ada yake ni TZS 1,400,000/= kwa mwaka na ameandikwa kuwa atapatiwa mkopo wa TZS 3,995,500/=. Sasa sijaelewa kama hii fedha ni jumla ya fedha yote atakayopatiwa kwa muda wa miaka mitatu ya kozi yake au vinginevyo. Vilevile je fedha hizi zinajumuisha malipo fedha ya kujikimu na malazi?

Wakuu hapo nimekwama na kwa bahati mbaya sana jamaa wa HESLB inaonekana wako bize sana kiasi kwamba inakuwa vigumu kwa wao kujibu maswali yetu sisi wananchi tuliowaajiri.

Nawasilisha hoja.

Hicho kiwango cha fedha alichopata ni kwa mwaka mmoja tu,mwaka wa kwanza.Atakapo maliza na kuendele na mwaka wa pili atapewa tena mkopo.katika hizo fedha HAPO KUNA ADA YA CHUO,FEDHA YA MWANAFUNZI YA KUJIKIMU,KUNA FEDHA YA MAFUNZO KWA VITENDO,KUNA FEDHA YA VITABU, PIA KUNA FEDHA YAKE YA STATIONARY(kwa uchache). Ili upate mchanganuo zaidi ulio sahihi waweza kwenda chuo alichopangiwa omba upewe INVOICE ya kijana wako kwa mwaka wa masomo 2011/12. Au subili kijana aripoti chuo na kupewa huo mchanganuo.Pia waweza kutembelea Website ya chuo husika na kutazama mchanganuo wa fedha kwa mwaka kutegemeana na kitivo husika.Kimsingi fedha atakayobakiwa nayo kijana wako ni kidogo baada ya kulipa michango yote inayotakiwa na chuo husika.

Mkuu shukrani sana kwa msaada wako ila ningependa kuuliza kama hizi data zimetoka HESLB au ni personal speculation. Samahani kama nitakukwaza ila ningependa kupata uhakika wa hili jambo.

Ubarikiwe mkuu.

I suggest u contact with HESLB for more information!

Huyo jamaa kakupa taarifa sahihi,leo niliangalia chanel 10 wakat wanahojia wa watu wa bod ya mikopo,wamesema hivyo hivyo, hyo ela ni kila kitu hapo.

Back
Top Bottom