Mikopo kwa wafanyakazi: Mabenki ya humu nchini yamekosa kabisa ubunifu wa kuvutia wakopaji

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,982
144,306
Kama wewe ni mfanyakazi wa serikali au wa sekta binafsi,bila shaka utaungana nami kuwa mabenki ya humu nchini yamekosa kabisa ubunifu wa kuvutia wakopaji. Tuna utitiri wa mabenki, lakini hakuna benki ambayo ukieenda, utaona kitu cha tofauti sana na benki nyingine kuanzia kwenye riba na mambo mengine yote yanayohusiana na utoaji wa mikopo kwa wafanyakazi.

Kabla ya CRDB kutangaza kushusha riba mpaka kufikia asilimia 13 siku ya jana, mabenki karibu yote kwenye riba yalikuwa na tofauti ya kati ya asilimia moja au mbili, tofauti ambayo haiwezi kuleta ushindani wa maana na kuifanya benki mojawapo kuvutia wakopaji wengi zaidi.

Najua kuna watu watakuja na hoja kuwa riba ya mabenki inategemea na riba wanayotozwa na BOT lakini tukumbuke mabenki haya kila mwaka yanatangaza kupata faida kubwa tu na sehemu ya faida hiyo inatokana na mikopo.Hii maana yake ni kuwa, hata wangeshusha riba zaidi, bado wangepata faida na huenda faida ingeongezeka badala ya kupungua kwasababu watafanya biashara zaidi(wakopaji wataogezeka).

Eneo lingine ambalo mabenki yangeweza kuvutia wakopaji, ni katika kuangalia namna ya kuwapunguzia mzigo wa madeni wakopaji wanaochukua mkopo juu ya mkopo mwingine(top-up). Hii ni kwasababu wafanyakazi wengi teyari wana mikopo na wakifanya top-up, wanachopata ni kidogo ila kutokana na majukumu na changamato walizonazo, wafanyakazi hulazimika kuchukua mkopo juu mkopo mwingine ili kujikimu kimaisha.

Hivyo, benki yenye watendaji wabunifu, ingeangalia namna ya kupunguza deni la mkopo wa awali ili kushawishi wakopaji kufanya top-up kwani katika mabenki mengi kinachopungua ni kidogo sana na hakuna tofauti ya maana katika punguzo hilo kati ya benki moja na benki nyingine. Benki ya Posta ndio angalau wameonyesha utofauti hata pale mtu unapotaka kufuta mkopo kabla ya muda kwani walau kunakuwa na punguzon la kuridhisha tofauti na mabenki mengine.

Udhaifu mwingine ni kwa baadhi ya mabenki kuweka shariti la kwamba ni lazima mshahara upite katika benki yao ndio wakupe mkopo. Hili ni moja ya shariti ambalo huwa linashangaza sana. Yaani kumlazimisha mfanyakazi abadili akaunti ya mshahara kisa tu anataka mkopo kutoka katika benkin yako? Huku tu si kuishiwa ubunifu, bali ni kuonyesha uwezo mdogo wa watendaji katika mabenki huska. Inawezekana kuna changamoto zinazopelekea mashariti ya aina hii ila ni ukweli kuwa, hakuna biashara isiyo na changamoto na huwezi kukabili changamoto ya kibiashara kwa kuweka utaratibu unaofukuza au kupunguza wateja.

Jambo lingine linaloonyesha ukosefu wa ubunifu ni karibu mabenki yote kutaka utitiri wa viambatanisho na ajabu zaidi ni pale ambapo hata mfanyakazi anahitaji kufanya top-up kutakiwa kuja na viambatanisho vyote kama ndio anachukua mkopo kwa mara ya kwanza wakati mfanyakazi anatoka katika taasisi ile ile na mwajiri wake bado ni yule yule.

Mfano,mtu anaamua kuchukua mkopo mwingine labda baada ya mwaka mmoja au miwili, ila ni shariti mkopaji aambatanishe tena mkataba wa ajira na barua ya kuthibitishwa kazini wakati mfanyakazi ni yule yule na mwajiri wake ni yule yule na taasisi yake ni ile ile.

Kasoro nyingine ni kumtaka mteja anaetaka kulipa mkopo wake wote(kabla ya muda wa mkataba) alazimike kulipa kiasi chote kinachotakiwa na hakuna option ya kumuwezesha mteja kulipa kidogo kigogo(kwa awamu) sambamba na kuendelea kukatwa kila mwezi ili metaja amalize deni mapema zaidi.

Kwa kifupi, kuna mapungufu mengi tu(kulingana na mtazamo wangu), mapungufu ambayo nin matokeo ya kukosekana kwa ubunifu wenye lengo la kuvutia wakopaji wengi, na hivyo hata riba ikiendelea kupungua(naamini na mabenki mengine yatashusha riba) bado hakuna benki itayokuja na kitu cha tofauti kuweza kuvutia wakopaji zaidi ya wote kushindana katika kushusha riba tu.

Kama ambavyo licha ya mabenki kuwa yanatangaza kupata faida kila mwaka, hakuna benki ilioona umuhimu wa kushusha riba za mikopo na kuvutia wakopaji wengi zaidi mpaka serikali ilipowataka kufanya hivyo, ndivyo ambavyo hakuna benki itayoonyesha nia ya kurahisisha taratibu za utoaji wa mikopo kama nilivyoeleza hapo juun labda mpaka waagizwe na BOT kutazama upya taratibu zao.

Inashangaza sana!
 
issue ya muhimu hapi ni riba....

Suala la riba linapaswa lisimamiwe kwa ukaribu na Serikali ikiwezekana iwe hata chini ya 5% kwa mikopo yote..
 
Benki zinafanya biashara na lengo lao ni kupata faida wakifanya uliyoandika watakuwa wanalenga kukunufaisha wewe sasa sidhani kama ndio lengo lao
 
Kumbuka wateja wengi ndio huongeza faida ya biashara yako kuliko unapokuwa na wateja wachache.
 
Hivi nyie watumishi mnaishije kwa kutegemea kipato kimoja tu?Mtakopa kopa hivi mpk lini,tafadhili amkeni nchi hii Ni tajiri Sana unaweza kua mtu tajiri Muda wowote ule ukiamua.Kinachotakiwa Ni kuchapa kazi kwa bidii kubwa,maono ya mbali na kuzalisha Mali.Poleni Sana watumishi.

Alisikika motivational speaker akiongea kwa sauti ya juu akiwa maeneno ya sokoni huku akiwa ameshika kipaza sauti wkt akitangaza kitabu chake kipya kiitwacho 'how to get rich'.
 
Kukopesha ni kazi, mipango na mbinu za mkopeshaji ndio vitakavyomvutia mteja.

Riba sio kitu pekee kinachomvutia mteja.
 
Kama wewe ni mfanyakazi wa serikali au wa sekta binafsi,bila shaka utaungana nami kuwa mabenki ya humu nchini yamekosa kabisa ubunifu wa kuvutia wakopaji. Tuna utitiri wa mabenki, lakini hakuna benki ambayo ukieenda, utaona kitu cha tofauti sana na benki nyingine kuanzia kwenye riba na mambo mengine yote yanayohusiana na utoaji wa mikopo kwa wafanyakazi.

Kabla ya CRDB kutangaza kushusha riba mpaka kufikia asilimia 13 siku ya jana, mabenki karibu yote kwenye riba yalikuwa na tofauti ya kati ya asilimia moja au mbili, tofauti ambayo haiwezi kuleta ushindani wa maana na kuifanya benki mojawapo kuvutia wakopaji wengi zaidi.

Najua kuna watu watakuja na hoja kuwa riba ya mabenki inategemea na riba wanayotozwa na BOT lakini tukumbuke mabenki haya kila mwaka yanatangaza kupata faida kubwa tu na sehemu ya faida hiyo inatokana na mikopo.Hii maana yake ni kuwa, hata wangeshusha riba zaidi, bado wangepata faida na huenda faida ingeongezeka badala ya kupungua kwasababu watafanya biashara zaidi(wakopaji wataogezeka).

Eneo lingine ambalo mabenki yangeweza kuvutia wakopaji, ni katika kuangalia namna ya kuwapunguzia mzigo wa madeni wakopaji wanaochukua mkopo juu ya mkopo mwingine(top-up). Hii ni kwasababu wafanyakazi wengi teyari wana mikopo na wakifanya top-up, wanachopata ni kidogo ila kutokana na majukumu na changamato walizonazo, wafanyakazi hulazimika kuchukua mkopo juu mkopo mwingine ili kujikimu kimaisha.

Hivyo, benki yenye watendaji wabunifu, ingeangalia namna ya kupunguza deni la mkopo wa awali ili kushawishi wakopaji kufanya top-up kwani katika mabenki mengi kinachopungua ni kidogo sana na hakuna tofauti ya maana katika punguzo hilo kati ya benki moja na benki nyingine. Benki ya Posta ndio angalau wameonyesha utofauti hata pale mtu unapotaka kufuta mkopo kabla ya muda kwani walau kunakuwa na punguzon la kuridhisha tofauti na mabenki mengine.

Udhaifu mwingine ni kwa baadhi ya mabenki kuweka shariti la kwamba ni lazima mshahara upite katika benki yao ndio wakupe mkopo. Hili ni moja ya shariti ambalo huwa linashangaza sana. Yaani kumlazimisha mfanyakazi abadili akaunti ya mshahara kisa tu anataka mkopo kutoka katika benkin yako? Huku tu si kuishiwa ubunifu, bali ni kuonyesha uwezo mdogo wa watendaji katika mabenki huska. Inawezekana kuna changamoto zinazopelekea mashariti ya aina hii ila ni ukweli kuwa, hakuna biashara isiyo na changamoto na huwezi kukabili changamoto ya kibiashara kwa kuweka utaratibu unaofukuza au kupunguza wateja.

Jambo lingine linaloonyesha ukosefu wa ubunifu ni karibu mabenki yote kutaka utitiri wa viambatanisho na ajabu zaidi ni pale ambapo hata mfanyakazi anahitaji kufanya top-up kutakiwa kuja na viambatanisho vyote kama ndio anachukua mkopo kwa mara ya kwanza wakati mfanyakazi anatoka katika taasisi ile ile na mwajiri wake bado ni yule yule.

Mfano,mtu anaamua kuchukua mkopo mwingine labda baada ya mwaka mmoja au miwili, ila ni shariti mkopaji aambatanishe tena mkataba wa ajira na barua ya kuthibitishwa kazini wakati mfanyakazi ni yule yule na mwajiri wake ni yule yule na taasisi yake ni ile ile.

Kasoro nyingine ni kumtaka mteja anaetaka kulipa mkopo wake wote(kabla ya muda wa mkataba) alazimike kulipa kiasi chote kinachotakiwa na hakuna option ya kumuwezesha mteja kulipa kidogo kigogo(kwa awamu) sambamba na kuendelea kukatwa kila mwezi ili metaja amalize deni mapema zaidi.

Kwa kifupi, kuna mapungufu mengi tu(kulingana na mtazamo wangu), mapungufu ambayo nin matokeo ya kukosekana kwa ubunifu wenye lengo la kuvutia wakopaji wengi, na hivyo hata riba ikiendelea kupungua(naamini na mabenki mengine yatashusha riba) bado hakuna benki itayokuja na kitu cha tofauti kuweza kuvutia wakopaji zaidi ya wote kushindana katika kushusha riba tu.

Kama ambavyo licha ya mabenki kuwa yanatangaza kupata faida kila mwaka, hakuna benki ilioona umuhimu wa kushusha riba za mikopo na kuvutia wakopaji wengi zaidi mpaka serikali ilipowataka kufanya hivyo, ndivyo ambavyo hakuna benki itayoonyesha nia ya kurahisisha taratibu za utoaji wa mikopo kama nilivyoeleza hapo juun labda mpaka waagizwe na BOT kutazama upya taratibu zao.

Inashangaza sana!
Hoja nzuri, ushauri mzuri.
 
Umesema kweli tupu! Watanzania wako hovyo Sana kibiashara! Hakuna ubunifu hata kdg!
 
Back
Top Bottom