Mikopo kwa makundi maalumu ya vijana na wanawake wenye ulemavu ya asilimia 10 yasitishwa

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
69,345
94,508
Waziri Mkuu amesema kuwa ameagiza Halmshauri zote zisitishe utoaji wa Mikopo ya Makusanyo ya kuanzia Mwezi April hadi mpango mpya utapofanyiwa kazi.

Ameyasema hayo Bungeni alipokuwa akihitimisha Taarifa na kujibu hoja.

-----
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezielekeza Halmashauri zote nchini kusitisha utoaji wa fedha za mikopo kwa makundi maalum ya vijana, wanawake na wenye ulemavu kuanzia Aprili hadi Juni, 2023 wakati Serikali inajipanga kuweka mfumo mpya wa utoaji wa mikopo hiyo.

Ametoa maagizo hayo leo (Alhamisi Aprili 13, 2023) wakati akihitimisha hoja zilizotolewa na Wabunge wakati wakijadili Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

“Katika mkutano huu wa Bunge kuliibuka hoja kuhusu kiasi kidogo cha fedha za mikopo zitokanazo na asilimia 10 ya makusanyo ya Halmashauri kinachotolewa kwa makundi maalum kutokidhi matakwa ya kuyainua makundi hayo kwa kufanya shughuli za uzalishaji au biashara”

Katika hoja hiyo ilielezwa kuwa kumekuwa na changamoto kwenye baadhi ya Halmashauri kutoa fedha hizo kwa watumishi wa Halmashauri au wakati mwingine vikundi hewa badala ya walengwa na kusababisha fedha za mikopo hiyo kutorejeshwa.

Machi 29, 2023 wakati akipokea taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022 Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza kuangaliwa upya kwa utaratibu wa utoaji wa mikopo ikiwemo kuangalia namna ya kutumia mabenki kupitishia mikopo hiyo.

Chanzo: star tv.
 
T DS whddjytsuww0juj9orzsj0f0o DDT
Waziri Mkuu amesema kuwa ameagiza Halmshauri zote zisitishe utoaji wa Mikopo ya Makusanyo ya kuanzia Mwezi April hadi mpango mpya utapofanyiwa kazi.

Ameyasema hayo Bungeni alipokuwa akihitimisha Taarifa na kujibu hoja
6
 
Wasitishe tu maan aiwafikii walengwa
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezielekeza Halmashauri zote nchini kusitisha utoaji wa fedha za mikopo kwa makundi maalum ya vijana, wanawake na wenye ulemavu kuanzia Aprili hadi Juni, 2023 wakati Serikali inajipanga kuweka mfumo mpya wa utoaji wa mikopo hiyo.

Ametoa maagizo hayo leo (Alhamisi Aprili 13, 2023) wakati akihitimisha hoja zilizotolewa na Wabunge wakati wakijadili Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

“Katika mkutano huu wa Bunge kuliibuka hoja kuhusu kiasi kidogo cha fedha za mikopo zitokanazo na asilimia 10 ya makusanyo ya Halmashauri kinachotolewa kwa makundi maalum kutokidhi matakwa ya kuyainua makundi hayo kwa kufanya shughuli za uzalishaji au biashara”

Katika hoja hiyo ilielezwa kuwa kumekuwa na changamoto kwenye baadhi ya Halmashauri kutoa fedha hizo kwa watumishi wa Halmashauri au wakati mwingine vikundi hewa badala ya walengwa na kusababisha fedha za mikopo hiyo kutorejeshwa.

Machi 29, 2023 wakati akipokea taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022 Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza kuangaliwa upya kwa utaratibu wa utoaji wa mikopo ikiwemo kuangalia namna ya kutumia mabenki kupitishia mikopo hiyo.

Source star tv.
 
Back
Top Bottom