Mikopo elimu ya Juu: Madaraja kuondolewa, Sayansi kupata mkopo asilimia 100 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikopo elimu ya Juu: Madaraja kuondolewa, Sayansi kupata mkopo asilimia 100

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Jan 29, 2009.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (HESLB), itafanya mabadiliko makubwa ya utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini kwa mwaka ujao wa fedha kama hatua mojawapo ya kupunguza matatizo yaliyokuwa yakiikumba bodi hiyo katika utendaji kazi wake.

  Uamuzi huo wa Bodi ulitangazwa jana jijini hapa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Nicholaus Mbwanji wakati alipozungumza na waandishi wa habari. “Nia yetu kama Bodi ni kufungua ukurasa mpya wa utendaji wetu na zaidi kuweka utaratibu wa utoaji mikopo na vigezo vyake na pia kuishauri serikali katika utoaji mikopo na urejeshaji wake,” alisema Profesa Mbwanji.

  Alisema chini ya mabadiliko hayo, kuanzia mwaka ujao wa fedha maombi yote ya mikopo yatakuwa yakijadiliwa na kupitishwa na kamati za elimu katika ngazi ya kijiji, kata ama tarafa na baadaye kupitishwa kwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya husika. Alisema lengo likiwa ni kuwabaini zaidi ni wanafunzi gani walio na uwezo na ambao hawana uwezo ili wakati wa utoaji wa mikopo iwe ni rahisi kwa Bodi kuyashughulikia maombi yao.

  “Lengo la mabadiliko haya ni kuzuia udanganyifu na kuwasilishwa kwa taarifa zisizo sahihi kwetu na maombi ambayo hayakupitishwa katika kamati hizo hayatapokelewa na Bodi,” alisisitiza na kuongeza kuwa katika mwaka ujao wa fedha, Bodi pia itaendelea kutumia vigezo sita katika kutambua uwezo wa kiuchumi kwa waombaji wa mikopo inayotolewa na bodi yake.

  Kwa mujibu wake, vigezo hivyo ni historia ya elimu ya mwombaji ili kumbaini mwombaji anayeghushi nyaraka za kujiunga na chuo; kiwango cha elimu ya wazazi wake; shughuli zake za kiuchumi; mali za mwombaji na za wazazi wake; hifadhi yake ya maisha na hali yake ya kijamii kwa ujumla.

  Kuhusu sifa kwa wale wanaopatiwa mikopo, alisema sifa za ufaulu kwa viwango vya daraja la kwanza na la pili havitatumika tena kuanzia mwaka ujao wa fedha na badala yake, Bodi itazingatia udahili unaofanywa na vyuo vya elimu ya juu nchini. “Nawaomba Watanzania watambue kuwa katika kuzingatia mpango huu, wanafunzi watakaopata udahili katika kozi za sayansi kwa mwaka 2009/10 watapewa mikopo yao kwa asilimia mia, hii imetokana na kubainika kuwa wanafunzi wa sayansi wanaonufaika na mikopo hiyo imekuwa ni pungufu ya asilimia 35 tu, hali hii sio nzuri kwa taifa letu,” aliongeza.

  Chanzo: Habari Leo

  Maswali ya kujiuliza:

  Kwa kuwa haya ndio mambo ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na wanavyuo, wazazi, DARUSO, TSNP, TAHLISO, CHADEMA nk; je ni kwamba serikali imesikiliza kilio cha umma au ni kwa sababu uchaguzi wa 2010 umekaribia?

  Kwa kuwa utaratibu huu unakuja baadaye, si ishara ya kwamba wanafunzi wa sasa walikuwa na hoja, kwa nini mpango huu usihusu pia wanafunzi ambao mwaka huu wameshindwa kuendelea na masomo yao kutokana na masharti yale ya mwanzo?

  Palikuwa na haya gani kutumia nguvu ya dola kama madai haya ya wanafunzi yalikuwa ni ya kweli?

  Je, ilikuwa sahihi kufanya udahili upya kwa wanafunzi? Kwanini udahili mpya haukufuata utaratibu huu?

  Zaidi ya wanafunzi 2000 walishindwa kujaza fomu kwa hiyo serikali imetangaza kuwa wamejifukuzisha fomu. Je, fomu zilikuwa zinapatikana vijijini waliporudishwa baada ya chuo kufungwa? Je, masharti na muda wa kupata fomu hizo viliruhusu wote kupata? Kwanini bodi isitangaze utaratibu wa kuwawezesha hao pia kusoma?

  Asha
   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....eti wataanzia ngazi za vijiji kuangalia kama mwombaji anastahili mkopo? naona wanatengeneza ufisadi mwingine tuu hapo....all in all hii ni habari nzuri kwa wapenda maendeleo.
   
 3. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  The entire proposal is good but the general operandi may be more tricky. It will be too bureaucratic having three different bodies taking into account the actual time from the time form six results are out to the time of joining universities. On the otherhand it brings another country modelling challenge, 'the country and its people need to be modelled' we should have a national database for all households. This needs to be fully computerised and should be integrated with all hospitals, courts and say pollice stations across the country for updating informations.

  Anyway what I want to say here is that, the approach they are proposing is not an optimal solution for is not efficient one.
   
 4. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,261
  Trophy Points: 280
  2010 is around the corner jamaa wameshaanza kampeni
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Thank you so much Asha. I think this is a mind-shift and a great turning point. The problem is that the timing puts them in big shit. They cannot get away with feeling that this is a vote trap for 2010 elections. The same promises were made in 2005. Unless they these new proposals are made in legally binding standing orders, they will remain to be political statements or ambitions. The board has so far failed to win confidence of its stakeholders and it requires to be revamped.
   
 6. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Dalili za ushindi zinaonekana mwisho itakuwa ni kwa wanafunzi wote.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yuko wapi ze marcopolo?????, good move!!!!!!!! ila sasa ni nani utamwamini kufanya assesment ya nani anastahili mkopo kwenye chi corrupt kama hii?

  Nahisi kama tutarudi kule kule sema kwa staili "nyengine"
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  This article says it all!!!

  EYE SPY: The clowning and lies are on!


  ADAM LUSEKELO
  THIS DAY
  DAR SALAAM

  ACCORDING to the government, more than 1.27 million jobs have been created during the last three years. But then you would expect them to say that, wouldn�t you?

  You don’t need to get A-pluses in the political show in Bongo to know that the ruling CCM has unofficially kicked off the election campaigns for the 2010 general elections. They are now busy tarting themselves up to look pretty before the people of the United Republic of Tanzania.

  But are the people buying that? I bet they donèt. If you hear some government ruler start the process of going to a salon to tart himself up on how beautiful the government is, reach for your remote control and watch soccer. Watch Brazilian soccer star Kaka think with his feet. Or phone your chick for a chat.

  According to the government, they have created 27 per cent above the one million five-year target set by the Fourth Phase government, which came into office after the 2005 general elections.

  If you believe that then you will believe me too. My real name is not Adam Lusekelo, but Julius Caesar, Emperor of Rome!

  There are more flowery truths coming from the government. The economy of Tanzania is growing very fast. In fact last year it recorded a 25 per cent growth. All that amid crippling water shortages in the real capital Dar es Salaam and not that designated capital joke called Dodoma.

  By the way only the other day, the Prez, Jack Mrisho, was photographed by the ubiquitous State House press corps inspecting sketches of the planned Julius Nyerere convention centre in Dodoma? No bozo in Dar! The planned shift to Dodoma is going to take only a few hundred years. As I told you my real name is Julius Caesar.

  So while the economy has been booming, there have been intermittent power-cuts. No fear, I hear the government has imported millions of night-vision goggles for Tanzania’s students to wear while reading and doing their homework at night.

  Talk of students, Tanzania is also leading in persuading students to go to classes in universities or any pretension calling themselves universities or institutions of higher learning!

  By the way, after lengthy meditation and reflection, the government has decided to stop importing those eyesores called ’shangingis’, those embarrassing four-wheel cars for the status-conscious ruling class.

  Instead the Prez, says he will buy tractors from the money saved. After saying that agriculture is the backbone of the economy of Tanzania for the last 45 years, the government has now come to realize that it has to do something about that backbone of the economy.
  These are times for flowery speeches which will go on until after the 2010 general elections. You ve to give it to those politicians. They will yap a lot without actually saying anything. Without batting a lid. What a tough way to make a living!

  mbwene2@yahoo.com
   
 9. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Mkuu, umeuliza maswali yako vizuri. Na mimi najiuliza pia: kwa vile wanafunzi watakaopata udahili katika kozi za sayansi kwa mwaka 2009/10 watapewa mikopo yao kwa asilimia mia, si hii itafanya masomo mengine yakose wanafunzi na karibu wengi wajidahili kwenye masomo ya sayansi kwa kutaka hiyo asiliamia mia moja? Je, mpango huu hautaleta matatizo mengine?

  Kukopeshwa asilimia mia moja kugefanywa kwa kufuata hali halisi ya wazazi/wanafunzi. Recommendations zitoke huko vijijini na zisibitishwe pia na viongozi wa dini/au watu makini katika ngazi ya kijiji na kata.

  Shule za seminari zinafuata mfumo kama huu na walimu wanajua wanafunzi wanaotoka familia maskini na wale wanaotoka familia zenye uwezo. Hata kukiwa na haja ya kumsaidia mwanafunzi huwa wanafuata style hii.
   
 10. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uhuhni wa wanafunzi umewasaidia! sasa angalau wanaanza kusikilizwa.Tena inaonesha madai yao yalikuwa sahihi.Hili linadhihirisha serikali ilkurupuka kuwafukuza na kuwaita wahuni.At last wameshinda sasa na Maghembe anaweza kutuambia hapa muhuni nani!
   
 11. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  SEMA UHUNI WENU KWANI NA WE SI MWANAFUNZI WA MLIMANI AU?? KIBENGE MCHAGA FULANI HIVI........ see u when u see me!
   
 12. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa Sayansi kupata 100% ya mkopo naunga mkono, upande wa sayansi madaraja yameondoka. Sasa tunaanza kupiga KELELE kuondoa daraja la wachukuao Sayansi na wale wa michepuo ya Biashara, kwanini sayansi wapate 100% na wengine wasipate. Wakati nchi ni ileile na kipato cha mwananchi kinajulikana?.
   
 13. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Tunahitaji mapinduzi ya Sayansi na Teknologia kwanza! Hayo ya biashara na social sciences baadae!
   
 14. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Hawa viongozi wanajaribu kukwepa hoja. Suala si sayansi, ishu ni umasikini wa watoto wa wakulima. Kwa hio hata mtoto wa waziri apate 100% kisa anasoma sayansi, halafu mtoto wa mkulima anaesoma arts 60% hii haingii akilini. Serikali inachofanya ni ubaguzi mwingine tena mbaya sana. Huku ni kuwagawa wanafunzi ili iwe rahisi kuzima harakati za kudai haki. Basi masomo ya arts yafutwe kama ishu ndio hii. Kila kozi ina umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa. Huu ni uhuni mwingine umeletwa.
   
 15. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya vijana wahini PCB na PCM hizo mchukue fweza kiulaini.Sasa wale wenzangu ambao Biology,Chemistry etc ni baba mkwe basi mtaula wa chuya!!!
   
 16. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  hali ya masomo ya science hapa bongo ni mbaya sana. inaonekana wazazi wanaolipia watoto wao wana prefer kuwapeleka sheria, commerce, education nk. pia wanafunzi waliofaulu vizuri PCM, PCB nk wanapendelea kwenda huko na sababu ni moja tu uhakika wa ajira. ukiangalia mhimbili/sua/coet/aru hawapati wanafunzi wazuri
   
 17. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sasa watajidahili wapi?tangia form 2 au unatoka tu na HGK yako unakwenda kujidahili civil engineering?Tatizo hapo hata ukijidahili sayansi ili upate hiyo 100% je una uwezo wa kuyamudu hayo masomo?utafaulu?manake suala siyo kujidahili tu ili upate mkopo,suala ni kugonga hizo alama zao.
  anyway wacha watie chachu kwa vijana manake nchi yetu ina uhaba mkubwa wa wanasayansi.
   
Loading...