Mikopo elimu ya juu liwe mjadala wa kitaifa

Smkwawa

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
651
964
Watanzania ni wabinafsi sana... Hili suala la wanafunzi kukosa mikopo ya elimu ya juu ilipaswa kuwa mjadala wa kitaifa..., bahati mbaya watanzania wengi wanapenda 'umbea na porojo' sasa wanajadili siku ya tatu mfululizo issue ya Dr, Louis Shika na nyumba za Lugumi kwenye mnada..., tubadilike kidogo leo.., tujadili masuala "issues"..,

September 14, 2015 katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora.. Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM katika kampeni za uchaguzi mkuu, alisema kwenye serikali yake hawezi kukubali na kuruhusu kuona wanafunzi wanakosa mikopo ya elimu ya Juu.., akasisitiza kwamba HESLB watashughulikiwa ipasavyo ikitokea hivyo..

Mungu wetu sio Bashite aisee.., sio Yohana ambae wengine tunamuita John... NEC wakamtangaza mgombea urais kwa tiketi ya CCM kama mshindi wa uchaguzi ule.., (nakumbuka; washirika, ACT-wazalendo walisalimisha ilani yao ya uchaguzi kwa mgombea yule wa CCM kuonesha kwamba ni wadau wao).., Sasa tuachane na hilo.., tuseme kuhusu hili la "mikopo ya elimu ya juu"

Zimeidhinishwa tsh 147bn pekee kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo (2017/2018), huku idadi ya wanafunzi walioomba mikopo ikiwa ni wanafunzi 63,737 ...., Na kwa maelezo ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HELSB) wanafunzi wenye uhakika wa kupata mkopo ni 30,000

Hili ni zaidi ya balaa kubwa kwa taifa; Wanafunzi 63,737 wamedahiliwa mwaka wa masomo 2017/18, miongoni kati ya watakaopewa mikopo. ni wanafunzi 30,000 pekee. Yaani kwa hesabu ndogo tu tunafanya hivi; 63,737—30,000 = 33,737 (hivyo wanafunzi 33,737 watakosa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018)..., hii tumefanya hesabu ya darasa la 3c..,

Kuweka kumbukumbu sahihi; mwaka wa masomo 2016/2017 (serikali hii ya sasa ikiwa madarakani) wanafunzi waliokuwa na sifa ya kupata mikopo ni takribani 48,000, na waliopewa ni 25,000+ huku zaidi ya wanafunzi 22,000+ wakikosa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka huo wa masomo...

Sasa najaribu kutafuta namna ipi hawa watu wanasema hii serikali ya sasa inafanya vyema kwenye suala la elimu.. Ikiwa serikali ya awamu ya tano (pamoja na madudu yote ya wanafunzi hewa, wafanyakazi hewa, mishahara hewa) bado wanamiliki takwimu nzuri kuliko hawa jamaa waliopo madarakani kwa sasa;

Twende kwa takwimu; katika suala la mikopo..., Mwaka wa masomo wa 2014/15, bajeti ilikuwa karibu tsh 341bn na wanafunzi waliopata mikopo ni zaidi 99,000+...., Mwaka wa masomo wa 2015/16 bajeti ya mikopo kwa wanafunzi ilikaribia 450bn+ na takribani wanafunzi 122,000+ walipata mikopo... Sasa linganisha na miaka miwili hii ya serikali ya awamu ya tano.. Wapi kuna afadhali au ahueni!?? Ingawa serikali zote za CCM ni taabu tupu..

Watanzania ambao wanalipa madeni yao ya mikopo kwa bodi ya mikopo wanalipa 100% ya madeni yao.., kila mwezi wanakatwa kwenye mishahara yao..., ongeza na pesa za wananchi (kodi) ambazo zinatoka serikali kuu kwenda HESLB.., sasa nashindwa kuelewa; matumizi ya pesa hizi yanakwenda wapi ikiwa wanafunzi wa elimu ya juu wanakosa mikopo ya elimu ya juu!??

Unatumia vigezo gani kumnyima mkopo mwanafunzi ambae wakati anasoma baba yake alikuwa diwani!!? Kwamba kwa sababu ya "udiwani" wa baba yake mwanafunzi akose mkopo wa elimu ya juu? Kuna wengine wamefaulu vyema (division one and two) wananyimwa mkopo kwa sababu walisoma shule binafsi (private schools)..., vipi kama walikuwa wanafadhiliwa katika elimu zao huko!?

USHAURI WANGU KWA WAZAZI; Mimi nilifikiri sasa; wazazi waache kupenda vitu vya ovyo-ovyo.., wakubali kulipa Ada ya elimu ya Sekondari (tsh 20,000/= kwa mwaka, yaani tsh 10,000/= kwa miezi sita) lakini elimu ya juu watoto wao wapate mikopo bila kukosa.., wazazi wasipendezwe na hii 'dezo' ya elfu 20 na wakaumizwa na balaa elimu ya juu..., wazazi wengi wamekuwa 'mazwazwa' sana katika hili.. Wafikirie nje ya box, hawajachelewa..

Wanafunzi 33,737 wanakosa mikopo na watanzania wametulia kimya tu.. Wametulia kwa sababu katika hao 33,737 labda wengi sio wanaotoka katika familia zao.., Watanzania tumekubaliana kuwa wabinafsi kweli-kweli.. Kwa sababu tatizo halikugusi.. Basi unatulia kimya...

Wanafunzi waliopata mikopo ya elimu ya juu (30,000) kati ya wale 63,737 waliomba mikopo.., walipaswa leo kuunganisha nguvu zao na wale 33,737 waliokosa mikopo ya elimu ya juu ambayo ni haki yao ili kudai na kushinikiza wenzao wapate mikopo ya elimu ya juu.. Bahati mbaya waswahili wana ubinafsi ndani yao.. Kwa sababu kapata mkopo hawezi kutafuta haki za mwenzake nae apate mkopo...
_____________________________

Martin Maranja Masese (MMM)
 
Na izingatiwe kwamba hatuwezi kuwana Tanzania ya viwanda kama hatuna raslimali watu,
0+0= 0
 
Mjadala huu ungekuwa muhimu,lakini serikali imeshaziba masikio haitasika chochote, na huu mjadala ungehamasishwa kwenye majukwaa mbalimbali lakini wapi watanzania tunasubiri matukio yasiyo na maana,.
 
Back
Top Bottom