Mikopo elimu ya juu kwa watoto wa walalahoi,haijakaa sawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikopo elimu ya juu kwa watoto wa walalahoi,haijakaa sawa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MUNYAMAKWA, Jul 13, 2012.

 1. M

  MUNYAMAKWA Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali imejitahidi kujenga shule za sekondari hapa nchini karibu kila kata.Lakini kuna changamoto nyingi zimejitokeza ikiwemo upungufu wa waalimu na vitendea kazi(vitabu, maabara n.k).Hali ambayo imechangia wanafunzi wengi (watoto wa wakulima)wachukue michepuo ya sanaa.Hata wale wachache (watoto wa wakulima)wanaofaulu na kuendelea hadi kidato cha tano na sita na michepuo hii ya sanaa,wanakuwa kwenye giza totoro wanapofaulu na kutaka kujiunga na vyuo vikuu hasa kusomea shahada ya kwanza ya Sheria.Hapo ndipo kidudu mtu 'mikopo kwa elimu ya juu' anapowazingua.Sijui tunataka wanasheria wawe watoto wa wenye uwezo tu ,maana wazazi wao wanauwezo wa kugharamia malipo ya elimu ya juu katika Shahada ya kwanza ya Sheria,au tunaogopa nini kwa hawa watoto wa wakulima mpaka tuwawekee vikwazo namna hii?
   
 2. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Sina uhakika kama nimekuelewa.
   
Loading...