Mikononi mwa polisi: what else can you live by if you die by the gun?

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
878
320
Jana kwa mara nyingine tena kumetokea vurugu kati ya raia na polisi ambayo yalisababisha mtu mmoja kujeruhiwa na risasi. Hapa nitatoa maoni yangu kwa kuangalia suala moja ambalo ndilo naliweka jukwaani tulijadili.

Natambua kuna maoni tofauti juu ya fujo kama hizi ambapo watu huchagua upande kutokana na sababu mbalimbali na wengine GTs huangalia mambo haya kwa mapana. Ni rahisi mtu kuwa na mtizamo Fulani kama fujo zimetokea kutokana na harakati za kisiasa au za kidini lakini wengi wetu ni mashihidi juu ya uonevu wa majeshi yetu (karibu yote) dhidi ya raia nje ya muktadha huo wa dini na siasa.

Kuna msemo maarufu usemao ‘if you live by the gun you die by the gun’ ambao unaendana na msemo wa Kiswahili ‘ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga’. Tuangalie upande wa pili wa huu msemo, inakuaje kama ukifa kwa bunduki? (what if you die by the gun?). Raia wasio na silaha wanauliwa kwa silaha hii inatujengea jamii ya aina gani?

Miaka kadhaa nyuma watu walikuwa wakitawanywa na mabomu ya machozi na baadae wakaja na mbinu ya kutembea na maji, ikafuata ya kumwagiwa maji ya kuwasha wengine wakawa wanatembea na oil chafu kukabiliana na hilo. Swai la kujiuliza ni wananchi watatembea na nini kujikinga na risasi, ‘bullet proof', au nao watatembea na silaha?

Polisi wameonekana mara nyingi kukosa busara kwa kushindwa kuhimili vurugu na kutumia silaha za moto. Njia hii ni suluhu ya wakati wa tukio lakini inaleta tatizo kubwa zaidi mbeleni kwa kujenga jamii yenye chuki na isiyo na utii wa sheria wa hiari. Polisi kazi yao si kushindana na raia bali kuwalinda, hata mtu anayetaka kujiua haumsaidii kwa kumpa njia rahisi zaidi ya kujiua bali unatafuta njia ya kumuepusha na kifo, sasa iweje polisi waone njia rahisi ya kulinda raia ni kwa kuua raia?

Hebu tuangalie katika vituo vya daladala ambavyo kuna wapiga debe na wengi wao wakiwa ‘mateja’, japo wanaweza kuonekana tofauti (wa ovyo) lakini wana utaratibu wao wa kazi, nafikiri tumesikia hili neno ‘kitengo’. Kitengo kina uwezo wa kuwaongoza ‘administrate’ mateja lakini watu ambao ni wasomi kama polisi wanashindwa kuongoza watu wenye akili timamu.

Jamii yoyote ina kiongozi, awe wa kisiasa, kidini, kiumri na wengineo. Mtu huyu lazima anakuwa na ushawishi katika jamii yake na watu siku zote wanamsikiliza hata pale wanapotofautiana nae katika hoja. Mfano ni vurugu zilizotokea Mbeya mjini ambapo mbunge wao aliweza kuwatuliza watu wake na amani ikarejea.

Nachojiuliza ni kwanini polisi hushindwa kuwatumia watu hawa pale ambapo ‘intelijensia’ yao inaonesha kuna tatizo sugu na badala yake wanatumia nguvu zisizo na ulazima kisha maafa yakitokea ndio wanawakumbuka watu hawa? Mambo haya yanaleta maswali mengi sana juu ya utendaji wa jeshi la polisi na viongozi wenye dhamana(wizara, kamati ya bunge, w/Mkuu na Rais).
Mtetezi wa raia kwa sasa ni nani? Kwanini tunajenga mazingira ya kuwafanya watu wajitete wenyewe, tunajua watatumia njia gani kujitetea?

Kwenye kemia wanasema ili moto uwake unahitaji hewa(O2), mgandamizo(pressure) na joto lakuwezesha kitu kiwake(autoignition temperature/kindling point) na ikiwa ‘presha’ ni kubwa au hewa ipo kwa wingi basi joto la kusababisha moto huitajika kwa kiasi kidogo tu.

Tusidharau mambo haya kwa kusema watanzania ni waogo au ni mahiri kuzungumza kwenye ‘keyboard’, tuangalie kizazi kijacho kinakua kikiwa kinashuhudia nini na ni mambo gani yanasikika zaidi kwenye masikio yao. Uoga wetu(utulivu) umejengwa na kile tulichopitia katika makuzi yetu, sifa tulizoimba kuhusu nchi yetu na hasa misingi iliyowekwa na viongozi wa kipindi hicho.

Hatuhitaji kuwa kama Somalia au Tunisia na Misri, tunahitaji watu wenye busara na uzalendo wa kweli washikilie nafasi za uwakilishi (uongozi) wakielewa kuwa mamlaka kuu zaidi ni uma na si kofia zao. Na kwa kumalizia nitakopa maneno haya toka kwa Edmund Burke

“When good men do nothing, evil triumphs. Evil, sin and sinful men must be opposed. God commands those who are good, not just to avoid evil but actively oppose it.”…

“For evil to prosper all it needs is for good people to do nothing”
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,563
7,141
Police wanaua raia bila kuchukuliwa hatua kali za kishetia ikiwemo kunyongwa au kifungo cha maisha jela,kwa sababu moja tu.Waziri wa mambo ya ndani hawajibiki ktk nafasi yake ipasavyo.Tulishuhudia kwa wafanyaboashara wa Mahenge na dereva tax waliuwawa kwa makusudi na police/tumeshuhudia Nyamongo/Noth Mara/Arusha ktk maandamano ya Chadema/tumeshuhidia kwa Dkt Ulimboka alivyoponea chupuchupu/tumeshuhudiwa kwa ndugu yetu Daudi Mwangosi alivyouwawa na police kinyama.Hakuna kiongozi yeyote wa Serikali au wa wizara husika akiwajibika kutokana na hayo yoote,unafikiri wananchi watarajie nini kama sio mauaji ya kinyama na ya kutisha toka kwa jeshi la police dhidi ya raia?Inawezekana kabisa police hawa wanapewa kiburi na viongozi wa kisiasa linaoulinda utawala huu kwa nguvu yeyote ile.

Waarabu wanasema'haliwali'tukipata chance na sisi raia tutadill na hawa police mtaani tunapoishi nao kila siku,tumechoka kuonewa/kuuwawa kinyama bila ya kutetewa na yeyote ktk Serikali hii.
 

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
878
320
...Hakuna kiongozi yeyote wa Serikali au wa wizara husika akiwajibika kutokana na hayo yoote,unafikiri wananchi watarajie nini kama sio mauaji ya kinyama na ya kutisha toka kwa jeshi la police dhidi ya raia?Inawezekana kabisa police hawa wanapewa kiburi na viongozi wa kisiasa linaoulinda utawala huu kwa nguvu yeyote ile.

Bila uwajibikaji hali itakuwa tete huko mbeleni
 

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
878
320
Yakifanyika haya labda tofauti itaonekana


Alisema kuwa kutokana na ukimya wa rais, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwachukulia hatua Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP Mwema, makamanda wa polisi wa mikoa ya Iringa na Morogoro, CHADEMA watakutana kabla ya Krismasi na kutoa msimamo wa nini kifanyike kutetea haki ya wananchi. Dk. Slaa alisema madhumuni ya CHADEMA ni kukuza, kulinda na kutetea haki za binadamu, hivyo wanapaswa kuhakikisha wanafuatilia ukandamizaji wa watu katika misingi ya rangi jinsia, ukanda, rika na itikadi, jambo alilodai limewashinda CCM.


kutoka hapa
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,801
24,508
Its a shame kwa kweli. Badala ya kukimbilia polisi, tunawakimbia polisi. My old friends always ananiambia 'polisi, hata akiwa ndugu yako, usimfanye rafiki yako. Lazma atakugeuka siku moja'
 

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
878
320
Its a shame kwa kweli. Badala ya kukimbilia polisi, tunawakimbia polisi. My old friends always ananiambia 'polisi, hata akiwa ndugu yako, usimfanye rafiki yako. Lazma atakugeuka siku moja'

Huo ndio ukweli na matendo yao yanazidi kuaminisha uma juu ya hiyo nadharia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom