'Mikono Yako Imejaa damu' - Aambiwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza TONY BLAIR | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Mikono Yako Imejaa damu' - Aambiwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza TONY BLAIR

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Oct 11, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,339
  Likes Received: 5,649
  Trophy Points: 280
  'Mikono Yako Imejaa damu' - Aambiwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza
  [​IMG]
  Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair Sunday, October 11, 2009 2:29 AM
  Mzee mmoja wa nchini Uingereza ambaye mtoto wake wa kiume alifariki katika vita vya Iraq mwaka 2003 alikataa kupeana mikono na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair na kumwambia kuwa mikono yake imejaa damu kutokana na vifo alivyosababisha katika vita hivyo.Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair ambaye alishirikiana na rais wa zamani wa Marekani, George Bush kutuma majeshi nchini Iraq kupambana na aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein aliaibika juzi baada mzazi ambaye mtoto wake alifariki kwenye vita hivyo alipokataa kumpa mkono wake na kumwambia kuwa mikono yake imejaa damu.

  Tukio hilo lililotokea wakati wa hafla ya kuwakumbuka wanajeshi waliofariki katika vita vya nchini Iraq.

  "Siwezi kupeana mikono na wewe, mikono yako imejaa damu", alisema Peter Brierley, ambaye mtoto wake wa kiume koplo Shaun Brierley, 28, aliuliwa mwezi machi mwaka 2003 nchini Iraq.

  "Najua kwamba wanajeshi wanapoenda vitani wanaweza kufariki, lakini inabidi waende vitani kwasababu za msingi na wapewe zana kamilifu za kivita", aliendelea kusema Brierley.

  Bwana Brierley aliongeza "Naamini Tony Blair ni mhalifu wa kivita, siwezi kukaa naye chumba kimoja na nimeshangazwa ameruhusiwa kuja kwenye hafla hii".

  "Naamini ana damu ya mwanangu na wanaume wote pamoja na wanawake waliofariki nchini Iraq chini ya mikono yake".

  "Hisia hizi hunijia kila siku na hasa kila ninapoona jeneza la mwanajeshi wa Uingereza likishushwa kwenye ndege, hunikumbusha kilichomtokea mwanangu", aliendelea kusema Brierley.

  Tukio hilo lilitokea kwenye hafla hiyo muda mfupi baada ya Blair kuamriwa akae chini na asikilize wakati askofu mkuu wa mji wa Canterbury alipokuwa akitoa hotuba yake kuwaponda wanasiasa kwa kushindwa kufikiria thamani ya maisha ya binadamu kwenye vita vya Iraq.

  Tony Blair alikuwa chanzo cha mjadala mkubwa nchini Uingereza mwaka 2003 kwa kumpa ushirikiano wa kivita George Bush na huku akituhumiwa kuwapotosha waingereza juu ya kuwepo kwa silaha za maangamizi nchini Iraq.Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair ambaye alishirikiana na rais wa zamani wa Marekani, George Bush kutuma majeshi nchini Iraq kupambana na aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein aliaibika juzi baada mzazi ambaye mtoto wake alifariki kwenye vita hivyo alipokataa kumpa mkono wake na kumwambia kuwa mikono yake imejaa damu.

  Tukio hilo lililotokea wakati wa hafla ya kuwakumbuka wanajeshi waliofariki katika vita vya nchini Iraq.

  "Siwezi kupeana mikono na wewe, mikono yako imejaa damu", alisema Peter Brierley, ambaye mtoto wake wa kiume koplo Shaun Brierley, 28, aliuliwa mwezi machi mwaka 2003 nchini Iraq.

  "Najua kwamba wanajeshi wanapoenda vitani wanaweza kufariki, lakini inabidi waende vitani kwasababu za msingi na wapewe zana kamilifu za kivita", aliendelea kusema Brierley.

  Bwana Brierley aliongeza "Naamini Tony Blair ni mhalifu wa kivita, siwezi kukaa naye chumba kimoja na nimeshangazwa ameruhusiwa kuja kwenye hafla hii".

  "Naamini ana damu ya mwanangu na wanaume wote pamoja na wanawake waliofariki nchini Iraq chini ya mikono yake".

  "Hisia hizi hunijia kila siku na hasa kila ninapoona jeneza la mwanajeshi wa Uingereza likishushwa kwenye ndege, hunikumbusha kilichomtokea mwanangu", aliendelea kusema Brierley.

  Tukio hilo lilitokea kwenye hafla hiyo muda mfupi baada ya Blair kuamriwa akae chini na asikilize wakati askofu mkuu wa mji wa Canterbury alipokuwa akitoa hotuba yake kuwaponda wanasiasa kwa kushindwa kufikiria thamani ya maisha ya binadamu kwenye vita vya Iraq.

  Tony Blair alikuwa chanzo cha mjadala mkubwa nchini Uingereza mwaka 2003 kwa kumpa ushirikiano wa kivita George Bush na huku akituhumiwa kuwapotosha waingereza juu ya kuwepo kwa silaha za maangamizi nchini Iraq.
   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  so long as watoto wao hawaendi huko its OK, ebu angalia since the 1980's only one senior ranking officer has died that tells you the value of life. Walindwe wenye high class and that is the ideology behind Muingereza.

  Walisema wanataka kuongeza majeshi ambush waliopata marekani last week imewafanya wafikirie tena. Kibaya zaidi you have to feel sorry for those soldiers patrolling the streets and markets ni a matter of time before a fanatic attacks, well out of no 10 downing street.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,339
  Likes Received: 5,649
  Trophy Points: 280
  Mbafu zao na vizazi vyao...
   
 4. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  well he is so popular they want to make him the EU president. This is the man who is responsible for radar in bongo proper conservative yaani ata sielewi kwa nini alijiunga na labour well all he did was steer the party to the central left.

  You should see what they do now to migrants in africa utachoka na policies zao
   
 5. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Iraq war was a '51-49' decision - Cherie Blair
  Saturday, October 10, 2009, 15:3016
  Choosing to go to war in Iraq was a "51-49" decision, Cherie Blair said in Cheltenham today.
  Speaking at the town's Literature Festival, the wife of the former prime minister said his authorisation of the 2003 invasion was not an obvious decision.
  Mrs Blair earlier told a packed crowd at the Town Hall that her husband was adept at making such close calls appear a lot more straightforward afterwards.
  She said: "A lot of the time these choices are not clear cut. They are not black and white. Instead of being 80-20, many of them are actually more like 51-49.
  "When taking those decisions, Tony is able to step back, absorb all the information and then choose.
  "He is also very good at then convincing everybody else that it was a 70-30 decision all along.
  "I think it [the Iraq war] was one of those 51-49 questions."
  For full story, see Monday's Echo.
   
 6. B

  Bumbwini Member

  #6
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mungu azidi kumlaani mshenzi mkubwa huyu blair na mbwa mwenzake bush,wameua malaki ya watoto wazee na vijana wa irak na afghanistan mungu atawalaani inshaallah,na lazima wapelekwe the haige wakashtakiwe nguruwe hawa.
   
Loading...