Mikoa yenye baridi; jinsi nilivyo tatua tatizo langu la kuamka asubuhi

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Natumaini wote humu wazima, pamoja na mikiki mikiki ya hapa na pale na habari zinazotrend kwa c.a.g na wazee wa liquid namshukuru mungu kwa kuvipa vidole pumzi ya kutype hapa j.f :):):)

Haya sasa, kila mtu ana mapungufu yake ila haya yangu yamekuwa ya ajabu na kugeuka kituko pale nilivyokuwa nikiyawasilisha kwa watu walioonekana wana nia ya kunisaidia huku wakiangua vicheko wakati ni tatizo lililonotesa sana.

Kwa ufupi Mimi nilikua na tatizo la usingizi mzito, hapo nyuma ilikuwa kawaida kwangu kuamka saa tatu asubuhi, kuna kipindi chuoni nilikosa mtihani kwa sababu ya usingizi kitu kilichoniudhi sana na kwa qakati huo huo kuwa kituko kila nikikumbuka.

Iko hivi...enzi hizo nilale saa 2 usiku, saa nne, saa sita hata saa nane ilikuwa lazima niamke saa tatu asubuhi mara nyingi, na hata alarm ikipiga narudi Tena kulala na nikichelewa kuamka najilaumu.

Uzuri ni kwamba nimejiajiri na kazi yangu hapo awali nikiwa na hili tatizo nikiamka saa tatu shughuli ziliendelea kama kawaida, sipati picha kama ningekua nimeajiriwa

Kwa nilichogundua ni kwamba kwa baridi ya mkoa wa mbeya na hata arusha nilikokaa sana ni kwamba nilikua nalala na boksa tu nikijifunika blanketi zito (devet) kitu kilichochangia hili tatizo.

Kwa sasa ni kwamba nikiingia kulala huwa nalala na suruali, soksi na jezi au tshirt nikimalizia na blanketi, nikiweka alarm hata ya saa kumi huwa naamka vizuri tu bila kujivuta vuta na kutaka kurudi kuchapa usingizi, bila alarm saa 12 huwa nimekwisha amka.

Yawezekana ni hali mavazi ya kulalia iliyochangia Mimi kuwa na haya matatizo kwa muda mrefu,

Ni hayo tu, kwa watu wengine wanaosumbuliwa na hali kama yangu kwa mikoa yenye baridi Kali mnaweza kufata njia yangu hii endapo mnasumhuliwa na tatizo la kuamka asubuhi
 
Back
Top Bottom