Mikoa ya Pwani imependelewa sana katika mgawanyo wa Rasilimali za Nchi.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Kwa muda mrefu kumekuwepo malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu kuwa mikoa ya Ukanda wa Pwani (Tanga, Pwani, Morogoro, Linda, Mtwara na Dar) imekuwa ikitengwa na Serikali katika maendeleo na kwamba haifaidiki na keki ya Taifa. Aidha, kwa sasa kuna tatizo kubwa la mauaji katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga, mkoani Pwani, ambazo zimepelekea kusikika tuhuma kuwa, kutengwa kimaendeleo kwa wananchi wa maeneo hiyo ndio kumepelekea mauaji hayo.
Hata hivyo, ukifuatilia katika takwimu za NBS utashangaa kukuta kwamba, mikoa ya Ukanda wa Pwani (ukitoa ya Ukanda wa Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini), inaongoza kwa mbali dhidi ya mikoa mingine iliyobaki nchini katika vigezo karibia vyote vya kimaendeleo licha ya kuwa na watu wachache.
Mikoa hiyo ina mapato makubwa yatokanayo na mishahara kutokana na uwepo wa taasisi nyingi za umma (na hata za binafsi) na hivyo kujikuta wana maisha mazuri kulinganisha na Kanda nyingine za Ziwa, Magharibi na Kati.
Mfano: Mikoa hiyo ya Pwani - Tanga, Pwani, Lindi, Morogoro na Mtwara ina wakazi (sensa 2012) 7,400,000, ukiweka na Dar inakuwa 11,800,000. Ina watumishi wa umma (mwaka 2014) 193,000 na ukiweka Dar inakua 285,000.
Hata hivyo mikoa ya Kanda ya Ziwa - Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Geita ina wakazi 11,800,000 na ukiongeza Kigoma na Tabora inakuwa 16,200,000. Hata hivyo cha ajabu licha ya watu hao wengi kuzidi wa Pwani, ina watumishi wa umma (2014) 134,000 pekee na ukiongeza wa Kigoma na Tabora ni 179,000 pekee.
Aidha, mishahara inayolipwa kwa watumishi waliopo kwenye ukanda wenye watu 11,800,000 wa Ukanda wa Pwani ni Tsh. 8,134,000,000,000/= wakati Ukanda wa Ziwa wenye wakazi 16,200,000 unalipwa mishahara ya Tsh. 2,285,000,000,000/=. Cha ajabu hata ukitoa Mkoa wa Dar es Salaam wenye watu milioni 4.3 na mishahara inayofikia trilioni 5.5, bado mikoa ya Pwani yenye watu wachache milioni 7 pekee ina mishahara inayofikia trilioni 2.6: linganisha na wakazi wa Kanda ya Ziwa milioni 11 (ama 16) lakini mishahara ya trilioni 1.8 (ama 2.2) pekee.
Tafakari.
 
Kwa muda mrefu kumekuwepo malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu kuwa mikoa ya Ukanda wa Pwani (Tanga, Pwani, Morogoro, Linda, Mtwara na Dar) imekuwa ikitengwa na Serikali katika maendeleo na kwamba haifaidiki na kesi ya Taifa. Aidha, kwa sasa kuna tatizo kubwa la mauaji katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga, mkoani Pwani, ambazo zimepelekea kusikika tuhuma kuwa, kutengwa kimaendeleo kwa wananchi wa maeneo hiyo ndio kumepelekea mauaji hayo.
Hata hivyo, ukifuatilia katika takwimu za NBS utashangaa kukuta kwamba, mikoa ya Ukanda wa Pwani (ukitoa ya Ukanda wa Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini), inaongoza kwa mbali dhidi ya mikoa mingine iliyobaki nchini katika vigezo karibia vyote vya kimaendeleo licha ya kuwa na watu wachache.
Mkila hiyo ina mapato makubwa yatokanayo na mishahara kutokana na uwepo wa taasisi nyingi za umma (na hata za binafsi) na hivyo kujikuta wana maisha mazuri kulinganisha na Kanda nyingine za Ziwa, Magharibi na Kati.
Mfano: Mikoa hiyo ya Pwani - Tanga, Pwani, Lindi, Morogoro na Mtwara ina wakazi (sensa 2012) 7,400,000, ukiweka na Dar inakuwa 11,800,000. Ina watumishi wa umma (mwaka 2014) 193,000 na ukiweka Dar inakua 285,000.
Hata hivyo mikoa ya Kanda ya Ziwa - Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Simiyu na Geita ina wakazi 11,800,000 na ukiongeza Kigoma na Tabora inakuwa 16,200,000. Hata hivyo cha ajabu licha ya watu hao wengi kuzidi wa Pwani, ina watumishi wa umma (2014) 134,000 pekee na ukiongeza wa Kigoma na Tabora ni 179,000 pekee.
Aidha, mishahara inayolipwa kwa watu 11,800,000 wa Ukanda wa Pwani ni Tsh. 8,134,000,000,000/= wakati Ukanda wa Ziwa wenye wakazi 16,200,000 unalipwa mishahara ya Tsh. 2,285,000,000,000/=. Cha ajabu hata ukitoa Mkoa wa Dar es Salaam wenye watu milioni 4.3 na mishahara inayofikia trilioni 5.5, bado miko ya Pwani yenye watu wachache milioni 7 pekee ina mishahara inayofikia trilioni 2.6: linganisha na wakazi wa Kanda ya Ziwa milioni 11 (ama 16) lakini mishahara ya trilioni 1.8 (ama 2.2) pekee.
Tafakari.

Mkuu samahani, hii mishahara ya watumishi kanda ya Pwani inalipwa kwa watumishi hewa? Wingi wa watumishi wa kanda ya pwani inatokana na sababu zifuatazo:-

Wizara na makao makuu ya mashirika na taasisi nyingi za umma zipo ukanda wa pwani (Dar es salaam ). Mfano, idadi ya watumishi wa Ikulu ya Dar es salaam ni wengi Sana ukilinganisha na watumishi wa ikulu ndogo ya Chamwino au Iringa.
 
Mkuu samahani Morogoro ni moja ya mikoa inayopatika ukanda wa pwani?
Mkoa wa Morogoro muda mwingine unawekwa katika Kanda ya Pwani inyojumuisha Morogoro, Pwani na Dar. Nimeuweka kwa sababu kiutamaduni una mahusiano makubwa na watu wa Pwani, ukitoa Wilaya za Ulanga na Kilombero. Aidha, hata kijiografia Wilaya za Morogoro na Mvomero ziko karibu na Pwani sawa sawa ama kuliko hata Wilaya za Nachingwea na Liwale mkoani Lindi, ama Nanyumbu mkoani Mtwara.
 
Mkuu samahani, hii mishahara ya watumishi kanda ya Pwani inalipwa kwa watumishi hewa? Wingi wa watumishi wa kanda ya pwani inatokana na sababu zifuatazo:-

Wizara na makao makuu ya mashirika na taasisi nyingi za umma zipo ukanda wa pwani (Dar es salaam ). Mfano, idadi ya watumishi wa Ikulu ya Dar es salaam ni wengi Sana ukilinganisha na watumishi wa ikulu ndogo ya Chamwino au Iringa.
Sawa ndio maana nimeweka takwimu za mikoa hiyo bilateral kuingiza Dar, inaonekana bado wako juu sana ya Kanda ya Ziwa ambapo ina watu Mara mbili yake.
Jamani naomba tuyajadili masuala haya magumu kuonyesha werevu wetu badala ya watu kukimbilia kulaumu JPM kuwa anapendelea udini na ukanda.
 
Wakazi wa Pwani na Ziwa wafanane wote 11,800,000 pumbafu kabisa.
Usinitukane, soma vizuri between the lines, usiwe mvivu. Bila research usikosoe, onyesha idadi ya wakazi wa mikoa niliyoitaja kwa sensa ya watu na makazi mwaka 2012.
 
Usinitukane, soma vizuri between the lines, usiwe mvivu. Bila research usikosoe, onyesha idadi ya wakazi wa mikoa niliyoitaja kwa sensa ya watu na makazi mwaka 2012.
Mkuu hakuna aliyekutukana, watumishi wa umma nchi nzima wapo 570,000 kabla ya kuondolewa vyeti fake, hao wa kwako 11,800,000 Pwani pekee umewatoa wapi?
 
Mkuu kupokea mshahara ni jambo moja lkn kuitumia hiyo mishahara ni Jambo jengine. ebu jiulize hiyo idadi ya watumishi iliyoweka wa pwani ni watumishi wangapi wazawa wa pwani? Na idadi ya watumishi uliyoiweka wa Kanda ya ziwa ni watumishi wangapi wageni kutoka pwani? Unaweza kuwatafuta kotekote na usiwapate. Yani si huko bara wala pwani kwenyewe wapo kwa uchache pia. Alafu kumbuka moja ya changamoto tunayopigia kelele kama taifa kwa wawekezaji kwamba hawahifadhi fedha ktk ma Bank ya ndani, sasa hoja ni sawasawa na hoja ya wa pwani kwamba hata km inawatumishi wengi, lkn wengi hao si watu wa pwani na hawa invest kimaendeleo pwani.
 
Watu huhama mikoani kuelekea pwani. Wafanyakazi wengi wakifika mikoa ya pwani hawarudi kwao, wakiacha mazingira ya mikoa yao kuwa duni.
Unasema watu huhama hilo linajulikana lakini bado Kanda ya Ziwa ina watu wengi kuliko zote. Suala siyo watu kuhama Bali inakuwaje Mkoa Pwani uwe na watumishi wa umma karibia na Mikoa wa Mwanza wakati Mwanza ina watu karibia Mara tatu?
Angalia takwimu hizi za mwaka 2014: Pwani ina watumishi wa umma 29,000 kwa wakazi 1,098,000 wakati Mwanza ina watumishi 35,000 pekee kwa wakazi 2,772,000 - karibia mara tatu, jiulize.
 
Kwa kifupi ukanda wa pwani ndio wenye rasilimali nyingi na zenye uhakika hivyo hata shughuli za kimaendeleo huwa nyingi na za uhakika pia...
 
Unasema watu huhama hilo linajulikana lakini bado Kanda ya Ziwa ina watu wengi kuliko zote. Suala siyo watu kuhama Bali inakuwaje Mkoa Pwani uwe na watumishi wa umma karibia na Mikoa wa Mwanza wakati Mwanza ina watu karibia Mara tatu?
Angalia takwimu hizi za mwaka 2014: Pwani ina watumishi wa umma 29,000 kwa wakazi 1,098,000 wakati Mwanza ina watumishi 35,000 pekee kwa wakazi 2,772,000 - karibia mara tatu, jiulize.
Kwahyo unataka napo papendelewe ka chato airport. Maana watumishi wengi huhama nakuja mikoa karibu na Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom