Mikoa ya Kigoma na Kagera yatajwa kuwa vinara wa kuchafua noti

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Kigoma. Wakazi wa mkoa wa Kigoma wametajwa kuongoza kwa uchafuzi wa fedha hususan noti kuliko mikoa yote nchini, wakifuatiwa na Kagera.

Kauli hiyo imetolewa leo na meneja msaidizi wa uhusiano wa umma kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Victoria Msina alipozungumza na viongozi wa Serikali, madiwani, wafanyabiashara na baadhi ya wananchi mjini Kigoma.

"Utafiti tuliofanya tumebaini mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuchafua noti, fedha zinachakaa mno ukilinganisha na mikoa mingine ndiyo maana tumeamua kutoa elimu kwa umma tukianza na mikoa hii miwili (Kigoma na Kagera)," amesema Msina.

BoT wanalenga kufundisha watu wajue umuhimu wa kutunza fedha na kuepuka uchakavu wa noti na sarafu, sambamba na alama muhimu ili kutofautisha noti halali na bandia.

Meneja msaidizi wa utunzaji fedha na usalama kutoka BoT, Abdul Dollah ametaja baadhi ya sababu zinazofanya noti kuchakaa haraka ni utunzaji mbovu kama vile kushika pesa mikono ikiwa michafu.

"Kuna watu wanafanya kazi ya kuuza mkaa, samaki na mama lishe ambao kuna wakati hulazimika kupokea fedha mikono yao ikiwa michafu, matokeo yake fedha zinachakaa haraka," amesema Dollar.

Ili kuepuka noti kuchakaa mapema, ameshauri wananchi kufungua akaunti benki na kufanya malipo ya bidhaa kwa njia za kibenki au simu za mkononi.

Diwani wa Kigoma mjini, Hussein Kalyango amekiri noti nyingi zinazotumika Kigoma zimechakaa na ni vigumu kuzitumia unapofika mikoa mingine.

"Kuna noti tunazitumia hapa Kigoma lakini hizohizo ukifika nazo Dar es Salaam utaambiwa ni mbovu na hawazipokei. Kwa hiyo lazima BoT mtoe elimu hasa kwa jamii ili wajue umuhimu wa kutunza noti zisichakae mapema," amesema Kalyango.

Watumishi wa BoT wapo mkoani Kigoma kwa ziara ya siku tano kuelimisha jamii juu ya utunzaji bora wa noti na kuepuka uchakavu na wilaya za Uvinza na Kasulu.

-Mwananchi
 
Huyo Msina atakuwa na matatizo binafsi na watu was Kigoma na Kagera.mbona wachaga na wengineo wengi wapo poa huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vizuri. Ushauri wa kwanza ni kuchapisha noti zilizo imara zaidi. Pia ili la kutumia malipo benki badala ya manoti ni la msingi. Kwanza waanze na viongozi wetu na hasa wanasiasa kuwaelimisha ili wasaidie kupromote matumizi hayo kwa wao kuacha kutembea na kugawa mabulungutu ya manoti hadharani.
 
ni wakati wa kwenda na teknolojia. Nchi zilizoendelea asilimia kubwa ya biashara ,manunuzi ,malipo nk nk yanafanyika kwa kadi.mfano. Kununua vitu supermarket, mafuta sheli, nk wanatumia kadi au transfer sio physical cash.hii inasaidia pesa haishikwi mikononi hovyo hata kuchakaa inachukua muda.
 
Kigoma. Wakazi wa mkoa wa Kigoma wametajwa kuongoza kwa uchafuzi wa fedha hususan noti kuliko mikoa yote nchini, wakifuatiwa na Kagera.

Kauli hiyo imetolewa leo na meneja msaidizi wa uhusiano wa umma kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Victoria Msina alipozungumza na viongozi wa Serikali, madiwani, wafanyabiashara na baadhi ya wananchi mjini Kigoma.

"Utafiti tuliofanya tumebaini mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuchafua noti, fedha zinachakaa mno ukilinganisha na mikoa mingine ndiyo maana tumeamua kutoa elimu kwa umma tukianza na mikoa hii miwili (Kigoma na Kagera)," amesema Msina.

BoT wanalenga kufundisha watu wajue umuhimu wa kutunza fedha na kuepuka uchakavu wa noti na sarafu, sambamba na alama muhimu ili kutofautisha noti halali na bandia.

Meneja msaidizi wa utunzaji fedha na usalama kutoka BoT, Abdul Dollah ametaja baadhi ya sababu zinazofanya noti kuchakaa haraka ni utunzaji mbovu kama vile kushika pesa mikono ikiwa michafu.

"Kuna watu wanafanya kazi ya kuuza mkaa, samaki na mama lishe ambao kuna wakati hulazimika kupokea fedha mikono yao ikiwa michafu, matokeo yake fedha zinachakaa haraka," amesema Dollar.

Ili kuepuka noti kuchakaa mapema, ameshauri wananchi kufungua akaunti benki na kufanya malipo ya bidhaa kwa njia za kibenki au simu za mkononi.

Diwani wa Kigoma mjini, Hussein Kalyango amekiri noti nyingi zinazotumika Kigoma zimechakaa na ni vigumu kuzitumia unapofika mikoa mingine.

"Kuna noti tunazitumia hapa Kigoma lakini hizohizo ukifika nazo Dar es Salaam utaambiwa ni mbovu na hawazipokei. Kwa hiyo lazima BoT mtoe elimu hasa kwa jamii ili wajue umuhimu wa kutunza noti zisichakae mapema," amesema Kalyango.

Watumishi wa BoT wapo mkoani Kigoma kwa ziara ya siku tano kuelimisha jamii juu ya utunzaji bora wa noti na kuepuka uchakavu na wilaya za Uvinza na Kasulu.

-Mwananchi
Same thing in burundi au kwakuwa ni majirani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutumia mitandao ya simu ni ghali sana, na wafanyabiashara ndogo ndogo kuhifadhi hela bank nayo ni mtihani.

Endeleeni kuwa elimu namna ya kuzitunza, waswahili husema kitunze kidumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi juzi mada kulalamika WAHA wa Kigoma kukithiri kwa Uchaffu imepita hapa jukwaaani wakatoa povuuuu, sasa hiii ya BOT imeweka sawa mambo.
 
Nilikua najua Kigoma ni kama Zanzibar yaani inajitegemea. Kumbe iko Kagera. Asante kwa taarifa ila hii Uvinza ndio inanichanganya maana nasikia watu wa Dar wanaingiaga uvinza usiku.
 
Na lile dongo lao jekundu hatari, noti za Tsh.500, na 2000 ndo zinakumbwa zaidi.
 
Kigoma. Wakazi wa mkoa wa Kigoma wametajwa kuongoza kwa uchafuzi wa fedha hususan noti kuliko mikoa yote nchini, wakifuatiwa na Kagera.

Kauli hiyo imetolewa leo na meneja msaidizi wa uhusiano wa umma kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Victoria Msina alipozungumza na viongozi wa Serikali, madiwani, wafanyabiashara na baadhi ya wananchi mjini Kigoma.

"Utafiti tuliofanya tumebaini mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuchafua noti, fedha zinachakaa mno ukilinganisha na mikoa mingine ndiyo maana tumeamua kutoa elimu kwa umma tukianza na mikoa hii miwili (Kigoma na Kagera)," amesema Msina.

BoT wanalenga kufundisha watu wajue umuhimu wa kutunza fedha na kuepuka uchakavu wa noti na sarafu, sambamba na alama muhimu ili kutofautisha noti halali na bandia.

Meneja msaidizi wa utunzaji fedha na usalama kutoka BoT, Abdul Dollah ametaja baadhi ya sababu zinazofanya noti kuchakaa haraka ni utunzaji mbovu kama vile kushika pesa mikono ikiwa michafu.

"Kuna watu wanafanya kazi ya kuuza mkaa, samaki na mama lishe ambao kuna wakati hulazimika kupokea fedha mikono yao ikiwa michafu, matokeo yake fedha zinachakaa haraka," amesema Dollar.

Ili kuepuka noti kuchakaa mapema, ameshauri wananchi kufungua akaunti benki na kufanya malipo ya bidhaa kwa njia za kibenki au simu za mkononi.

Diwani wa Kigoma mjini, Hussein Kalyango amekiri noti nyingi zinazotumika Kigoma zimechakaa na ni vigumu kuzitumia unapofika mikoa mingine.

"Kuna noti tunazitumia hapa Kigoma lakini hizohizo ukifika nazo Dar es Salaam utaambiwa ni mbovu na hawazipokei. Kwa hiyo lazima BoT mtoe elimu hasa kwa jamii ili wajue umuhimu wa kutunza noti zisichakae mapema," amesema Kalyango.

Watumishi wa BoT wapo mkoani Kigoma kwa ziara ya siku tano kuelimisha jamii juu ya utunzaji bora wa noti na kuepuka uchakavu na wilaya za Uvinza na Kasulu.

-Mwananchi

Taarifa hii kwa hakika ina ukweli...Binafsi nilipokwenda Kigoma nilipata mshangao kwa namna noti zilivyo chafu
 
Mimi nikiwa Kagera hua sipokei chenji. Mpaka wamenijua wananiita mzee wa keep chenji
 
Back
Top Bottom