Mikoa ya Kanda ya Ziwa kinara wa matukio ya ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mwakilishi wa Shirika la umoja wa mataifa la Elimu ,Sayansi na utamaduni nchini Tanzania (UNESCO) Tirso Dos Santos amesema hayo wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya kupinga ukatiri wa dhidi ya wanawake na watoto yakiyifanyika Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Tirso Dos Santos alibainisha kuwa Kanda ya Ziwa inakiwango cha juu cha ukatili wa kijinsia ikilinganishwa na maeneo mengine ya Tanzania ambapo unyanyasaji wa wenzi ni kati ya 78%katika mkoa wa Shinyanga na Mara na 60%kwa mkoa wa Mwanza,Wakati Pemba / Zanziba kiwango cha ukatioi wa kijinsia ni kati ya 8%na 9%.

Alisema kuhusiana na kuenea kwa unyanyaeaji wa kijinsia nchini Tanzania utafiti huo ulionyesha kuwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto unatifautiana kutoka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine na kati ya maeneo ya Vijiji na mijini.

"Kutokana na hiyo UNESCO pamoja na Shirika la UN women kwa kushirikiana na Serikali watahakisha wanakosha ukatilu wa dhidi ya akina mama na watoto " alisema Tirso Dos Santos.

Priska Saidi (22) mkazi wa Sengerema ni mmoja wa wa akina mama waliofanyiwa ukatili wa kijinsia wakati yuko darasa ya sita alipata ujauzito lakini hadi sasa mtoto ana miaka 11 nasoma darasa ya sita bwana aliyepatia ujauzito hajatoa matumizi yoyote ya mtoto hivyo anaomba Serikali imsaidie.

Kaimu Mkurungezi wa Halmashauri ya Sengerema Samsoni Ndalo alisema anashukuru mashirika haya kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Sengerema kutoa Elimu mashuleni juu ya ukatili wa kijinsia kwa akina mama na watoto
 
Omba radhi

QUOTE="Bujibuji, post: 37403742, member: 13443"]
Wakurya si watu, Wasukuma ndio hao wanabebesha matrip ya mchanga wake zao kisa umemwagwa pasipo.
[/QUOTE]
 
Wakurya si watu, Wasukuma ndio hao wanabebesha matrip ya mchanga wake zao kisa umemwagwa pasipo.
Mkuuu hatari hii. Hii kitu niliisikiaga mahala ikabidi nikimbie dhuu kuna watu wababena ila ubabe wa kijinga. 😂😂😜

Ndo maana wamama wa kanda ile wanyenyekevu kweli yaani.
 
Back
Top Bottom