The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Naomba kusamehewa kwa kushindwa kwangu kulielewa jambo hili mwenyewe na hivyo kuamua kuwashirikisha Greater Thinkers ili kupata logic. Nimesikia na kushuhudia baadhi ya wakaazi wa maeneo husika wakifurahia na kuwashukuru watawala kwa uamuzi wa kuwaundia mikoa au wilaya na kuweka makao makuu katika maeneo yao. Nisichokijua kwa uhakika ni je kuna chochote anachokipata mtanzania wa kawaida katika kuundwa wilaya au mkoa mpya ambacho asingekipata katika wilaya na mikoa ya awali?
Je si wazi kwamba fedha nyingi zitakazotumika kuendeleza makao makuu ya mikoa na wilaya mpya, kuwalipa wakuu wake na wasaidizi wao zingeweza kuleta maendeleo muhimu na makubwa katika mikoa iliyokuwapo awali? Tafadhali tutafakari pamoja swala hili. Was this decision that important to our poor country?