Mikoa wa Katavi na Rukwa ni kiboko

banned do

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
574
508
Tangu nianze kutembelea hii mikoa katika maeneo mbalimbali kama Inyonga,Majimoto,sumbawanga,mpimbwe na hapa katavi mjini nimekutana na watu wenye magonjwa ya kushangaza sana.Nilikutana na mama mmoja ambaye mwili wake wote ulikuwa umeharibika(Ni dhambi kusema umeoza) huku ukimwaga maji chapachapa.

Siku nyingine ndani ya basi nilishangaa kumuona mzee mmoja aliyekuwa amepanda na dumu la maji la lita tano na kila baada ya muda mfupi alikuwa akijimwagia maji kwa madai kuwa miguu yake inawaka moto.

Pia wakazi wa huko walinishangaza baada ya kuniambia kuwa huko kwao radi inauzwa,nilishngaa kwa sababu najua radi ni umeme tuli.Lakini jamaa waliniambia nikitaka hata kwa elfu kumi ninaipata .

Pia mtu alishawahi kupanda basi na kuwafanya wasafiri wenzake wote kushindwa kula wala kunywa maana alikuwa na kidonda kikubwa ambacho kilikuwa na wadudu na kilifanya hali ya hewa ya basi zima kubadilika na hata aliposhuka hali haikuwa shwari.

Nimetembea sehemu nyingi sijawahi kukutana na maradhi ya aina hii lakini nilipowauliza wakazi wa maeneo haya walihusisha maradhi hayo na imani za kishirikina.

Najua mtaomba picha,picha ninazo lakini sina ujasiri wa kuzianika mtandaoni.
 
Huko kuna kijiji kule Nkasi kinaitwa Kalundi, huko ni mkusanyiko wa wachawi waliotimuliwa sehem mbali mbali..ukijifanya gangwe wanakukomoa tu unaambiwa unaweza chemsha maharage wiki nzima na hayaivi: kuna siku viongozi wa serikali walikua wanahimiza mchango ujenzi wa maabara! I naambiwa kila walipokua wanatembea wanakutana na wanawake na watoto tu mbaya zaidi wakawa watu wanawacheka mwishowe wakahoji mbona wanachemka kumbe walikua uchi KWAMBA wananchi wanawaona wako uchi...Ila sumbawanga town pazuri mno kuliko hata bukoba! Lami nzuri..kumepangika..bata la kufatu!
 
Asee huko ni sheeda.
 
Plenty of exaggerations.Mlioko Sumbawanga, ila siyo wa Sumbawanga, mmekaa huko muda mrefu nadhani mna tangible informations kuliko za observer wa wiki moja!
 
Back
Top Bottom