Mikoa na wilaya mpya zote zilizotangazwa mwaka jana zifutwe mara moja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikoa na wilaya mpya zote zilizotangazwa mwaka jana zifutwe mara moja!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Mar 1, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Mwaka jana serikali ilitangaza kuanzishwa kwa mikoa, wilaya na kata mpya. Hata hivyo hakuna mkoa, wilaya wala kata moja iliyoanza kazi kwa sababu serikali haina fedha. Aidha hakuna mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya wala katibu kata aliyeteuliwa! Kibaya zaidi hakuna mahali popote ambapo miundo mbinu kama ofisi na nyumba za watumishi imeanza kujengwa.

  Baadhi ya wilaya za zamani zinakosa wakuu wa wilaya kwa sababu hazina ya nchi ni tupu. Wilaya za zamani kama Bahi iliyoko mkoani Dodoma watumishi wake kuanzia mkuu wa wilaya hadi muhudumu wa ofisi anakaa na kufanya kazi mjini Dodoma kiasi cha kusababisha ofisi ya halmashauri ya Bahi iliyojengwa kwa fedha za wananchi imeanza kuhujumiwa kwa kuvunjwa vioo na baadhi ya vitu kuibiwa kwa sababu hakuna walinzi.
  1. Kwa nini serikali iendelee kututia hasara na kutuongezea umaskini kwa kuongeza maeneo mapya ya utawala wakati uwezo hatuna?
  2. Kwa nini fedha ambazo zingeweza kutumika kwa kujenga zahanati, shule, barabara, madawati nk zitumiwe hovyo namna hii bila huruma?
  3. Kwa nini serikali yetu inafikiria kuwa kwa kuongeza maeneo ya utawala ni kuleta maendeleo?
  Wana JF ni vema tukatumia muda huu kuiambia serikali yetu kufuta mara moja mipango ambayo haina tija!
   
 2. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi sana mkuu. Ufikirie ati kuweka Mkoa wa Geita just 90 kms toka Mwanza. Watu wanawaza kuweka au kuongeza mitandao yao ya wizi tu and nothing more. Sana sana ni kutafuta sehemu ya kuweka wapendwa wao tu. Ni hasara tena kubwa kuliko.
   
 3. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,929
  Likes Received: 1,461
  Trophy Points: 280
  watu wanatafuta pa kupata ulaji kwa hiyo tusishangae saaaana!
   
 4. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa tunajifunza na kuona udhaifu wa serikali yetu katika mawasiliano ya ndani kwa ndani baina ya taasisi zake. Pia, udhaifu wa watendaji wake katika kutoa ushauri. Dalili za kutokuwa na uwezo wa kifedha serikalini zilionekana siku nyingi na hakukuwa na mbinu mbadala za kukusanya mapato hivyo nilitegemea watu wa wizara ya fedha, Tamisemi, mipango, ofisi ya pm na taasisi husika katika uundwaji wa wilaya na mikoa mipya wangemshauri rais kuwa nguvu haipo kwahiyo suala hili lisubiri lisitangazwe.
   
 5. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Mwishoe ntatukana kwa hasira niliyonayo.
   
 6. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Tafadhali usitukane bali unatakiwa kusaidia katika kuhakikisha serikali yetu inafanya kazi kwa busara na kupambana kuondoa umaskini na siyo kufuja rasilimali kidogo tulizonazo!
   
 7. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,054
  Likes Received: 1,440
  Trophy Points: 280
  1. Mie fikra zangu ni kuwa hii mikoa ilianzishwa ili CCM wapate KURA mwaka 2010. Kwa kuwa lengo lao limetia, hawana MSUKUMO wa kutekeleza mipango yao.
  2. Wakati mkoa wa KATAVI UNAPAA katika mipango ya upanuzi, mikoa mingine kama SIMIYU wasukuma na Wanyantuzu wanapigana vikumbo wapi makao makuu ya mkoa yawe! (Wengine wanaona kuwa itikadi za kisiasa zinakwamisha mipango ya maendeleo).
  3. Mikoa yote iliyoanzishwa ina wabunge wa VITI MALUUM wa CCM, (kwa mfano kule NJOMBE ni Pindi Chana).
  4.Mie naona MIKOA na Wilaya Isi/zisi FUTWE bali serikali ITEKELEZE lengo lake la kui/kuzi anzisha. Kama haiwezi ibanwe!
   
 8. j

  jjjj Senior Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  1. Ndugu yangu Ileje hiyo ndiyo serikali yetu,kwani waliyasema hayo walitegemea hizo hela zinatoka wapi za kuanzisha mikoa mipya ama wilaya mpya?waliyasema hayo kwakuwa walihitaji kura zenu sasa walishazipata
   ninyi mnataka nini tena wanasema akili ya mbayuwayu changaya na ya kwako.
   
 9. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135

  Viongozi wetu pamoja na Rais walishauriwa kwa kina kuwa kuanzisha mikoa na wilaya mpya kwa sasa kutaiongezea mzigo Serikali na mchanganuo wa kina ulifanywa kuhusu gharama ya kuanzisha mkoa na wilaya mpya lakini kutokana na ugumu wa uelewa walionao viongozi wetu hawakutaka kuzingatia ushauri huo na matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona kwa sasa.

  Itakuwa siyo vyema kuwalaumu watendaji wanaohusika na masuala ya kitaalamu na kutoa ushauri kwani kazi yao waliifanya kwa ufasaha kabisa ila tatizo liko kwa viongozi wanaotoa maamuzi yao kisiasa zaidi.
   
Loading...