Mikoa mipya ina upya gani?

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,888
1,347
Mi najiuliza kwamba tunapozungumzia mikoa mipya upya wake ni upi hasa tukizingatia kwamba
wote tunaelewa "kitu kipya maana yake ni nini" hizi sehemu zilikuwepo toka enzi hizo leo hii zimeungwa ungwa zinaitwa mikoa mipya ili nini ?
Tunataka paitwe mkoa mpya ili tufanye kitu gani?
Nani tunataka awe mkuu wa mikoa hii na kwa sababu gani?
Kuna umuhimu gani wa kubadilishwa majina ya hizi sehemu na kupaita mikoa mipya ?
Je ni kwa nini pasiendelezwe bila kupaita mkoa mpya ?
Tumefanya nini kwa mikoa ya zamani?
Tukipaita mkoa mpya kuna nini kinapatofautisha na palivyokua awali?
Mikoa hiyo inatakiwa iwe na wilaya ngapi na wakuu wa wilaya hizo watakua kina nani na kwa nini?
 
Umesema vizuri sana mkuu! Bora ingekuwa ukiweka mkoa mpya na kasi ya maendeleo inaongezeka,kumbe ni kupeana ulaji tu!
 
Mkuu enzi zetu shule ya msingi ukiulizwa swali hili jibu lake lilikuwa rahisi lakini siku hizi mhuuuuu.
 
mh subiri iongezeke upate jibu la uhakika.kwani hata njombe itakuwa mkoa.

Njombe haitakuwa mkoa mkuu...Muunganiko wa Ludewa,njombe na makete ndio watengeneza Mkoa wa njombe.Na kuna wilaya mpya itaitwa wang'ing'ombe itakuwa ndani ya huu mkoa.
 
Mzee serengeti naomba tuheshimiane tafadhali. Hakuna tanzania bara, kuna Tanganyika. Ebo!
 
<span style="font-family: verdana">Njombe haitakuwa mkoa mkuu...Muunganiko wa Ludewa,njombe na makete ndio watengeneza Mkoa wa njombe.Na kuna wilaya mpya itaitwa wang'ing'ombe itakuwa ndani ya huu mkoa.</span>
<br />
<br />
 
Wewe kaka kuna tafsi ya mkoa mpya ujue?? Aliye nacho ale na asiye nacho akapate...Hakuna mtu wa chini anayeibuka na kupewa nafasi zaidi ya walio kwisha kuwa juu kuendelea kupanda hata kama wanatumia Masaburi kuweka mambo yao fresh.....Mimi nasema watu wanapewa ulaji kwa fadhila tuu..HIKI CHEO SIJUI HATA MAANA YAKE NINI...mara kuna Meya, mkurugenzi, Mkuu wa mkoa sasa kila mmoja wajibu wake nini na jee hizi idara ni kubwa kuliko uwaziri ambao unatizama nchi nzima?? people ni lazima kupunguza mibajeti isiyo na maana...Sijui bwana mimi nakereka tuu hapa...
 
ukiandalia in 3-dimension kuna opportunities za uongozi, dealz mpya za kutajirika chapchap na kugawana umaskini. ntarudi na faida kwa maskini baadae
 
Mimi ninavyoona kuongeza mikoa na wilaya nikuongezea tu mzigo wananchi nakutumia rasilimali za nchi vibaya , Kutakuwa na wakuu wa mikoa ,wilaya, wakurugenzi naviongozi wengine wengi tu ambao watalipwa mshahara
 
Njombe haitakuwa mkoa mkuu...Muunganiko wa Ludewa,njombe na makete ndio watengeneza Mkoa wa njombe.Na kuna wilaya mpya itaitwa wang'ing'ombe itakuwa ndani ya huu mkoa.

Kaka unapata shida kuelimisha watu ambao hawajajipanga. Hii basic information walitakiwa waijue kabla hata hawajaingia humu JF, lakini haraka za kuchangia ndo zimejaza upotoshaji huu.
 
Hiyo ndo gharama ya utawala ambao ni de-centralized. Wewe ulitaka kila kitu kifanyikie Dar?Unajua Mkoa kama wa Rukwa ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kwamba Wilaya ya Mpanda peke yake ilikuwa kubwa kuliko Mtwara mara mbili au zaidi. Acha kuangalia gharama za kuwa na institutions za utawala badala ya kuangalia gharama za kushindwa kuwafikia wananchi na kuwahudumia ipasavyo.
 
Mkuu wa kaya ameona wananchi mnawatosa washkaji zake mf. Bendera, ameamua kubuni mradi wa kuwapa chakula. Ila hakuna la zaidi hapo.
 
Back
Top Bottom