Mikoa Mipya 3 ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikoa Mipya 3 ya Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jun 6, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mikoa mitatu iliyoanzishwa mwaka jana kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ni:

  Mkoa wa Njombe
  ambao unaundwa na wilaya za Njombe, Ludewa na Makete ambazo awali zilikuwa ndani ya Mkoa wa Iringa na wilaya mpya ya WangingÂ’ombe sehemu ya iliyokuwa wilaya ya Njombe.

  Mkoa wa Geita unaoundwa na Wilaya za Geita (iliyokuwa mkoa wa Mwanza), Bukombe (kutoka Mkoa wa Shinyanga) na Chato (iliyokuwa ya Mkoa wa Kagera). Mkoa huu pia una Wilaya mpya ya NyangÂ’hwale (imetokana na kugawanywa kwa Wilaya ya Geita).

  Mkoa wa Simiyu ambao unaundwa na Wilaya za Bariadi, Meatu na Maswa (zilikuwa za Mkoa wa Shinyanga), Wilaya mpya ya Busega (awali ilikuwa mkoani Mwanza na Wilaya ya Itilima (inatokana na kugawanywa kwa iliyokuwa Wilaya ya Bariadi).

  Kwa mamlaka aliyopewa, Rais anaweza kuigawa nchi katika mikoa au Wilaya ili kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utendaji wa Serikali kuu kwa kupunguza ukubwa wa maeneo ya mikoa mama ili wananchi wapate huduma za kiutawala ngazi ya mikoa kwa karibu.
   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Shukrani kaka kwa taarifa nilikuwa sijui kama kuna mikoa zaidi ya 26 ya Jamhuri ya Muungano Tanzania,sijui sasa makao makuu ya hiyo mikoa ni wilaya zipi kati ya zinazounda hiyo mikoa,na sijui wakulu wa hiyo mikoa na wakulu wa wilaya hizo ni akina nani,au bado mkulu anangpjea kutoa sandakalawe kwa wateule wa njii hii wachache
   
 3. Shagihilu

  Shagihilu Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  X-PASTER MIKOA ILIYOUNDWA NI ZAIDI YA 3:
  1. [FONT=&quot]Njoruma
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Ludewa
  [/FONT][FONT=&quot]Makete
  [/FONT][FONT=&quot]Njombe
  [/FONT][FONT=&quot]Wanging'ombe

  2. [/FONT]
  [FONT=&quot]Katavi
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mpanda
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kaliua
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mlele

  3. [/FONT][FONT=&quot]Simiyu
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Bariadi
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Itilima
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Meatu
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Maswa
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Busega
  4.[/FONT]
  [FONT=&quot]Geita
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Geita
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Nyang'hwale
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mbogwe
  [/FONT]
   
 4. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama nia ni kutaka kufikisha maendeleo kwa urahisi kwa wananchi kama inavyodaiwa mi nao ni kuongeza ghalama zisizo za msingi na kuitwika serikali mzingo zaidi.
   
 5. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  wilaya kumi mpya ni zipi?
   
 6. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Napenda mnijuze je ni mikoa 3 au 4 naona mkoa wa Katavi hautajwi au mpango wa kuwa mkoa umefutwa? Mikoa inayotajwa ni Njombe,Geita Na Simiyu lakini Katavi hatajwi why?
   
 7. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Naomba niwaambie ukweli ndugu zangu, hakuna kitu kama hicho cha mikoa mipya wala wilaya mpya kwa sasa, zile zilikuwa ni danganya toto ili Kikwete aweze kupata kura wakati tukielekea uchaguzi mkuu kwani hali yake ilikuwa mbaya sana. Ushahidi ni katika bajeti itakayosomwa bungeni muda si mrefu ambayo inahusu mikoa 21 tu na soma hapa Bajeti ijayo haiitambui mikoa mipya Kikwete mkweere ni msanii mno na hana uwezo wowote wa kiuongozi. Mwalimu Nyerere aliona mbali sana 1995 kumkataa yeye na swahiba wake Lowassa. ndiyo maana akasema "Kama unaupenda uzuri wa sura yake mkaribishe nyumbani kwako umpe chai" lakini si kwa uongozi.

  Nasema hakuna mikoa mipya!....
   
 8. Jerhy

  Jerhy JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2016
  Joined: Jul 11, 2013
  Messages: 3,152
  Likes Received: 340
  Trophy Points: 180
  Hivi mpka leo imefikia mikoa mingapi na ni ipi
   
Loading...