Mikoa mingine igeni mkoa huu kuwaamini vijana

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,067
709
Wananchi wa mkoa wa Kigoma hawana budi kumshukuru Rais Kikwete kwa kuwakumbuka angalau kwa mara ya kwanza wananchi wa mkoa wa Kigoma wamepata kuona barabara ya rami, si haba. Rais Kikwete amejenga daraja katika mto maragarasi, na barabara kutoka Tabora mpaka Kigoma ipo katika hatua nzuri kwa kiwango cha rami. Ni rais wa kwanza kumteua angalu waziri mmoja kutoka mkoa wa Kigoma, mheshimiwa Christopher Chiza. Tangu uhuru kama inavyoonyesha hapo chinibhakuna waziri aliyewahi kuteuliwa kuwa waziri kutoka mkoa wa Kigoma, tofauti na naibu waziri mmoja tu. Kwa sababu hizo wananchi wa mkoa wa Kigoma wamekuwa mfano wa mabadiriko ya kisiasa na kiuchumi. Wananchi wake wamepoteza imani kwa cha tawala CCM na kuunga mkono vyama vya CHADEMA NA NCCR MAGEUZI. Ni mkoa pekee unaoamini vijana kuwaletea maendeleo. Ukiacha wabunge 2 tu kutoka CCM wabunge wote waliobaki kutoka Kigoma ni vijana. (ZITO-CDM, DAVID KAFULILA-NCCR, OBAMA-CCM, MOSES MACHALI-NCCR NA MKOSAMALI-NCCR). CCM bila kufanya maendeleo yanayoeonekana itawachukua muda mrefu kurudisha imani kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma. Ni wananchi wa kwanza kuwa na imani na upinzani kwa kumchagua Dr Aman Warid Kabour kutoka Chadema 1995. wakati mikoa mingine ikiwa ndiyo inapata changamoto za kisiasa kutokana na vipigo vya polisi wananchi wa mkoa wa Kigoma walianza kupata changamoto hizo tangu 1995. wakati ule reli ya kati ilifungwa kusafirisha abiria ili kusafirisha askari wa jeshi la POLISI-FFU kwenda kupambana na wananchi wasifanye uchaguzi wa kidemokrasia. CCM kwa kutumia polisi walifikiri kuwa wnanachi wangetishika kumbe ndiyo walikuwa wanawapa morali zaidi, kwaani baada ya miaka 10 majimbo yote ya mkoa wa Kigoma ilikuwa wachukuliwa na vyama vya CHADEMA NA NCCR MAGEUZI. yaliyotokea jimbo la Kgm mjini na Kasulu Magharibi yanajulikana. Dawa pekee ni kuleta maendeleo.

Mwisho: Je wabunge kutoka mkoa wa Kigoma hawana uwezo wa kuongoza wizara au ni ubinafsi wa marais wetu waliopita? je wabunge walipita kutoka Kigoma km Pr. Mbwiliza, Mpologomyi na nk.



BARAZA LA MAWAZIRI TANZANIA TANGU UHURU NI WAZIRI MMOJA (C.CHIZA) KUTOKA MKOA WA KIGOMA , JE UWEZO NI MDOGO.?


Mawaziri Wakuu

1. Julius Kambarage Nyerere
2. Rashid Mfaume Kawawa.
3. Edward Moringe Sokoine,
4. Cleopa David Msuya
5. Edward Sokoine
6. Dk Salim Ahmed Salim
7. Joseph Sinde Warioba,
8. John Malecela
9. Cleopa David Msuya Msuya
6. Frederick Sumaye
7. Edward Ngoyai Lowassa
8. Mizengo Pinda


Mawaziri-Ofisi ya Rais (Ikulu)

1. Ali Hassan Mwinyi
2. Profesa Kighoma Ali Malima
3. Amran Mayagila
4. Fatma Saidi Ali
5. Wilson Masilingi
6. Sofia Simba
7.Hawa Ghasia

MAWAZIRI-OFISI YA MAKAMU WA RAIS
1. Aboud Jumbe
2. Edward Sokoine
3. Muhammad Seif Khatibu .
4. Muhammad Seif Khatib
5. Dk. Batilda Burian
7. Dk. Husesein Mwinyi
8. Mark Mwandosya (Mazingira)


MAWAZIRI-OFISI YA WAZIRI MKUU
1. Peter Kisumo
2. Robert Ng’itu
3. Edward Lowassa
4. Dk. Batilda Buriani
5. Philip Marmo
6. Aggrey Mwanri
7. Celina Kombani

Mawaziri
(a). Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
1. Dk. Stirling (Waziri)
2. Derek Bryceson
3. Lawi Nangwanda Sijaona
3. Dk Aaron Chiduo
4. Prof Philemon Sarungi
5. Prof David Mwakusya

Wizara ya Ardhi

(i) Mawaziri wa Ardhi na Nyumba
1. Lawi Nangwanda Sijaona
2. Austin K.E. Shaba
3. Musobi Mageni
4. John Mhaville,
5. Thabita Siwale
6. Gideon Cheyo
7. Mercel Komanya,
8. Edward Lowassa
9. John Pombe Magufuli
10. John Chiligati,


Wizara ya Elimu
1.Solomon Eliufoo,
2. Chediel Mgonja,
3. Abel K. Mwanga
4. Nicholaus Kuhanga,
5. Padri Simon Chiwanga
6. Thabitha Siwale
7. Prof Philemon Sarungi,
8. Margareth Sitta,
5. Profesa Jumanne Maghembe,

SAYANSI, TEKNOLOJIA, NA ELIMU YA JUU:
A. MAWAZIRI
1. Dk William Shija,
2. Professa Peter Msolla,

Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi (sasa wizara ya Miundombinu)
1. Mustafa Nyang’anyi
2. William Kusila
3. Dk Shukuru Kawambwa

Wizara ya Fedha
1.Mark Bomani
kati ya 1962 na 1965
2. Abdulrahman Mohamed Babu,
3. Amir Jamal,
3. Abdulrahman Mohamed Babu,
4. Paul Bomani, kuanzia
5. Amir Habib Jamal
6. Edwin Mtei,
7. Profesa Kighoma Ali Malima
8. Cleopa David Msuya
9. Profesa Simon Mbilinyi
10. Steven Kibona
11. Daniel Yona,
12. Basil Pesambili Mramba,
13. Zakhia Hamdani Meghji
14. Mustafa Mkulo,
15.


Wizara ya Ulinzi
1. Abdallah Twalipo,
2. Philemon Sarungi
3. Profesa Juma Kapuya
4. Dk Hussein Mwinyi

(b) Manaibu waziri
1. Seif Bakari,
2. Abdallah Twalipo,
3. Edgar Maokola Majogo,
4. Emmanuel Nchimbi
5. Dk. Hussein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani

1. Job M., Lusinde,
2. Said Maswanya,
3. Ali hassan Mwinyi,
4. Muhidin Kimario, kuanzia 1985
5. Augustino Lyatonga Mrema,
6. Lawremce Masha
7. Shamsi Vuai Nahodha
8. Dr.Emmanuel Nchimbi


Wizara ya Nishati na Madini
1. Jeremiah S. Kasambala,
2. Wilbert Chagula,
3. Al-Noor Kassum,
4. John Malecela,
5. Jakaya Kikwete,
6. Daniel Yona,
7. Shamsa Selesia Mwangunga
8. William Ngeleja
9. Pro Sospeter Mohiong’o
 
Back
Top Bottom