Mikoa 20 yathibitisha kuhudhuria kesi ya Mbowe Kisutu Agosti 5, 2021

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Kesi ya kubambikizwa Ugaidi Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe inatarajiwa kutajwa Alhamisi August 5 Kisutu jijini DSM.

Akizungumza na wanahabari jana Jumamosi Katibu Mkuu John Mnyika aliwataka wana Chadema na wananchi kufurika Kisutu siku ya Alhamisi August 5 ili kufuatilia kwa ukaribu kesi hiyo na kuonyesha mshikamano kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Mpaka Leo saa 5 Asubuhi taarifa kutoka makao makuu ya Chadema zinasema tayari mikoa 20 ya Tanzania imethibitisha kutuma wanachama kwa gharama zao kuhudhuria kesi hiyo.

Kesi hiyo inayolaaniwa kote duniani kutokana na hila za kisiasa kumnyamazisha Freeman Mbowe inaonekana kuvuta hisia za kila mpenda haki.

Hali inavyoonekana huenda zaidi ya watu elfu 5 wakahudhuria kesi hiyo kitendo ambacho kitazidi kuvuta hisia za Dunia.

Vyombo kadhaa vikubwa vya Habari Duniani Kama BBC, CNN, DW, Aljazeera, na VOA vimekuwa vikifuatilia na kutangaza Mara kwa Mara habari hizi za uonevu wa dola dhidi ya Mbowe.

Freeman Mbowe alibambikwa kesi ya Ugaidi ili kumdhibiti kutokana na kampeni yake ya kudai Katiba Mpya.Jambo lililo wazi ni kwamba kila mtu ndani na nje ya nchi anaelewa kesi hii ni ya uongo na isiyo na maana yoyote yenye Lengo la kumdhibiti Demokrasia nchini.

Updates Jumatatu 2 August

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saimon Sirro Leo ameitisha Mkutano wa wanahabari na kuonya kile alichosema mpango wa CDM kupanga kuhudhuria kesi ya Mbowe Kisutu Alhamisi.

Huku akionekana kuwa na chuki ya ndani kwa kile wananchi kulaani Mbowe kubambikizwa kesi ya Ugaidi, IGP Sirro amesema Mbowe ana makosa makubwa Sana ya kufanya Ugaidi na kulipua vituo vya mafuta.IGP huyo ameenda mbali zaidi na kuonya wale wote wanaosema Mbowe anaonewa akidai wanaingilia Uhuru wa Mahakama huku yeye mwenyewe akimhukumu Mbowe kwamba ni Gaidi
 
Hehehehehehe siasa za Tanzania leo mnampigania mwanasiasa fulan watu wanapata ulemavu wanakufa dakika ya mwisho mwanasiasa huyohuyo anaishia kuunga juhudi

All in all kila kheri kamanda mbowe watanzania wanakusaliti sana ingekua nchi zingine sitaki kusema ingekuwaje
 
Kesi ya kubambikizwa Ugaidi Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe inatarajiwa kutajwa Alhamisi August 5 Kisutu jijini DSM.

Akizungumza na wanahabari jana Jumamosi Katibu Mkuu John Mnyika aliwataka wana Chadema na wananchi kufurika Kisutu siku ya Alhamisi August 5 ili kufuatilia kwa ukaribu kesi hiyo na kuonyesha mshikamano kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe.
Mkuu niko njiani kama vipi waje watufunge wote..
 
Akizungumza na wanahabari jana Jumamosi Katibu Mkuu John Mnyika aliwataka wana Chadema na wananchi kufurika Kisutu siku ya Alhamisi August 5 ili kufuatilia kwa ukaribu kesi hiyo na kuonyesha mshikamano kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe
Mnyika ana mambo ya kizamani sana
Mafuriko hayaachii mtuhumiwa
Hao ndio chadema waliopiga kelele corona ipo,leo KM anahimiza watu wakajazane mahakamani
 
Kesi ya kubambikizwa Ugaidi Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe inatarajiwa kutajwa Alhamisi August 5 Kisutu jijini DSM.

Akizungumza na wanahabari jana Jumamosi Katibu Mkuu John Mnyika aliwataka wana Chadema na wananchi kufurika Kisutu siku ya Alhamisi August 5 ili kufuatilia kwa ukaribu kesi hiyo na kuonyesha mshikamano kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Mpaka Leo saa 5 Asubuhi taarifa kutoka makao makuu ya Chadema zinasema tayari mikoa 20 ya Tanzania imethibitisha kutuma wanachama kwa gharama zao kuhudhuria kesi hiyo.

Kesi hiyo inayolaaniwa kote duniani kutokana na hila za kisiasa kumnyamazisha Freeman Mbowe inaonekana kuvuta hisia za kila mpenda haki.

Hali inavyoonekana huenda zaidi ya watu elfu 5 wakahudhuria kesi hiyo kitendo ambacho kitazidi kuvuta hisia za Dunia.

Vyombo kadhaa vikubwa vya Habari Duniani Kama BBC, CNN, DW, Aljazeera, na VOA vimekuwa vikifuatilia na kutangaza Mara kwa Mara habari hizi za uonevu wa dola dhidi ya Mbowe.

Freeman Mbowe alibambikwa kesi ya Ugaidi ili kumdhibiti kutokana na kampeni yake ya kudai Katiba Mpya.Jambo lililo wazi ni kwamba kila mtu ndani na nje ya nchi anaelewa kesi hii ni ya uongo na isiyo na maana yoyote yenye Lengo la kumdhibiti Demokrasia nchini.
Mama anatumika vibaya
 
Kwa hiyo makongamano ya katiba mpya nchi nzima yameishia hapo Kwa sasa?
 
Mungu ibariki Chadema
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom