Mikiki ya Ujasusi katika Ikulu ya Ahasuero

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,050
50,998
KITIMU TIMU CHA JASUSI ESTA NDANI YA IKULU.

Na, Robert Heriel.


Huu ni muendelezo wa makala za kijasusi ambazo zitaonyesha nafasi ya mwanamke katika medani ya fani ya Ujasusi.

Jana nilipokea maswali mengi kuhusiana na nini maana ya ujasusi. Hivyo nitaeleza maana hiyo hapa ili wote tuweze kuwa kitu kimoja katika makala hii.

UJASUSI ni fani inayohusisha utafutaji wa siri, ukusanyaji wa taarifa za siri, uibaji wa siri za nchi moja kwa manufaa ya nchi nyingine. Mtu anayejishuhulisha na Ujasusi hujulikana kama JASUSI. Ujasusi ni moja ya fani hatari zaidi duniani kutokana na kuwa ukikamatwa adhabu yake ni kifo.

Ujasusi una pande mbili ambazo ni Usaliti na Uzalendo. Unapokamatwa kwa kosa la kutoa siri kwenda nchi nyingine unaitwa msaliti wa nchi hiyo wakati huo huo kwa upande wa pili utafahamika kama Mzalendo na mtu wa heshima.

Jasusi lazima awe na elimu kubwa na kama sio elimu basi awe na akili au kipaji fulani muhimu ambacho kupitia hicho kazi yake ataifanya kwa urahisi. Ikumbukwe kuwa Jasusi ni mpelelezi kwa ngazi ya kimataifa. Hivyo hawezi kuwa mtu wa hivi hivi bali lazima awe amepewa mafunzo maalumu kuepusha hatari ya kukamatwa na kuuawa. Hii ni tofauti na Kachero kwa ngazi ya kitaifa(Ndani ya nchi). Kachero kwa ngazi ya kitaifa anaweza kuwa mtu yeyote hata asiye na elimu.

Kama nilivyokwisha kusema lengo la Jasusi ni kupata taarifa za siri za nchi moja kwa manufaa ya nchi nyingine. Manufaa ya msingi ya kijasusi yanajikita katika sekta ya ulinzi na usalama, Sekta za kiuchumi, na Kisiasa. Hii ni kusema Ujasusi ni fani inayohitaji wataalamu wenye elimu nyingi kwa wakati mmoja. Hii ni kusema Jasusi kwa sehemu kubwa anapaswa awe Genius/Gifted. Mafunzo muhimu kwa zama hizi ni awe anaujuzi wa masuala ya Tanakilishi(Kompyuta), Awe anajua lugha au mwepesi kujifunza lugha ngeni, Awe na mafunzo ya kijeshi, awe mwepesi kuchanganua mambo, awe mwepesi kukariri kila atakalo liona na kulikumbuka hii ni pamoja na ujuzi wa mambo ya kijiografia hasa Ramani na mambo mengine.

Baada ya kuelezea kwa uchache kuhusiana Maana ya Ujasusi sasa nirudi kwenye Mada yetu ya leo.

Nakurudisha nyuma kabisa katika Ufalme wa Ahasuero aliyemiliki tokea bara Hindi mpaka nchi za Kushi(Ethiopia na Sudan ya leo) akitawala majimbo 127. Ahusuero alikuwa Mfalme wa Waajemi(Iran ya leo) Persian Kingdom. Ambapo ni baada ya kuanguka kwa dola la Kiashuru( Syria ya leo). Wamedi na Waajemi walichukua kila kitu kilichokuwa chini ya Dola la Kiashuru ambapo utawala wa Kifalme wa Belteshaza mtoto wa Nebuchadreza ulipodondoka.

Mfalme Ahasuero baada ya kumfukuza Malikia Vashti kutokana na kumkosea heshima akahitaji Malikia mwingine atakayekuwa mke wake. Migogoro katika taifa fulani ni fursa kwa taifa jingine kujiimarisha kijasusi na kunufaika na mgogoro huo. Hii ni kusema kuwa mgogoro wa Mfalme Ahasuero na Malikia Vashti ilikuwa kete muhimu kwa taifa la waisrael kuitumia kujikomboa na mateso ya Waajemi. Kumbuka Wayahudi muda huu walikuwa wapo uhamishoni baada ya kuchukuliwa mateka kipindi kile cha Mfalme Nebuchdreza Mfalme wa Babeli. Sasa bado wapo kama mateka utumwani chini ya utawala wa Waajemi, chini ya Mfalme Ahasuero, huko Shushani Ngomeni ( Jimbo la Khuzestan, nchini Iran leo hii)

Sasa Mfalme Ahusuero akaagiza watafutwe mabinti wazuri wenye Bikra ili ajichagulie Malikia. Hapo ndipo Jasusi Mordekai(Mjomba wake Hadasa) akatumia ujasusi kudaka taarifa hiyo iliyomsaidia kumpandikiza Hadasa kwa manufaa ya taifa la Israel.

Hadasa alikuwa mwanamke mrembo aliyelelewa na Mjomba wake(Jasusi) baada ya Mama na Baba yake kufariki. Hii ni kusema Hadasa alikuwa Yatima. Hadasa ni jina la Kiebrania lenye maana ya "mti wa myrtle" ambao ulikuwa na "harufu nzuri" lakini "ladha chungu" pia Hadasa ilimaanisha "Haki"

Mordekai katika kutimiza lengo la kijasusi kwa manufaa ya Waisrael alishamfundisha Mrembo Hadasa baadhi ya medani za kijasusi hivyo hiyo haikuwa kazi kubwa kwa Hadasa bali kilichokuwa kimebaki ni utekelezaji.

Hivyo katika Ujasusi hatua ya awali ni Mafunzo. Hapa tayari alishapewa Hadasa. Hatua ya pili ni kufahamu eneo la kazi. Hapa tunamuona Mordekai(Jasusi) akipata taarifa muhimu kutoka Kwenye Kasri/Ikulu ya mfalme Ahasuero.

Hatua ya tatu ni maandalizi ya kufanya ujasusi. Hapa tunamuona Mordekai akimuandaa Hadasa kwa ajili ya kazi maalumu ambayo ni kutafuta taarifa kwa maslahi ya taifa. Hatua hii tunaona Hadasa akibalishwa jina na kuitwa ESTA lengo likiwa ni kuficha utambulisho(identity) wake kuwa yeye ana asili ya Uyahudi.

Katika kumpa jina Esta, bila shaka Mordekeai alizingatia maana na asili ya jina hilo. Kwanza, Esta ni jina lenye asili ya Kiajemi. Hii ingemsaidia kuficha kuwa yeye ni Myahudi. Pili, Esta ni jina la Kiajemi lililobeba maana 'Star' Yaani "Nyota". Hatua hii tunaona kuwa Mordekai anafoji majina ya Hadasa na kumuita Esta.

Hii pia inafanywa hata hivi leo katika medani za kijasusi. Majasusi baada ya kupewa mafunzo na serikali, serikali inatafuta target Area(nchi fulani), Baadaye humuandaa Jasusi kwa kufoji baadhi ya nyaraka za Jasusi husika. Hapa Jasusi anaweza kuwa na Passport zaidi ya nne zenye majina tofauti tofauti. Pia humsapoti kwa fedha, na dhana muhimu katika majukumu ya Kijasusi.

Ni kawaida kwa Jasusi kuwa na majina mengi kulingana na nchi husika anazoenda kufanya ujasusi wake. Jasusi sharti awe mwepesi kuendana na utamaduni wa mahali husika ikiwa ni pamoja na jina, lugha na uvaaji.

Sifa za Hadasa/Esta jasusi aliyeshindikana.
> Alikuwa amefunzwa vyema na Mordekai mjomba wake. Hivyo alikuwa na elimu ambao Mordekai aliamini atamudu kazi hiyo. Hapa tunaona elimu ni muhimu.

> Alikuwa ni Mwanamke mwenye maadili na nidhamu.
Maadili ya Hadasa/ Esta yandhihirishwa kwa namna mbili. Mosi, Maadili ya kimaumbile hapa tunaona alikuwa na bikra. Hii ni kusema kama asingekuwa bikra basi kazi hii ya ujasusi asingeipata. Kumbuka Mfalme alitaka waitwe wanawake wenye bikra. Kwa zamani bikra ilikuwa ni heshima hata hivi leo ni heshima. Pili, alikuwa na maadili ya kitabia, hapa tunaona akiitikia wito wa Mordekai mjomba wake. Esta alikuwa na uwezo wa kukataa kwani haikuwa lazima bali lilikuwa ni ombi. Lakini kwa sababu ya nidhamu alikubali. Hii inatufundisha kuwa kazi ya kijasusi inahitaji watu wenye maadili na nidhamu kwa tamaduni zao na watu wao.

> Alikuwa mzuri sana.
Esta alikuwa mzuri sana hii ikamfanya awabwage wanawake wengine na yeye kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha Kuwa Malkia wa Shushan Ngomen. Hii inatufundisha kuwa wanawake wazuri ni muhimu katika masuala ya kijasusi. Tuliona hata Ufaransa jinsi Mfalme Loius XVI alivyoihairibu nchi kutokana na matumizi mabovu ya Malikia Marie Antoinette(Mu-Austria) hali iliyopelekea mapinduzi ( French Revolution, 1789). Kumbuka kwa kipindi kile Ufaransa ilikuwa na uadui na Austria. Tuachane na stori hii labda siku nyingine nitaielezea.

> Alikuwa na Akili sana
Esta baada ya kuwa Malikia alijua kucheza na akili ya Mfalme Ahasuero. Mpaka anafanikisha misheni mbili muhimu kwa taifa lake. Misheni ya kwanza, ni kuwachomea Bigthana na Tereshi ambao ni wasimamizi wa nyumba ya Mfalme waliotaka kumchongea Mordekai mjomba wake na Esta kwa Mfalme. Hii ndio ilikuwa misheni namba moja ya Esta. Wasimamizi hao waliuawa kwa amri ya Mfalme(Mfalme asijue kuwa ni hila za Malikia Esta na Mordekai Mjomba ake). Misheni ya pili aliyoifanya Esta ni kumchongea Hamani aliyepandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Maakida wa majimbo yote 127. Hamani alikuwa anataka kuwaangamiza wayahudi kisa na mkasa ni kutokana na Mordekai(Mjomba wa Esta) Alikataa kumsujudia kila alipokuwa akipita malangoni. Mfalme bila kujua hila za Esta akamuangamiza Hamani ambaye ni raia wake.

Kupitia kisa hiki yapo mengi sana ya kujifunza ikiwa tutachambua nukta kwa nukta. Lakini kwa vile muda ni mdogo na wengi wetu tuwavivu kusoma makala ndefu inabidi niishia hapa.

Lakini kabla Taikon sijamaliza ninayohaja ya kusema machache kuwa:

Ujasusi uliwasaidia Waisrael katika utawala wa Wamedi na Uajemi kipindi wakiwa mateka uhamishoni. Walikuwa wametawaliwa na kama watumwa. Lakini mara kadhaa Ujasusi umewasaidia kuwakomboa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hivi leo Taifa leTU bado lipo mateka, bado tupo chini ya ukoloni. Hakuna atakayebisha kile nikisemacho kuhusiana na ukoloni mamboleo. Sisi ni mateka wa kiuchumi kwa mabeberu kiasi kwamba bila mikopo serikali zetu zinashindwa kujiendesha.

Sisi ni Mateka wa Kiutamaduni. Hakuna asiyejua jinsi watu wetu walivyokuwa watumwa na utamaduni wa wazungu. Hilo lipo wazi kabisa. Imefikia hatua utamaduni wa wazungu unaonekana ni bora kuliko utamaduni wetu. Imefikia mtu asipojuwa utamaduni wa wazungu anachekwa na kutukanwa. Mathalan, Hivi Juzi niliwasikia watu wakimtukana na kumteta Waziri wa Elimu, Mhe. Joyce Ndalichako alivyoboronga kuzungumza kingereza. Ni kweli aliboronga lakini hakukuwa na sababu ya kumnanga ikiwa lengo sio kuonyesha umahiri wa lugha ya kingereza. Utamaduni wa mavazi, ndoa, chakula, ibada, n.k yote tupo matekani. Usishangae hata Mimi jina langu Robert limeniteka kwa sababu halina asili ya Unyamwezi ambalo ndio asili yangu.

Sisi ni Mateka wa Teknolojia, karibu kila teknolojia tunayoitumia haina asili ya kwetu. Hii ni dalili ya kutekwa.

Serikali inaowajibu wa kutumia mbinu mujarabu katika kudhibiti mambo haya. Ujasusi ndio msingi wa mambo yote.
Mbinu zinazopendekezwa na Taikon wa Fasihi ni kama ifuatavyo;

1. Kutumia Scholarship kama kete muhimu.
Serikali kupitia vyombo vyake vya wazi na siri ihakikishe wale wote wanaopewa Scholarship wapitie/watoke kwenye mikono ya serikali. Ihakikishe kijana yeyote anayeenda kusoma nje kwa Scholarship ya namna yoyote ile apewe mafunzo maalumu walau ya miezi mitatu ya uzalendo na kuipenda nchi. Mpango huu uwe wa siri kuepusha maadui kutambua hili. Nafahamu kuwa kupitia Scholarship nchi nyingi za Afrika zimeharibiwa vibaya mno. Kupitia scholarship wazungu wanajipatia double Agents wa masuala wa kijasusi wanaoiba taarifa zetu na kuzipeleka kwao.

Kupitia Scholarship tunaona teknolojia yetu ikizorota kutokana na Maprofesa wengi na wanasiasa wa juu waliopewa Scholarship kipindi cha nyuma kuzuia teknolojia yetu na kuruhusu teknolojia ya wenzetu iteke soko hapa nchini. Wazungu wanajua ikiwa nasi tutajua kutengeneza ndege, maagri, simu, madawa n.k basi soko lao lkitayumba na kudondoka. Hivyo huwatumia watu waliopewa scholarship ambao ni wataalamu au viongozi wakubwa nchini.

Huko kwenye dini, afya, elimu kote wameharibu. Sasa tunachopaswa kufanya sio kufunga mlango wa Scholarship bali kuutumia kwa manufaa ya taifa. Na hili litafanyika endapo kutakuwa na utaratibu maalumu wa kuwapeleka vijana kusoma nje ya nchi. Nani asiojua kuwa watetezi wa ushoga ni wale wale vijana waliosoma nje ya nchi, nani asiyejua kuwa watetezi wakubwa wa demokrasia isiyo na mipaka inayoleta mitafaruku nchi mbalimbali wengi wao wamesoma nje ya nchi, nani asiyejua walioanzisha vita barani Afrika wengi wao wamesoma Nje ya nchi. Na mambo yakiwazidia hukimbilia nchi zile zile zilizowafadhili.

2. Kutumia Migogoro ya nchi zingine kujiimarisha.
Moja ya mambo ambalo nchi yetu ilifeli ni hili. Kabla hatujachelewa kutambua hili ni bora niseme kuwa; Afrika haiwezi kuungana na kuwa kitu kimoja. Halikadhaliika na dunia. Jinsi tunavyohangaika kuungana ndivyo tunavyothibitisha kutengana. Dunia itaungana kama atatokea adui nje ya dunia. Pia hii itachukua muda mrefu kuungana.

Serikali itumie migogoro ya nchi zingine kujinufaisha. Hivyo ndivyo dunia inataka. Kuenda kinyume na kanuni hii ni kutafuta umasikini. Hakuna nchi duniani iliyoendelea bila kutumia migogoro ya nchi zingine. Lazima mmoja aumie ili mmoja afurahie. Hiyo ni kanuni ya dunia.

Utaratibu maalumu uandaliwe kama taifa hili lipo sirius. Kuzisogelea nchi zisizojitambua. Nchi ambazo raia wake ni wehu wanaogombana wenyewe kwa wenyewe wakati wao ni ndugu. Hatuwezi poteza muda kuwapatanisha ndugu wanaogombana. Upo msemo usemao, ndugu wakigombana chukua jembe ukalime. Sasa kisiasa hakuna kuwaacha bali unawatumia ili siku wakiwa na akili wakuheshimu baada ya kuwaibia vya kutosha. Mbinu mbili tutakazozitumia ni mbinu kijeshi( yaundwe makundi mawili, moja liwe linapatanisha, la pili liwe linagombanisha. Hapa matokeo yake ni machafuko)

Pia wapo wasanii ambao wataimba nyimbo na kuigiza filamu za matokeo ya migogoro katika nchi hizo. Filamu hizo zitapelekwa huko huko kwao wakaziangalie jinsi walivyo wajinga. Yawepo makampuni ya kusimamia jambo hili chini ya uangalizi wa serikali.

Kwa leo niishie hapa maana kuna watu wangu humu ni wavivu sana kusoma.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300 au 0711345431
 
Nimeipenda tatizo lakini Je! hao majasusi ni weledi kutosha kufanya hao? Wana ushindani katika nyanja tofauti tofauti? Kiuchumi, kisiasa, kitamaduni, kijamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli,lakini huoni kuwa una discourse informations ambazo zikitumika zitakuwa tayari zimekwisha fahamika?
 
Hivi Juzi niliwasikia watu wakimtukana na kumteta Waziri wa Elimu, Mhe. Joyce Ndalichako alivyoboronga kuzungumza kingereza. Ni kweli aliboronga lakini hakukuwa na sababu ya kumnanga ikiwa lengo sio kuonyesha umahiri wa lugha ya kingereza.
Ndalichako ana wadhifa gani ktk jamii? Jamii inatarajia nini kutoka kwake? Taaluma yake iko vipi?
 
Hivi Juzi niliwasikia watu wakimtukana na kumteta Waziri wa Elimu, Mhe. Joyce Ndalichako alivyoboronga kuzungumza kingereza. Ni kweli aliboronga lakini hakukuwa na sababu ya kumnanga ikiwa lengo sio kuonyesha umahiri wa lugha ya kingereza.
Ndalichako ana wadhifa gani ktk jamii? Jamii inatarajia nini kutoka kwake? Taaluma yake iko vipi?
 
Ukiangalia Movie kama White House Down na London Has Fallen hata ukiwa Mtanzania unajikuta tu umepayuka tu USA Baby!!!

Point yangu ni kuwa kama sanaa itatumika ipasavyo tunaweza tukarudisha tena ari ya uzalendo. Ifike mahali serikali itoe support ya kueleweka kwenye sekta ya sanaa. Kwa mfano utaratibu wa kutumia sare za jeshi, mahakama na nyenzo nyingine pia ungeangaliwa upya. Just imagine tungekuwa na movie ikionesha makomando wetu walivyofanya operesheni kumuondoa yule rais kule Comoro. Ingekuwa amaizing sana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom