Mike sikawa afariki dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mike sikawa afariki dunia

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mwawado, Nov 19, 2008.

 1. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mwandishi wa Habari wa siku nyingi Mike Sikawa (55) amefariki Dunia,Nyumbani kwake Njiro - Arusha siku ya Jumatatu (17.11.2008).Marehemu Sikawa amefarikiki baada ya kusumbuliwa na Ugonjwa wa Kisukari kwa muda mrefu.

  Katika uhai wake amewahi kufanya kazi Katika kampuni ya magazeti ya serikali (TSN),Pia amewahi kuwa Mtangazaji wa BBC Idhaa ya Kiswahili huko Johannesburg - Afrika kusini.Marehemu ameacha mke na watoto wawili.(wanaishi South Afrika).Mazishi ya marehemu yatakuwa kwao Arumeru Arusha...Mwenyezi Mungu amlaze mahali Pema Peponi!!
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hata katika magazeti sijaona watu hawatilii mkazo lakini poleni wahusika wa msiba huu , sijui jk akitoka huko alipo ataenda katika msiba ngoja tuone
   
 3. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Shy !,Tumeipeleka habari hii kwenye magazeti...itaonekana kama ilivyo chini
  Mike Sikawa wa BBC afariki dunia

  MTANGAZAJI wa idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Mike Sikawa (55) ,amefariki dunia jana mchana baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kisukari.

  Sikawa, ambaye pia aliwahi kufanya kazi katika Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) inayomiliki magazeti ya Daily News na HabariLeo, alifariki dunia juzi majira ya saa 8.47 mchana nyumbani kwake Njiro, nje kidogo ya mji wa Arusha.

  Kwa mujibu wa mdogo wake marehemu, Mchungaji Charles Sikawa, ndugu yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu na kutokewa na kidonda mguuni.
  Mchungaji huyo alisema ndugu yake alipata matibabu katika hospitali mbalimbali hapa nchini ikiwamo AICC, KCMC, St. Thomas na Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili iliyoko Dar es Salaam lakini hakupata nafuu yoyote.

  Alisema ilifika wakati nusura akatwe mguu uliokuwa na kidonda lakini madaktari walifanikiwa kukwangua nyama ya mguu wa kidonda lakini haikuweza kusaidia.
  Mchungaji huyo aliendelea kusema kuwa baada ya kuhangaika kwa muda mrefu katika hospitali mbalimbali hapa nchini na kushindwa kupata nafuu, Sikawa alikuwa akipata matibabu akiwa nyumbani kwake hadi alipofikwa na mauti.

  Alizaliwa King'ori wilayani Arumeru mkoani Arusha na kusoma elimu ya msingi katika eneo hilo kabla ya kufaulu na kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Ilboru na Mzumbe ya mkoani Morogoro.

  Katika miaka ya 1970, aliajiriwa katika kampuni ya TSN kama mwandishi wa kawaida na baadaye kujiunga na idhaa ya Kiswahili ya BBC kama mtangazaji. Ameacha mjane na watoto wawili ambao wako Amerika ya Kusini.

  Mipango ya maziko inasubiri ndugu, jamaa na marafiki walioko nje ya mkoa wa Arusha na sehemu zote alizofanyia kazi.

  Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ametuma salamu za rambimbi kutokana na kifo cha mwandishi huyo na kuelezea jinsi alivyoguswa na msiba huo.

  Dk. Migiro alisema alipoteuliwa kushika wadhifa huo katika UN, Sikawa alikuwa mwandishi wa kwanza kumtafuta kwa ajili ya kumhoji juu ya uteuzi huo.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 19, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Poleni na msiba wafiwa wote, Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Amina.
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Rest in peace Mike.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mungu amrehemu Mike Sikawa na pole wafiwa wote
   
 7. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi aliyemuumba Mike Sikawa, hatimaye amemrudisha kwake.
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen.

  Poleni wafiwa wote, Mwenyezi Mungu awape nguvu na uvumilivu wakati huu mgumu wa majonzi.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwawado,
  Nimeipokea habari hii kwa masikitiko makubwa. Nilimfahamu Mike Sikawa kwa muda mrefu. Katika ziara yake hapa Marekani alinipigia simu akiwa ubalozini na nikamchukua nyumbani kwangu. KInachonisikitisha ni kwamba he died too young. 55 is a very young age, lakini mapenzi ya mwenyezi Mungu hayana makosa. I will miss him and may his family find refuge in the fact that he was loved by many.
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  RIP Mike Sikawa
   
 10. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ilikuwa inatia raha sana kusikiliza BBC. RIP brother.....
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  he was one of our famous son..sikujuwa kama ni mtanzania...nilifikiri ni m south ..or else...sijuwi alikuwa attached south..?maana yupo muda sana huko tangu enzi pasipoti zetu zimeandikwa kuwa huwezi kwenda south...jamani tupeni wasifu muruwa wa mike.....

  R.I.P
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mara nyingi hawa ndugu zetu wakati fulani wanapoandika habari huwa hawafanyi research hata kidogo. Ndio maana JF will always be first. Sina hakika kama kweli huyu mheshimiwa ameacha mjane Amerika ya Kusini
   
 13. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  duh! noma tupu
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,600
  Trophy Points: 280
  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN na awape nguvu, subira na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao.
   
 15. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  RIP Man Mike Sikawa...........! Kazi ya Mungu haina makosa, jina la bwana lihimidiwe, Milele na milele amina!
   
 16. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nafikiri ni Afrika ya Kusini....kidole cha ndugu yetu kiliteleza!
   
 17. I

  Iddi Rajab Member

  #17
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu aipumzishe kwa Amani Roho ya Marehemu Mike Sikawa na awape nguvu ya Kuhimili Msiba huu ndugu na jamaa zake wote. Aamin.
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Poleni wafiwa na wanataaluma wenzake. Aliimudu sana taaluma hii.
   
 19. L

  Lione Senior Member

  #19
  Nov 20, 2008
  Joined: Dec 1, 2007
  Messages: 115
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  They have sayed it all,
  rip mike sikawa
   
 20. M

  Masatu JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  RIP Sikawa
   
Loading...