Mike McKee wa JamiiForums tunaomba utufafanulie hili la OGP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mike McKee wa JamiiForums tunaomba utufafanulie hili la OGP

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Faru Kabula, Mar 26, 2012.

 1. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa ninaangalia kipindi cha Changamoto cha Mlimani TV na kukutana na mjadala uliowahusu wadau kadhaa akiwamo Mike McKee wa JamiiForums (kama alivyojitambulisha mwenyewe). Mjadala uliokuwapo mezani ulihusu Mpango wa kuendesha shughuli za serikali kwa uwazi (Open Government Partnership - OGP).

  Kwa kuwa Mike alibeba idea ambayo alikuwa anaitetea kwa kutumia support ya wingi wa members wa JF, na kwa kuwa mimi ni mmojawapo kati ya hao members wengi wa JamiiForums, nimeona si vibaya nikajua kwa undani idea yake hiyo ilihusu nini zaidi. Kwa kuwa suala lenyewe linahusu uwazi, sitegemei kama mkuu atatunyima kutupa hizo information.

  Nawasilisha ombi langu

  ======

  Majibu

  =======

   
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Arifu nami nina maswali mengi na nategemea bwana mdogo mike atatupa update......liel swali lake kama halikujibiwa vizuri maana yule mzee kama alimuuzia chai mike.....

  mike.....OGP ni kimdudu gani?
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  yeah alete nasi tujiridhishe
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  tumpe kamuda kidogo anaanda power point presentation
   
 5. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Oooh i didnt see this,
  Mike hebu tupe hii kitu kwa undani
   
 6. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Natamani nibonyeze kile kitufe cha REPORT ABUSE ili Mods waiangalie haraka hii thread, halafu wakikuta ni ya kawaida wamshtue mwenzao atupe majibu. Au kuna njia nyingine ya kumshtua mtu aufikie mjadala?
   
 7. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Jabulani,

  Kwanza nilialikwa kama mdao wa Maswala ya Mtandao. Na pia kwasababu nina idea kidogo ya jinsi hii program ya OGP inavyofanya kazi. Mimi wala JF sio wenye hiii initiative, Ni serikali.

  Maelezo kuhusu hii program yanapatikana katika website yao. www.data.go.tz

  Ila nitaelezea kiufupi.

  Tanzania imeridhia kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership - OGP). Mpango huu ni juhudi za kimataifa katika kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji wa huduma bora.


  Mpango huu ulizinduliwa rasmi na Viongozi wa Nchi za Marekani, Mexico, Norway, Afrika ya Kusini, Indonesia na Uingereza tarehe 20 Septemba, 2011 wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. Kwa kutambua umuhimu wa Mpango huu, Tanzania imeridhia kujiunga nao. Hadi sasa nchi nyingine 37 zimeridhia kujiunga zikiwemo nchi nne (4) kutoka Bara la Afrika ambazo ni Afrika ya Kusini, Ghana, Kenya na Liberia.

  Kwa lugha nyepesi ni kwamba huwa serikali kila mwezi june inapeleka makadirio ya mapato na matumizi bungeni. Lakini sisi wananchi huwa tunaona zile figures kubwa kiujumla mfano, Mishahara billion 20, au posho billion 30 au furniture billion 2. Hatuoni zaidi. Sasa kwa mpango huu, maana yake kwa kila bajeti ya wizara, unapewa nafasi ya kuona kila aina ya kifungu kidogo na pesa zilizotumiwa. Mfano utaweza kuona kiasi gani kilitumika kujenga madaraja, kampuni gani liyopewa na hata receipt ya malipo ya kila shillingi ya serikali inayotumika.

  Hizo information zote zitawekwa kwenye website ziwe wazi kwa kila mwananchi kuona. Kwahiyo kama mkitengewe fedha kwenye bajeti na zikatolewa hazina na mtu akalipwa na hakuna aliyefanya kazi, inakuwa rahisi kuona vitu vya aina hii.

  Sasa serikali yetu ndio ipo kwenye mchakato wa kuanza hii program ya kuweka vitu vyote hivo wazi. Na sio information za bajeti tuu, hata takwimu zote za Sensa ya watu na makazi. Kenya wamefanya hichi kitu angalia hapa. https://opendata.go.ke/

  Nilichokuwa nasupport ni utekelezaji wake. Sababu kubwa pia ya serikali kuamua kutekeleza hii program ni kwamba wahisani (donors) wanapotoa pesa yao, inakuwa rahisi kwa wao kufuatilia kama kweli pesa waliotoa imefanya kazi. Naamini presure kubwa inatoka kwa hizo nchi kwa tanzania kutekeleza hii program. Lakini pia ni nzuri kwa wananchi.

  Sasa changamoto kubwa hapa ni je, hizo taarifa zitakuwa zikitolewa kwa utaratibu gani? Na information zipi ni Usalama wa Taifa? Kwa kusolve tatizo hilo Tanzania itapitisha muuswada na kuwa sheria naathani mwaka huu, utakaoipa hii program nguvu ya kuweka kutekelezeka. Mfano sheria itasema kila miezi mitatu lazima kila wizara i-submit report yake kwa OPEN DATA ili ziwekwe kwenye website. Ila kwenye hii sheria ndio sisi wananchi tunatakiwa tuwe wakati kwamba turequest vitu vingi viwe open, sio wavifunge kwa kutumia dhana ya usalama wa taifa.

  Vitu vingine vitakavyoingizwa kwenye mpango huu ni wamiliki wa viwanja vyote tanzania na majira yao. Na mambo mengine mawili matatu nimesahahu.
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  always Kenya wako safi kuliko tz....yao inaeleweka....
  nalichukia hilo neno.....
   
 9. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa kujitokeza kutoa mwangaza, ngoja kwanza niziangalie hizo tovuti mbili ulizotoa ili niwe ktk position ya kupima uelewa wangu kwenye hili. Nisipoelewa nitarudi kwako. Thanks
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Siku hizi wanaitwa Uhasama wa Taifa.
   
 11. Kagondo

  Kagondo JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2016
  Joined: Jun 6, 2016
  Messages: 291
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  kwakweli na mimi bado najiuliza kama ushirikishwaji wa wananchi kwa njia hii unafaa
   
Loading...