Mikate ya maji iliyochanganywa na kuku

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Habari wadau wa mapishi, wapenda misosi mitamu.

Leo nawaletea pishi hili tamu sana baada ya kulionja nikaona niwaletee na nyie ndugu zangu wa JF ili mkapike nanyi mfaidi kama mimi nilivyofaidi.

Basi nisiwachoshe naomba mfatane nami katika maandalizi haya mpaka mtatoa kitu murua.

Viamba upishi

Vipande vidogo vya vidari vya kuku-mbatata/viazi, tangawizi,thoum,chumvi,ndimu,vinegar, unga wa uzile/bizari ya pilau-mdalasini-pilipili manga-giligilani. Viungo viwe kiasi kutokana na vidari ulivyonavyo.

Maandalizi

Chukua sufuria linalotosha vidari vyako na utie vitu vyote hapo juu na uchemshe jikoni kwa moto wa wastani .

Wakati vinachemka katakata nyembamba sana kwa urefu carrot-pilipili mboga-beetroot-vitunguu maji kisha kamua maji yake yote yatoke, kisha usiyamwage yahifadhi.

Kuku akishaiva maji yote yakikauka mimina katika sinia acha mpaka ipoe. Kisha weka mboga zote changanya vizuri.

Kuandaa mikate ya maji

Tumia blender au mwiko na sufuria changanya kikombe 1 cha chai unga wa ngano mfuto,chumvi,mayai 2 na maji ya mboga ulizokamua pamoja na maji ya kawaida upate kikombe 1. Pika mikate upande mmoja tu isikauke sana na isiwe mikavu na usigeuze iwe myembamba.

Toa weka kwenye sinia mpaka umalize kupika yote. Utapata mikate 9 kwa kipimo cha frying pana sana ila unaweza kuipika midogo au kwa kiasi ya ukubwa unavyopenda ila iwe membamba.

Kwa kila mkate 1 weka mchanganyiko wa kuku vijiko 2 vya supu kisha funga sokota pembeni isiwe wazi.{funga kama unavyofunga sambusa lakini iwe pembe nne }

Ukimaliza yote,zungusha kwenye unga wa ngano. kisha kwenye mchanganyiko wa mayai upige na kotmiri uzikate ndogo sana pamoja na pilipili manga kisha zungurusha kwenye tambi nyembamba sana ambazo uzivunje ziwe ndogo sana. Ukikosa tumia chenga za mikate ya toast.

Kaanga kwenye mafuta kiasi sio mengi. Ziache zipoe kwa masaa ndio ukate hazitavurugika. Kula kwa tomato au chilly sauce ukipenda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom