Mikataba ya madini na nishati iletwe bungeni sasa ijadiliwe!!

mkulima gwakikolo

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
1,767
2,854
Wadau ,mi naona msimamo wa Mh Rais juu ya Mchanga Wa madini..uwe ndy chachu ya wabunge wote kuitaka serikari kuleta mikataba yote iliyopita kidhalimu au kifisadi ijadiliwe wananch wajue.Wabunge wote Kwa ujumla wao walisemee hili...Vinginevo neno tunampongeza Rais waache mana kumpongeza ni kumwacha apigane pekee yake...Wabunge hawakuchaguliwa kupongeza Bali kutetea maslahi ya walowachagua na kuishauri na kusmamia Serikari....
 
Kwani ikijadiliwa wewe utapata nini? Au unaropoka ?
 
Badala ya kushauri iundwe timu ya wataalam kwa ajili ya kupitia hiyo mikataba wewe unashauri ipelekwe kwa hao vilazaz kana kwamba kuna chochote cha maana wamewahi kufanya, zaidi ya kutumbua pesa za makalio
 
Katiba Ya JMT, inatamka kuwa mikataba itajadiliwa na kuridhiwa na Bunge iwapo mikataba hiyo ina masharti kwamba Bunge liridhie. kwa hiyo, mikataba yote kati ya serikali na wawekezaji, hailazimishwi kikatiba kupitiwa na Bunge. Kwa Hiyo, Mikataba Hiyo Ina Nguvu Kushinda Katiba Ya Nchi. Yaan Inaweza Ikasainiwa Hata Ndan Ya Guest Bubu Pale Tandale
 
Hao wa bungeni wanaojua kusoma na kuandika?

Halafu ccm walisaini katika mikataba na kuapa kutoipeleka bungeni wala kuiweka wazi,wanajua wakiiweka wazi wanashtakiwa
 
Mikataba sio ngoma ya sindimba au kale ka usemi "kidumu chama cha mapinduzi"!huko bungeni nani ataelewa ?kina ndiiiioooo au ?
 
Hiyo mikataba ikipelekwa bungeni ndio inajadiliwa na watu kama Msukuma, Maji Marefu, Lusinde na Godluck etc.
 
Badala ya kushauri iundwe timu ya wataalam kwa ajili ya kupitia hiyo mikataba wewe unashauri ipelekwe kwa hao vilazaz kana kwamba kuna chochote cha maana wamewahi kufanya, zaidi ya kutumbua pesa za makalio

Hao wataam nyenze si ndio hao walitumwa wakaleta umbea kwamba lazima mchanga uende majuu!

Au umesahau ya maprofessor nyenze kama

Lipumba.....na uchafuzi wa CUF

Mhongo na kufukuzwa kila wakati

Mkumbo na maajabu ya cdm...m1, m2 nk....ACT-wazalendo kabla ya kupiga u-turn kuingia ccm

Wanasheria mkaa kama mwawembeee ...mwalimu wa sheria mnafiki asiyesimamia ukweli

Nahuyu wasasa kabudi aliyeshiriki kuunda katiba ya warioba ghafla kala pindu......

wataalam gani hasa?.........
 
Katiba Ya JMT, inatamka kuwa mikataba itajadiliwa na kuridhiwa na Bunge iwapo mikataba hiyo ina masharti kwamba Bunge liridhie. kwa hiyo, mikataba yote kati ya serikali na wawekezaji, hailazimishwi kikatiba kupitiwa na Bunge. Kwa Hiyo, Mikataba Hiyo Ina Nguvu Kushinda Katiba Ya Nchi. Yaan Inaweza Ikasainiwa Hata Ndan Ya Guest Bubu Pale Tandale
Hiyo ndiyo CCM.
 
Hiyo mikataba ikipelekwa bungeni ndio inajadiliwa na watu kama Msukuma, Maji Marefu, Lusinde na Godluck etc.

Bora kuliko washenzi wanaobeba Phd kwenye mabegi nakusema kwa kila sh. 100 tulipwe sh. 3 na sh. 97 ziende ulaya

Lusinde au msukuma hawawezi kukubali ushenzi huo watasimamia 50/50.....niwasomi wenu tu ndio wanatuuza .
 
Watajua hata kilichoandikwa kwenye mikataba?
 
Back
Top Bottom