Mikataba ya Madini inasemaje kuhusu michanga ya dhahabu?

Kama TMAA wamecheza mchezo mchafu na wawekezaji,basi wa kuwajibishwa sio TMAA peke yao.Kuuzuia mchango inaweza hesabika kama kumwajibisha m wekezaji Vilevile.

Sawa mkuu ila agizo la kusafirishwa mchanga nje halikutolewa eti kwa sababu mchanga ulikuwa unachanganywa na gold bars sidhani.

Rais alisema ni kwamba unapopelekwa nje kinachoenda kupatikana tunaambiwa tu na inawezekana sicho...kitu ambacho mm sikubaliani nacho Kabisa.
 
Suala si hatutaki kuamini suala ni je makampuni haya yanatekeleza makubaliano au wameenda kinyume na makubaliano?
Hayatekelezi ndio maana tumezuia mchanga.subiri ufunguliwe halafu utalinganishwa na hiyo report ya huo mchanga,utazimia wewe
 
Usiwe na hofu tushazuia kontena zote tunapiga hesabu toka zilipoanza kusafirishwa.kitaeleweka tu
Tatizo lako bwana kapombe haya masuala unayaongelea kishabiki sana kuliko uhalisia wenyewe. Nakuhakikishia makontena yalikuwa yanasafirishwa kwa kufuata taratibu zote za makubaliano baina ya serikali na mchimbaji. Kama kuna namna yeyote ya kuvunja makubaliano ambayo serikali inataka kufanya basi tujiandae kubeba huo msalaba. Tupo hapa mkuu utakuja kuniambia.
 
Jf ya sasa imebadilika sana, yaan, nlitaraji MTU mmoja angeleta nyaraka za mikataba ya madin nw hakuna, hum ndan kwa sasa kuna watt wengi zaidi kuliko watu wazima...

Ambao wanataka mabadiliko,kwa shortcat way.....
 
Si umemsikia Ndugai amesema watapitia upya mikataba na watapendekeza kwa serikali au hujasoma mkutano wake na waandishi wa habari
Ndugai ana akili ndo maana kasema watapitia mikataba ila nyie kwa sababu akili zenu ndogo mnakurupuka.
 
Asante kwa majibu yako ya kiyakinifu mkuu.Kinachogomba ni false declaration.Mzigo unaoandikwa unakuwa na thamani ya chini sana,kuliko ukweli halisi hivi ndivyo tunavyopigwa hata wakati wa kuingiza makontena,kwenye mafuta hali ni hiyo hiyo.Unakumbuka kituo cha kupigia hesabu dhahabu yetu kilikuwa London!Bwana Mramba na Yona walivyotumia fursa?
Sasa hicho ndio hatutaki kiendelee,na sidhani kama huo mchanga una thamani kubwa kuliko dhahabu iliopatikana so far

Ndo maana nilikuwambia kama kuna kitu kama hicho wa kushika shati ni maafsa wa TMAA kwani wao ndo jicho letu huko migodini.
 
Ndugai ana akili ndo maana kasema watapitia mikataba ila nyie kwa sababu akili zenu ndogo mnakurupuka.
Hayo mawazo yako mkuu.aliosema Ndugai ni yatokanayo tu.Kwamba kama kweli mchanga una tatizo (under estimated) basi wao kama Bunge watapitia mikataba na kupendekeza marekebisho/maboresho ya mikataba ya madini
Hya yote yalikuwa yanapigiwa kelele na chadema/zitto
 
Hiyo ni nadharia mkuu.ukweli ni kuwa tunacholipwa ni kidogo mno kwa sababu madini yanashushwa thamani
Swala la kulipwa kidogo au si kidogo hilo mimi nawewe hatuwezi kujua kwa sababu serikali na wataalamu wake ndo wanajua wanapokea fedha kiasi gani kwenye hiyo biashara.
 
Hayatekelezi kivipi?
Makampuni ya uchimbaji dhahabu hayatekelezi mkataba,kwa kudanganya kuhusu mchanga,ripoiti inaonesha ni kiasi kidogo ili tulipwe kidogo.
Kwani umesahau kuwa TRA wanaidai ACACIA Bilioni 40 za kodi baada ya kufanya udanganyifu?
Wanakuwa na ripoti mbili za ukaguzi wa mahesabu,ripoti ya Tanzania inaonesha kuwa wamekula hasara au wamepata faida kiduuchu ili wasilipe kodi au walipe kodi ndogo.
Ripoti inayopelekwa kwenye soko la hisa la London stock exchange ndio ripoti halisi inaonesha faida kubwa waliovuna,ili hisa zao ziuzwe kwa bei kubwa
Kilichotokea,zile ripoti zao wanazowakilisha LSE,ndio zimetumika kukokotoa kodi,Jamaa wanadaiwa Bilioni 40,na lazima watazitema kwa sababu ndio faida halisi ,sasa mijizi kama hiyo utaiamini vipi kwenye mchanga.
Ingekuwa Ujerumani huyo CEO sijui vice president angefungwa
 
Hayo mawazo yako mkuu.aliosema Ndugai ni yatokanayo tu.Kwamba kama kweli mchanga una tatizo (under estimated) basi wao kama Bunge watapitia mikataba na kupendekeza marekebisho/maboresho ya mikataba ya madini
Hya yote yalikuwa yanapigiwa kelele na chadema/zitto
Tusubiri mkuu muda ni Hakeem mzuri sana.time will tell
 
Si umemsikia Ndugai amesema watapitia upya mikataba na watapendekeza kwa serikali au hujasoma mkutano wake na waandishi wa habari

Mkuu hii si kauli ya kwanza kuhusu kupitia hiyo mikataba. Kauli hii imekuwa ikitolewa mara kwa mara pindi kunapokuwa na shinikizo kubwa kuhusu utata wa mikataba hiyo.
 
Makampuni ya uchimbaji dhahabu hayatekelezi mkataba,kwa kudanganya kuhusu mchanga,ripoiti inaonesha ni kiasi kidogo ili tulipwe kidogo.
Kwani umesahau kuwa TRA wanaidai ACACIA Bilioni 40 za kodi baada ya kufanya udanganyifu?
Wanakuwa na ripoti mbili za ukaguzi wa mahesabu,ripoti ya Tanzania inaonesha kuwa wamekula hasara au wamepata faida kiduuchu ili wasilipe kodi au walipe kodi ndogo.
Ripoti inayopelekwa kwenye soko la hisa la London stock exchange ndio ripoti halisi inaonesha faida kubwa waliovuna,ili hisa zao ziuzwe kwa bei kubwa
Kilichotokea,zile ripoti zao wanazowakilisha LSE,ndio zimetumika kukokotoa kodi,Jamaa wanadaiwa Bilioni 40,na lazima watazitema kwa sababu ndio faida halisi ,sasa mijizi kama hiyo utaiamini vipi kwenye mchanga.
Ingekuwa Ujerumani huyo CEO sijui vice president angefungwa
Kwahiyo mkuu Kapombe kupeleka mchanga nje si tatizo serikali inaruhusu lakini shida ni udanganyifu siyo?
 
Kuna kitu hukielewi kuhusu samaki wa magufuli na siwezi kiandika hapa sababu ni siri ila kwa ufupi tu samaki wa magufuli ndio walimpa ujiko magufuli kuteuliwa kugombea uraisi.usilolijua ni kama usiku WA giza wewe Kama source ya taarifa za samaki wa magufuli ni magazeti jua huna taarifa sahihi .Samaki wa magufuli mtu aweza andika hata kitabu cha kurasa elfu. Mimi nilimpa kura sababu ya hao samaki wa magufuli.Muombe mungu akusamehe tu
Tuambie kuhusu hao samaki wa magu,yawezekana kuna kitu unakijua tusichokijua
 
Swala la kulipwa kidogo au si kidogo hilo mimi nawewe hatuwezi kujua kwa sababu serikali na wataalamu wake ndo wanajua wanapokea fedha kiasi gani kwenye hiyo biashara.
Kuna wazalendo wamechoka,wamemtonya mkulu.Si unafahamu watu wa kitengo wapo kwenye kila kwenye kampuni ilioajiri zaidi ya watu watano?
 
Mikataba haisemi chochote kuhusu mchanga.mchanga unachukuliwa kama vile machicha baada ya kutengeneza pombe ni ya kumwaga tu.
Ndio maana mchanga ukipelekwa nje hatulipwi kwa sababu hakuna anaejua kimetoka kitu gani baada ya kuchakatwa na kina thamani gani.
Kwa nini uogope kushitakiwa wakati sie ndio tunatakiwa tushitaki kwa kuibiwa mchanga miaka yote hii 20 ya kuchimba dhahabu

Hiyo mikataba uliipata wapi? Kwa nini spika anataka irudiwe na kuhakikiwa upya? kwa nini kabla ya mchanga kutoka getini mamlaka za serikali huakikisha kodi na mrahaba wa asilimia 4 zimelipwa ndiyo mchanga utoke?
 
Back
Top Bottom